Ndugai: Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uendelee, Dkt. Magufuli alishauriwa vibaya

Ndugai: Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uendelee, Dkt. Magufuli alishauriwa vibaya

Spika wa Bunge ameshauri mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo uendelee kwa sababu Magufuli alishauriwa vibaya, hii ni baada ya kamati ya Bunge ya bajeti kushauri kuwa serikali iangalie kuhusu kuendelea na mradi huo.

Ndugai amesema kuwa mradi huo utakuwa na faida kubwa kwa Watanzania na tukichelewa hatutauta tena.

Magufuli alisema mradi huo ulikuwa ni hasara kwani ulikuwa na masharti magumu ikiwemo ya kuzuia bandari yoyote kuendelezwa, wala TRA kukusanya kodi na kupewa lease kwa miaka 99.

Pia soma: Spika Job Ndugai: Kutokana na masharti ya Mradi wa Bandari Bagamoyo, ni sahihi Serikali kuusitisha
Nimeamini kwamba wale wanao kwambia tuko nyuma yako unaweza kugeuka na usiwakute
 
Nimecheka spika alichoongea Ndugai kwenye Clip anasema ukiangalia presentation waliyotufanyia wachina kule kwao ule mradi ni mzuri sana!!!

Nimweleweshe mradi mzuri huuangalii kwenye presentation nenda kwenye mkataba huko ndiko utajua ni mzuri au la
Tuonyesheni mkataba

Pili anasena ni kosa kuanza kujenga reli kabla ya bandari!!! kwa hiyo unaanza kujenga stendi ya mabasi kabla ya barabara? Mfano hakuna barabara hata moja ya kutoka Dar kwenda mkoa wowote kwa hiyo wewe cha kwanza utaanza kujenga stendi ya ubungo wakati huna hata barabara moja?

Bandari sisi tunayo tayari hilo la kusema tumetanguliza mkokoteni mbele ya punda anayetakiwa yeye kuwa mbele na mkokoteni nyuma sio kweli .Sisi bandari tunayo tayari huo mfano hautuhusu walitakiwa wawajibu hivyo hao wachinadio tu ku swallow everything!

Naanza kunusa harufu ya rushwa Ndugai na kundi lake China walipoenda kuna kitu waliahidiwa au walikula rushwa!!
Huwezi kuukubali mradi kwa ka kipresentation tu kadogio ka dakika chache ka power point bila kuona mkataba
Mkuu huu ndio ukweli wenyewe, hawa watu tayari wanataka kutumia fursa kupiga hela enzi za ku sign mikataba mibovu yatari zinaanza kurejeshwa kwa tamaa za hawa watu.
Pili naona Kama vile wamemsoma Mama kuwa ni mtu wa aina fulani fulani Sasa wamegundua udhaifu wake tayari . Wanafanya hivi kwa kujipendekeza wapate kuaminiwa lakini pia wakitumia mwanya huo kupiga hela kwenye miradi mbalimbali hata Kama ni mibovu.

Mama asipokuwa makini na hawa watu atadanganywa mengi kisha watakaa pembeni kumcheka.
 
Unafiki plus

Wangesubiri ata mwaka upite ndiyo waanze unafiki

Ata matanga hayajaisha wanaanza kumnanga shujaa wa Africa
Mkuu hebu Acha utani kabisa , usubiri mwaka tena , unacheza kulingana na mdundo wa Ngoma Mzee Baba , mtu akifa anakuwa helpless Mzee, wa kutomfanyia unafk ni Yesu tuu , wanadamu wenzetu hapa duniani tunashangiliana Kwa fursa mzee
 
Unafiki plus

Wangesubiri ata mwaka upite ndiyo waanze unafiki

Ata matanga hayajaisha wanaanza kumnanga shujaa wa Africa
sio unafiki, kwani nani hajui jiwe al
ifanya maamuzi mabaya ? angejenga bandali hiyo kwa pes alizoteketeza chato baada ya kuona masharti ya msaada magumu
 
Kuna wanasiasa ni wanafki balaa.Embu tujiulize Jiwe angekua hai ndugai angeshauri hivyo!?
 
Huu unafiki sio wa kuchekea, kwa namna hii kila kiongozi atakaekuja atakuwa anakuja na vipaumbele vyake na hawa kina Ndugai wataendelea kujipendekeza tu, kwa namna hii hiyo bandari ya Bagamoyo JK akifa nayo itakufa.
 
Naona ndugai kashakuwa msemaji wa serikali
 
Niliamini Ndugai angekua msaliti wa mwisho lakini daaah...Mwendazake anasalitiwa kwa kasi ya kimondo
 
Mbona sielewi elewi
Hata mimi mkuu......Nimejikuta nawaza hivi: Mzee wa MSoga amerudi kwa kishindo,...mkataba ukasainiwe Dubai huko kwa raha zao!
"Wapi Dr. MWAKYUSA, DR. JANABI,(sijuhi nimepatia jina, yule wa taasisi ya moyo ya Kikwete) Wapi Papa Mobimba mtu ya watu...hahahahaha"
NIMEAMINI HISTORIA KUMBE HUWA INA TABIA YA KUJIRUDIA!
 
Spika wa Bunge ameshauri mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo uendelee kwa sababu Magufuli alishauriwa vibaya, hii ni baada ya kamati ya Bunge ya bajeti kushauri kuwa serikali iangalie kuhusu kuendelea na mradi huo.

Ndugai amesema kuwa mradi huo utakuwa na faida kubwa kwa Watanzania na tukichelewa hatutauta tena.

Magufuli alisema mradi huo ulikuwa ni hasara kwani ulikuwa na masharti magumu ikiwemo ya kuzuia bandari yoyote kuendelezwa, wala TRA kukusanya kodi na kupewa lease kwa miaka 99.

Pia soma: Spika Job Ndugai: Kutokana na masharti ya Mradi wa Bandari Bagamoyo, ni sahihi Serikali kuusitisha
Taratibu nmeanza kuelewa
 
Kwani hao washauri walishikiwa Bunduki hadi kumshauri mwendazake vibaya??

Unaweza kuta washauri wale wale waliomshauri JPM kutotekeleza mradi kwamba hauna manufaa makubwa kwa Nchi ndiyo hao hao wanashauri mradi Mhe. Samia Suluhu kuutekeleza kwa kuwa wamegundua Una manufaa kwa Nchi mara hii.

Tanzania kinachotugharimu ni Unafiki, Woga na kuendekeza Majungu.

Imagine kama mradi ungetekelezwa 2016 leo hii si ingekuwa Meli zimeanza kushusha na mzigo hapo. Tumekubali kuyumbishwa na siasa uchwara hatimaye tumepoteza zaidi ya maTrilioni kwenye Ushuru na Kodi.
HApo kwenye bold....inaanzia kwenye familia, mtaani, makazini hadi TAiFA
 
Spika wa Bunge ameshauri mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo uendelee kwa sababu Magufuli alishauriwa vibaya, hii ni baada ya kamati ya Bunge ya bajeti kushauri kuwa serikali iangalie kuhusu kuendelea na mradi huo.

Ndugai amesema kuwa mradi huo utakuwa na faida kubwa kwa Watanzania na tukichelewa hatutauta tena.

Magufuli alisema mradi huo ulikuwa ni hasara kwani ulikuwa na masharti magumu ikiwemo ya kuzuia bandari yoyote kuendelezwa, wala TRA kukusanya kodi na kupewa lease kwa miaka 99.

Pia soma: Spika Job Ndugai: Kutokana na masharti ya Mradi wa Bandari Bagamoyo, ni sahihi Serikali kuusitisha

ama kweli ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko mwanasiasa kuingia katika ufalme wa mbinguni
 
Bado siamini kama Mkuu Ndugai ndio amesema hayo maneno ,ngoja nijipe muda kwanza.

Yesu akamjibu, “Nakuambia wewe Petro, kabla jogoo hajawika leo utakuwa umenikana mara tatu.”
 
Spika wa Bunge ameshauri mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo uendelee kwa sababu Magufuli alishauriwa vibaya, hii ni baada ya kamati ya Bunge ya bajeti kushauri kuwa serikali iangalie kuhusu kuendelea na mradi huo.

Ndugai amesema kuwa mradi huo utakuwa na faida kubwa kwa Watanzania na tukichelewa hatutauta tena.

Magufuli alisema mradi huo ulikuwa ni hasara kwani ulikuwa na masharti magumu ikiwemo ya kuzuia bandari yoyote kuendelezwa, wala TRA kukusanya kodi na kupewa lease kwa miaka 99.

Pia soma: Spika Job Ndugai: Kutokana na masharti ya Mradi wa Bandari Bagamoyo, ni sahihi Serikali kuusitisha

Ni unafiki wa kiwango cha PHD. Siungi mkono
 
Back
Top Bottom