Ndugai: Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uendelee, Dkt. Magufuli alishauriwa vibaya

Ndugai: Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uendelee, Dkt. Magufuli alishauriwa vibaya

Huo mkataba wa bandari ya Bagamoyo huyo Ndugai anayajua masharti yake?

Maana anaonekana ana tabia ya kudandia vitu tu ili awafurahishe mabosi wake.

Kuwa na mwanasiasa wa aina hii ndio maana tumeshindwa kuondokana na adui ujinga zaidi ya miaka 50 baada ya kupata uhuru.

Kama yeye kwa nafasi yake miaka yote bungeni bado mjinga, je wananchi wake kule Kongwa watakuwa na hali gani, ndio maana kila wakati wanaendelea kumchagua awe muwakilishi wao.
 
Yawezekana jamaa ana 10% kwenye huo mradi.

2019 pia aliupigia chapuo.

Ni muda muafaka hii mikataba iwe wazi kwa kila mtu kujionea kilichomo badala ya kuwaachia hawa wachonga ngenga watuhadithie.
 
Spika wa Bunge ameshauri mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo uendelee kwa sababu Magufuli alishauriwa vibaya, hii ni baada ya kamati ya Bunge ya bajeti kushauri kuwa serikali iangalie kuhusu kuendelea na mradi huo....
Ndugai Ana interest kwenye mradi huu. Ana maslahi mengi mno kwani watoto wake wapo China na wanasomeshwa bure! Na hata ukimchungulia vizuri mtagundua kuwa vijisenti alivyopiga kavifungia kwenye benki za China kwa kivuli Cha watoto wake waliopo huko!
Achinguzwe hata Kama walijiwekea Sheria ya kutokushtakiwa tutapiga kelele Hadi ifutwe!
 
Ieleweke, serikali haina hela, makusanyo yote ya mapato yanaenda kulipa madeni na kulipa mishahara na posho za safari. hivyo hawa watu hawana hela za kuiba, hapo wanachonga mzinga.

huyo speaker hapo waweza kuta ana taarifa hizo ndio akili za mama pia kuhusu bagamoyo, au la waweza kuta JK kageuka kuwa mshahuri mkuu wa mama, so kila kiumbe kinaanza kucheza ngoma zake za rushwa na ufisadi.

hapa tunazungumzia maandalizi ya ufisadi mkubwa kuwahi kutokea katika historia ya nchi.
 
Ieleweke, serikali haina hela, makusanyo yote ya mapato yanaenda kulipa madeni na kulipa mishahara na posho za safari. hivyo hawa watu hawana hela za kuiba, hapo wanachonga mzinga....
Kabisa naaona watu wanajiandaa kugawana nchi sasa, nina mashaka sana hata na Report ya CAG sasa
 
Ogopa sana watu wanao kushangilia na kukuunga mkono kwenye kila kitu.
Alafu kisha ndiyo wale wale kila siku wanabadilishana tu nafasi...Huku wakituachia mbegu mbaya ya tabia za kubadilika badilika...So pathetic!

Hata Mh. Mama Samia watamgeuka hivi hivi siku naye akifikia ukomo wake...They are there for their own interests...Aibu sana hii!
 
Ukiangalia wabunge karibia wote waliopitishwa na tume kimagumashi wengine bila kupingwa (hata kupigiwa kura za ndio/hapana) ndio walikuwa wanamsifia sana JPM hata alipokosea na ndio ghafla wamebadilika na kujionyesha kumuunga mkono Mama pamoja na kukigeuka kila alichokifanya mwendazake!...
Hapo ondoa CCM, tatizo ni la watanzania walio wengi maana hata huko CDM mambo ni yale yale, tumbo projects...
 
Hata Ndugai kamsaliti mwendazake....kazi kweli.
Hiki ni kirusi kinachotakiwa kuondolewa upesi sana. Matumizi yake ya pale bungeni tu yanaweza kumuondoa!!! Ukichunguza zaidi unaweza kugundua kuwa lazima ana interest kwenye huo mradi wa bagamoyo, inawezekana wachina walisha mpa chochote kwani kama mtakumbuka kuna wachina waliohusika na huo mradi waliwahi kumtembalea ofisini kwake!
 
Kwani hao washauri walishikiwa Bunduki hadi kumshauri mwendazake vibaya?

Unaweza kuta washauri wale wale waliomshauri JPM kutotekeleza mradi kwamba hauna manufaa makubwa kwa Nchi ndiyo hao hao wanashauri mradi Mhe. Samia Suluhu kuutekeleza kwa kuwa wamegundua Una manufaa kwa Nchi mara hii...
Ndicho nachosema, wamejaa kila mahali kuanzia chini mpaka juu...Hawa watu wakujipendekeza na kutengeneza CV za kwenda kupata viyoyozi badala ya kusaidia nchi na raia ili welfare ya kila moja ipande.

Hii ni hatari sana kwa taifa na kwa vizazi vyetu...Wemgi wamekuwepo kwenye mifumo miaka mingi wakirithishana tu nafasi kumbe lengo ni kuendeleza ubinafsi ambayo ndiyo gharama kwa taifa.
 
Spika wa Bunge ameshauri mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo uendelee kwa sababu Magufuli alishauriwa vibaya, hii ni baada ya kamati ya Bunge ya bajeti kushauri kuwa serikali iangalie kuhusu kuendelea na mradi huo...
Hao ndio waliokuwa wakimshauri vibaya magufuli magu alipotambuwa kwamba alikuwa na washauri hewa moyo umeshavimba wapinzani kina zito na lema walikuwa wanatowa ushauri mzuri tu lakini huyo ndugai ndiye aliyekuwa akiongoza kundi la wachumia tumbo kuwadhihaki na kuwaona hawapendi maendeleo.
 
Mama Samia kaa chonjo kuna kundi la wezi wanataka kurudi hewani kwa spidi ya mwewe hata arobaini haijaisha
YEHODA rafiki yangu (inabidi sasa nikuite hivyo), kwa sababu naona maumivu ni yetu sote, mimi na wewe, hata kama ni kwa sababu tofauti.

Nina mashaka sana na tumaini lako katika mstari huo hapo jjuu unapoliweka. Sipaoni- lakini natamani niwe mwenye hofu potofu; lakini nina hofu sana na yajayo kesho.

Huenda hili ndilo litakalotuunganisha wewe na mimi; lakini acha tuvute subira.
 
Hata Ndugai kamsaliti mwendazake....kazi kweli.
Waimba mapambio wote watajulikana tu.
Siku zote nasema mgogo yeyote ni shida.
1.john malecela alibadiri dini ili apewe urasi maana aliona wakristo wenzie ni wachache
2. Kibajaji kichwa mbovu kabia
Huyu ndugae ndiyo buyu tupu
 
Spika wa Bunge ameshauri mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo uendelee kwa sababu Magufuli alishauriwa vibaya, hii ni baada ya kamati ya Bunge ya bajeti kushauri kuwa serikali iangalie kuhusu kuendelea na mradi huo....
Japo najua ni utovu wa nidhamu, ila kiukweli huyu jamaa atakua ni mlevi, kwa sababu Hayati JPM alikwishasema, ni mlevi tu ndio anaweza akayakubali masharti ya mradi huo. Hili jamaa ni linafiki sijapatabona hapa duniani, damn it!!!!
 
Kumaliza utata mkataba huo uwekwe wazi uanikwe hadharani. Wazee akina Ndugai musije achia vizazi vijavyo mizigo isiyowahusu si vizuri kurithisha kizazi kingine zigo Wanamchi tunaomba uwekwe wazi sababu ni wa miaka mingi pengine wote tuliopo hatutakuwepo duniani tutalaaniwa na vizazi vijavyo...
Kama sisi tulivyorithishwa zigo la IPTL kkmmmmmmk zao!!!!
 
Back
Top Bottom