Ndugu Covax ninawajua wanaume wengi waliopewa mitaji na wake zao lakini wakashindwa Kufanya biashara. Hiyo dhana yako sio sahihi

Ndugu Covax ninawajua wanaume wengi waliopewa mitaji na wake zao lakini wakashindwa Kufanya biashara. Hiyo dhana yako sio sahihi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Nimesoma Uzi WA ndugu Covax unaowakataza kama siô kuwatahadharisha Wanaume kutokuwaanzishia Wake au Wenza waô biashara kwani lazima itafilisika.

Ushauri wa Covax siô Sahihi Kwa asilimia 99%.

Soma pia: Hamna kitu kinachoua mitaji ya watumishi kama kufungulia mke biashara. Msidanganyike!

Biashara Mbali na mtaji, inahitaji nidhamu, uzoefu, Kumiliki tàarifa Sahihi Kwa Wakati Sahihi, Mbinu za kuhudumia solo(wateja) na Kulinda wateja na kutafuta wateja wapya, ubunifu katika kukabiliana na changamoto mpya ikiwemo washindani wapya n.k.

Kusema Watu wasiwape Wake zào mtaji Kisa Wanawake kadhaa walioshindwa kuendesha biashara siô HAKI na NI Upotoshaji Mkubwa.

Jinsia haina athari yoyote katika suala la biashara. Biashara inaweza kufanywa na Mtu yeyote Yule Bila kujali jinsia Yake.

Ninawafahamu Wanaume àmbao Wake zào NI manesi, waalimu, wahasibu, yàani Wake walioajiriwa àmbao walichukua mikopo na kuwapa waume zào ili wafanye biashara na hao Wanaume wôte ninaowafahamu Karibu wôte wamepasua matajiri, wameshindwa kuendesha biashara. Na wameishia kununua Magari àmbayo wanayatumia Kwa shughuli za ufuska.

Covax kuiweza biashara kunachangiwa na mambo meñgi lakini kûbwa kuliko NI uzoefu katika biashara Husika.

NI Vizuri ungeshauri kuwa kama Mwanaume au mwanamke anataka kumfungulia mwenza wake biashara au mradi Basi NI muhimu kufuata Kanuni za kitaalamu kuhusu biashara au mradi Husika

Acha Nile Kwanza Kande hapa
 
Hakuna biashara inayokufa Kwa kuangalia Jinsia

Biashara inaweza kufa hata ikifanywa na mtu mwenye jinsia zote

Muhimu kuwa na strategic inayoeleweka na kufanya self assessment ya Kila wakati ili kuweza kujua namna ya kuboresha

Hivi Siku hizi hakuna wale mademu wa Enzi za Profesa ya Zali la Mentali? Wale wageti Kali na mboga saba 🙌
 
Mimi kama ntaoa mwanamke tamfungulia biashara na mtoto tamfungulia biashara....Dunia ya Sasa mke na watoto ndo watu wako wa karibu
Mimi x wife angu nilimfungulia biashara kwa pesa za kuunga mpaka kaolewa na mtu mwingine baada ya kuachana, ana maisha mazuri kupitia ile biashara na bado anajivunia mimi, japo yupo na mtu anajiweza mno ,mimi pia najivunia yeye now tunalea tu🤗
 
Safi sana! Hapo hata mtoto wako Kuna namna atazingatiwa pia ni ngumu Mme wake wa Sasa kumnyanyasa maaana anajua mke ana potential flan
 
Hilo muhimu sana Mkuu, Dunia ya sasa maisha kusaidiana

Wanasema usimpe mtu Samaki, Bali mfundishe Kuvua
Utafutaji wa mwanaume una mambo mengi kukosa na kupata, pia mda mwingine mengine hatuombei lkn inaweza kutokea ukatembea mbele za haki mzeee usidhani kama Kuna mtu atajali familia yako kama wanavopretend saivi we upo......Bora uwaandalie mazingira mapema na wao waweze kusimama wenyewe
 
Hilo ndiyo jambo la maana Mkuu

Ndugu zako ni Mke wako na Watoto tu, hata kama Mke atakugeuka mbele ya safari lakini bado watoto wako watakuwa salama mikononi mwake
 
Back
Top Bottom