Ndugu yangu amefeli F6 analia tu kila wakati naombeni ushauri

Inauma sana kwa mategemeo binafsi na kwa mategemeo ya familia pia ya wewe kufaulu na kwenda chuo kikuu.
Nimepita huko ila nashukuru Mungu kuna vitu unakosa na unakata tamaa ila badae unashukuru Mungu ni kama vile alipanga upite njia fulani.
Dogo anahitaji couselling ya kutosha maana mimi pamoja na wazazi kuwa wasomi na kuwasomesha dada na kaka zangu wote bado nakumbuka hadi mzee aliona nilivyosononeka akawa ananiambia "We bwana kuna watu hata hawajasoma na wana maisha usikae unawaza sana mambo ya shule we tulia endelea kupambana kwa upande mwingine naamini utapasua tu"
Looking back nashukuru sana kwa support yao na ushauri otherwise ningekuwa pagumu sana leo.kwa maamuzi yangu mwenyewe nlitaka niingie kufanya biashara niachane na vitabu ila sidhani kama ningetoboa bila kuwa mjanja mjanja au tapeli 🤣.
Anyways dogo anahitaji counseling yenu sana kwa sasa la sivyo atapoteana kwenye mawazo mengi mno tena wa kike ndio kabisa bora wa kiume wanaweza kujikaza.
Kuhusu kulia mwache alie ikiwezekana mshauri alie vizuri maana anapolia anatoa uchungu moyoni ,akikaa kawaida tu mpe miezi mitatu atapata sonona.
Muda wa kurelease maumivu ni sasa akishaacha kulia mpigeni counselling ya kutosha ya options kadhaa za yeye kupitia kusoma atakachokipenda na anachokiweza pia.
 
Wajumbe hamjambo.

Nakuja kwenu nikiwa na masikitiko makubwa sana nina ndugu yangu wa kike kafeli mitihani ya F6

Kapata as follows
Gs - E
Phy - S
Chem - E
Bio - D
B/math - F

Naombeni ushauri huyu dogo tumpeleke wapi sasa maana degree hawezi kujiunga kabisa hivyo option aliyonayo ni diploma tu yeye analia tu hawezi hata kuongea kitu.

Wajuvi wenye experience naombeni mchango wenu

Kama alikuwa na pass nzuri za PCBM kwenye mtihani wa Form IV
na kama Unaweza kumlipia mpeleke akapambane na Diploma ya Pharmacy ni nzuri na kwa kuwa amepita A- Level anaweza kufaulu vizuri ... na pengine kwenda Degree akipenda tena kwa mkopo 100%
 
Kuna mwamba alichaguliwa advance asome PCM, alisoma mwaka mzima ila mwisho wa siku akaona mambo magumu na hakujiona akitoboa.

Chap akabadili akaingia HGL, six akatoka na kijiti huku wenzio kibao alowaacha pcm walizungusha kabisa.

Ununda sometimes unawaponza wanaosoma science.
 
Inauma sana kwa mategemeo binafsi na kwa mategemeo ya familia pia ya wewe kufaulu na kwenda chuo kikuu.
Nimepita huko ila nashukuru Mungu kuna vitu unakosa na unakata tamaa ila badae unashukuru Mungu ni kama vile alipanga upite njia fulani.
Dogo anahitaji couselling ya kutosha maana mimi pamoja na wazazi kuwa wasomi na kuwasomesha dada na kaka zangu wote bado nakumbuka hadi mzee aliona nilivyosononeka akawa ananiambia "We bwana kuna watu hata hawajasoma na wana maisha usikae unawaza sana mambo ya shule we tulia endelea kupambana kwa upande mwingine naamini utapasua tu"
Looking back nashukuru sana kwa support yao na ushauri otherwise ningekuwa pagumu sana leo.kwa maamuzi yangu mwenyewe nlitaka niingie kufanya biashara niachane na vitabu ila sidhani kama ningetoboa bila kuwa mjanja mjanja au tapeli 🤣.
Anyways dogo anahitaji counseling yenu sana kwa sasa la sivyo atapoteana kwenye mawazo mengi mno tena wa kike ndio kabisa bora wa kiume wanaweza kujikaza.
Kuhusu kulia mwache alie ikiwezekana mshauri alie vizuri maana anapolia anatoa uchungu moyoni ,akikaa kawaida tu mpe miezi mitatu atapata sonona.
Muda wa kurelease maumivu ni sasa akishaacha kulia mpigeni counselling ya kutosha ya options kadhaa za yeye kupitia kusoma atakachokipenda na anachokiweza pia.
Shukran
 
Mbona amefaulu huyo?
Mwambia tu kwamba ajiamini na aamini kwamba hakwenda shule kupoteza MUDA bali kupata elimu na elimu ameipata.

Pili Hizo Max sio kipimo chake kipimo chake ni hichi anachokifanya baada ya Matokeo na atakachokifanya baada ya hapo.

Kama atakaa na kujilaumu tu basi hata angepata A zote basi angekuwa amefeli na kama atanyanyuka na kuanza kupiga hatua kuelekea kwenye ndoto zake bila kujadili DUNIA inampimaji basi yeye ana max nyingi kuliko hata aliyetunga Mtihani.
 
Wajumbe hamjambo.

Nakuja kwenu nikiwa na masikitiko makubwa sana nina ndugu yangu wa kike kafeli mitihani ya F6

Kapata as follows
Gs - E
Phy - S
Chem - E
Bio - D
B/math - F

Naombeni ushauri huyu dogo tumpeleke wapi sasa maana degree hawezi kujiunga kabisa hivyo option aliyonayo ni diploma tu yeye analia tu hawezi hata kuongea kitu.

Wajuvi wenye experience naombeni mchango wenu
Ananafasi kubwa sana. Akasome diploma ya clinical medicine, pharmacy. Hao waliofaulu atawapita kabisaaaaa!
 
Back
Top Bottom