Ndugu yangu amegoma kunirudishia pesa zangu

Ukiweza anua tanga maana ukiendelea kumdai halafu akadinda mnaweza kuleta mpasuko kati yenu utakaodumu vizazi vyenu vyote
Samehe ila usirudie tena! Utapata nyingine nyingi zaidi
Chukua huu ushauri mkuu...

Halafu nina wasiwasi hata wazazi wako upande wake...
 
Broo mm sin uwezo wa kumzamehe mtu milion 5 sina kwa kweli sina hata Uwezo wa kusamhe laki mbili sembuse hyo hapna jtatu kesi itanza
Ndugu wengi ni wapumbavu sana! Mimi miaka 15 hajanilipa Hela yangu na ni shemeji yangu amemuoa dada yangu! Alikuja anaomba utamhurumia sana na ni mtumishi wa uma! Qmmmmk!
 
Broo mm sin uwezo wa kumzamehe mtu milion 5 sina kwa kweli sina hata Uwezo wa kusamhe laki mbili sembuse hyo hapna jtatu kesi itanza
Ongea na wazee kwanza kabla ya kwenda kwenye sheria.. Kama ndio tabia yake hata huko kwenye sheria atakusumbua
Kesi za madai ni ngumu sana hasa kama hakuna maandishi.. Na anaweza kukubali deni lakini akaiambia mahakama kutokana na kipato chake uwezo wake wa kulipa ni elfu 20 kila mwezi.. Mahakama haina uwezo kwa kumlazimisha alipe kwa mkupuo
Chukua huu ushauri mkuu...

Halafu nina wasiwasi hata wazazi wako upande wake...
Hao ndio watazidi kuharibu sasa
 
Ndugu,ndugu narudia tena ndugu akikurudishia hizo pesa niitwe 🐒
 
Kesi na ndugu wa kuzaliwa nae imeleta majanga katika familia yetu, Ningejua huja badae, Adui na rafiki hawafahamiki yaani ni Ndumilakuwili.
 
Kaa chini mtengenezee sinema mkuu. Mtokee kwa nyuma huyo. Tafuta watoto wa mjin
 
Ujue hapo wanakusema una roho mbaya. Sasa ukimpeleka mahakamani hadi wazazi watakuzira.

Kuna ndugu wa damu walipigana risasi kwenye zile harakati za vyeti enzi za bwana yule

Na nyie mtafikia huko huko usipoangalia
 
Jibu ni Rahisi tu,

Imeandikwa, mwenye HAKI wangu ataishia Kwa Imani. Na application yake ni kwenye Kila kitu.

Kuna kijana nilimwamini nikampa Bodaboda Kwa mkataba wa miezi 8, akalipa vizuri miezi miwili Kisha akaiweka bond pikipiki yangu na kuacha kuleta marejesho.

Uwezo wa kudeal naye kisheria nilikuwa nao, pia hata kutumia watu ningeweza kumdaka na kumfunga alipe Hadi sent ya mwisho Kwa kuwa mikataba na vithibitisho vyote ilikuwa navyo,

Wengi walinifuata Ili nimkamate kupata HAKI yangu, lakini Kila nilipotaka kuchukua hatua nilikakatazwa na Mungu wangu, akaniambia mwache, HUTAPUNGUKIWA na chochote unachohitaji.

Kinachotokea sasa, ninatumia ninachotaka na sijawahi kuwa mhitaji financially.

Jifunze kuwa, waliookoka kamwe hawaendi mahakamani kudai HAKI, labda upate maelekezo kufanya hivyo Kwa sababu maalum.

Ubarikiwe 🙏
 
Kikwetu huwa tunasema imejila utumbo! Hivyo ndugu yangu nisamehe tu usonge mbele! Maisha ni haya haya hakuna mengine!
 
Always lend what you can afford to loose.
 
Ukimkopesha pesa ndugu, hesabu kama umetoa tu.

Ukirudishiwa sawa, usiporudishiwa sawa.

Kama unataka kurudishiwa, usimpe kabisa.
 
Mpotezee na muendelee na maisha na kuwasiliana kama ndugu itafika kipindi atakulipa na hata asipp kulipa achana nae usije anzisha balaa kwenye ukoo, writing from expirience.
 
Ukiweza anua tanga maana ukiendelea kumdai halafu akadinda mnaweza kuleta mpasuko kati yenu utakaodumu vizazi vyenu vyote.

Samehe ila usirudie tena! Utapata nyingine nyingi zaidi
Mkuu uko positive sana na maisha
 
Muite sehemu mzichape sana uondoe machungu, sababu hawezi kukulipa
Niliwah kuona jamaa mmoja alifanya hvyo,alimtembelea kaka ake ,akapikiwa msosi alipomaliza kula wakazirusha ngumi,mpaka mke wa kaka ake akatoka nje anapiga ukunga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…