Natumai wote hamjambo humu.
Nina ndugu yangu amekuwa mlevi wa kupindukia, hapo awali alikuwa ni mtu smart na mpambanaji wa maisha, sijui kitu gani kimemkuta, anakunywa pombe muda wote hata kazi ameacha kwa sababu ya pombe...
ikiwa karidhia mwenyewe na kwamba yeye binafsi anawiwa kuacha pombe lakini anashindwa, ukimpeleka huko utakua umesadia sana, atapona kabisa na kua mtu mwema na mwenye afya njema furaha tele. Na hakika atakushukuru na kukuombea sana kwa Mungu.
Lakini kama ni wakulazimisha anaweza kwenda huko na kurudi akiwa ama mlemavu ama hana meno.
niliwahi mpeleka ndugu yangu huko sober alirudi taya zimepishana, meno yamepasuka, halafu anakithembe.
Mfano ukimwambia sema Simba yeye ansema Thimbwaa,
neno sasa anasema thatha....
na wakati alikuaga yuko vizuri tu.
yaani ndio tukapata tabu zaidi kwenye hali hiyo lakini bado ndio akawa anatoroka kwenda kwenye pombe na akifika apo kwenye kibanda cha pombe akinunua kile kikopo cha elfu2 anakibugia na kukikata kap maramoja chote ili tusimkute anakunywa.
so, kwa hiari yake mpeleke tafadhali tena mapema iwezekanavyo.
mara zote tumemkuta yuko chakari....