Ndugu yangu kakamatwa kwa simu ya wizi, Nawasihi sana tuchukue tahadhari tunaponunua simu 'used'

Ndugu yangu kakamatwa kwa simu ya wizi, Nawasihi sana tuchukue tahadhari tunaponunua simu 'used'

Mambo ya kununua kwa unaemwamini kwa kauli mali pekee haitoshi kwa ulomwengu wa sasa, kesho mwaweza kupishana kauli akakuchoma ama nae aliinunua ya wizi likakukuta wewe.

Kama ilivyo kwa gari, kwenye simu pia hakikisha hata ukinunua kwa rafiki yako kuwe na mkataba ulioandaliwa na attorneys waliojaa kama utitiri mjini, ni heri umpe attorney elf 50 kwajili ya mkataba kuliko kukamatwa na huna nyaraka yoyotr ya usbahidi.
Kumbe wanasheria kazi yao ni kutakatisha mali za wizi ekh
 
Kwa hali ilivyo sasa mahala salama pa kununua simu ni dukani tu
Wewe unanunuaje simu mkononi pasipo na uthibitisho anayekuuzia ndiye mmiliki halali?
Simu yoyote iliyonunuliwa kihalali ina vithibitisho vikiwemo risiti halali na mkataba wa mauziano.

Kama hivyo hakuna basi endelea kununua simu kiholela ukisubiri somo la hekima.
 
Daaah! na wauza simu wamekua wengi sana,inabidi kujihadhari kwakweli.
 
Mwezi wa 8 mwishoni simu yangu ilinianguka mahali, kijana alieiokota nilipopiga alijibu vizuri tu na kuonesha nia ya kunirudishia lkn ilipofika time alioahidi nikaifuate simu yangu nilipopiga ikawa ishazimwa.































Nilitoka tu job nikaenda kituo cha police kilichokaribu na kuchkua RB na barua ya kupoteza simu, then nokaenda kurenew line. Sikuwa hata na pressure nilijua tu simu nitaipata. Box nilionunulia nilikuwa nalo bado, plus receipt plus imei numbers.































Ilichkua km 3 weeks tu simu yangu nikaipata ila of course niligharamika kdg kama kutoa ahsante kwa alienisaidia. Lkn jamaa aliekamatwa nae nikamtoa ile amount niliolipa kufidia. Maskin na yeye alikuwa kauziwa tu. Lkn ndio ivo simu ya 900K yeye kanunua kwa 450K.































































Vizuri ukinunua simu dukani ukipewa risiti uhifadhi pamoja na imei numbers zake. Mie nna box la simu nilioinunua 3 yrs back mpk Leo nimelihifadhi. (Sio hii nilioipoyeza)




























































Kwa kumalizia tu wakuu simu nunua dukani, simu za kuuziana mikononio sahihi watu wengi saivi wanakamatwa.
 
Nimecheza Sana na Uwinga hapok.koo,
Kiufupi ukiachilia bidhaa nyingne nimenunua simu za mikononi na kuuza Si chini ya PCs 150,
Mara mbili mwanzoni nilipatwa na hii kadhia, baada ya hapo nikawa makini sanaa...

BTW ni kazi nilikua nafanya kwa hofu sana, nina ushuhuda wa watu wengi sana wameumizwa kwa hili.
 
Pole sana kwake, nina rafiki alitoa hela nyingi kununua Samsung akashangaa baada ya miezi miwili anapigiwa simu na Askari wa Oysterbay kuwa simu ni ya wizi

Alichukulia masihara labda matapeli mpaka siku alivyoona kero ya kupigiwa imezidi na kuamua kwenda Polisi, akakuta kweli na simu kwa mujibu wao, ni ya mdogo wa kiongozi mkubwa sana nchini

Ilibidi aitoe bila masharti ya ziada maana walimtaiti kwa maelezo tu akaona hana pa kutokea na aliinunua kwa raia aliyeipost kwenye mtandao

Tuweni makini sana na simu hasa hizi Samsung either nunua dukani ama hakikisha anakupa risiti halali, vinginevyo nunua kwa unaemuamini
Hiyo huwaga ni michozi ya polisi na hao matapeli
 
Back
Top Bottom