Habari ndugu wana JF,
Jamani hii nchi kamatakamata haijaisha. Nina kaka yangu ambae ni wakwanza kuzaliwa, miaka 31 amekamatwa usiku wa manane yapata wiki mbili sasa na watu tunaowahisi ni Usalama wa Taifa.
Walienda wakavunja komeo la mlango wake wakaingia ndani. Walikuwa na bunduki, wakamkamata pasi na kutoa maelezo maalum. Wakabeba na simu zake hatujui aliko had leo hii. Mama yake mzazi analia kuchwa kutwa hajui kama mwanae ni mzima ama amekufa.
Kwakweli hali ya usalama nchini si shwari, na hatukuwahi kumuona ama kumuhisi ana vitendo hivyo isipokuwa tu ni muislamu dhehebu la sunni na shughuli yake kuu tunaijua.
Kwahiyo ombi langu kwa mamlaka; hatukatazi kuwakamata na kuwahoji, ila ni vizuri mkawafahamisha ndugu wa karibu ili waelewe wapendwa wao wamepelekwa wap. Pia ndugu Wanajf naomba muendelee kupaza sauti kutokana na vitendo hivi vya usalam wa taifa.