Ndugu yangu na wengine sita wakamatwa usiku wa manane wakihisiwa kujifunza ugaidi na hatujui waliko hadi sasa

Hili tukio limetokea nchi gani? Kama ni Tanzania mkoa au mji gani?
 
Nakushauri iteni Ayo Tv tu huku upo nusu nusu sana Mkuu.

Ila huu utaratibu uliotumika umekaa kushoto sana.
 
Daah its so sad ishu ikoje kile kipindi cha sakata la kibiti walikamatwa akiwepo na yeye ila wakarudishwa baada ya kuona hawakuw na hatia ila huyo imamu ambae alikuwa anawapa mawaidha yanayohusiana na jihadi nasikia aliuliwa huko huko na tangu kipindi hicho ratba yake masaa 24 tunaijua asubuh mpak saa 12 yupo kazin kwake alafu jion anarud nyumban analala na mkewe anathibitisha hajawahi kutoka usiku hata siku moja labda akahisi kuna shughuli nyingine anaifanya kwa siri
 
Ungejitambulisha kwanza ili wajue wewe ni nani? Unaishi wapi? Hii itasaidia kukujua na kukuletea msaada.
 
Ukanda wa kusini bado si salama hasa maeneo ya mpaka na msumbiji kingine inawezekana yeye si gaidi ila marafiki zake au alikkuwa anafanya na biashara na wanaoshukiwa bila yeye kujua shughuli zao poleni
Okay.

V I jana wa akiiskam wasidanganyike kwa tamaa ya pesa.

Uislam haufundishi ugaidi.

Mkiona mtu hata msikitini anajidai kufanya urafiki abawarubuni kwa pesa mumtolee ripoti polisi haraka sana.
 
kama kachukuliwa na TISS basi kuna kitu nyuma yake. TISS hawawezi kukurupuka tu, labda kuwe na msukumo wa kisiasa.na kwa maelezo yako inaonyesha ndg yako hakuwahi kujihusisha na harakati za kisiasa.

chunguza vizuri mienendo yake, ukute anauhusiano na kile kikundi cha kigaidi kinacho terrorise eneo la cabo delgado, msumbiji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…