Ndugu yangu Sugu 2025 tumia bajeti ya kile unachoweza kuhimili ukipoteza

Mkuu ni ushauri tu,maana watu wanataka maendeleo na Dr.Tulia nasikia ni mwendo wa kuwaletea maendedeleo tu,sasa ili chawa wasimdanye mheshimiwa Sugu,nampa ushauri,nimekosea wapi?

Wewe ndio chawa wa Tulia, maana hakuna mtu aliyeleta suala la Sugu kugombea zaidi yako. Halafu unasema unasikia Tulia analeta maendeleo, kumbe huna uhakika?
 
Ndugu yangu sugu mwaka 2025 usipoteze pesa nyingi kwenye kampeni, maana uwezekano wa kupita ni finyu sana kutokana na maendeleo anayoyaleta Dr.Tulia.Mfano bara bara,vijana na akina mama kupewa mitaji n.k.Pona pona yako ni kuundwa kwa jimbo jipya la uchaguzi la uyole.Hakuna haja ya kukasirika ni maoni tu.
Tulia ndiyo umekuja kwa staili hii?
 
Mkuu nasikia kaanza na barabara za mitaa ni mwendo wa lami kila kona.
Unasikia? Barabara za lami za mitaa Mbeya nyingi zimejengwa na Sugu (japo hili ccm hamtaki lipenye masikioni mwenu). Taja barabara gani ya lami iliyojengwa au inayoendelea kujengwa na tulia Mbeya?. Zaidi yeye anachofanya yeye kwa sasa ni kuongezea vipande vya matope pembeni ya barabara kuu. Ili bajaji zake zipate angalau njia pembeni ya barabara kuu. Ni kama kujikanyagakanyaga tu
Lakini yote kwa yote akitaka kupita kirahisi uchaguzi ujao,nenda kamwambie aachane na kurekebisha hivyo vipande. Atumie nguvu barabara kuu kuanzia igawa mpaka songwe ianze kutengenezwa kwa four way. Na kutengwa kwa barabara ya maloli.
Umeona ule mchanganyiko wa maloli,coaster,magari ya binafsi,bajaji na pikipiki katikati ya jiji Mbeya?. Unatia kinyaa. Lakini ccm wanajifanya hawaoni. Ile barabara inapitisha maloli mengi kwenda Zambia na DRC. Ona maloli yanavyoendelea kuua raia na wanafunzi pale mlima wa kuingia mbalizi.
Mwambie atengeneze jina sasa kupitia hiyo barabara tu. Zingine zote hizo anapoteza muda tu. (Bahati mbaya jinsia. Nawajua wana Mbeya. Uliopita si mnajua mlichokifanya ccm
 
Labda km ni mgeni na Mbeya sugu hajawah kushindwa Mbeya mjini zaidi ya uporaji wa wazi uliofanyika 2020 kwa sisi wenyeji wa Mbeya tunajua majimbo ya kyela,Rungwe mashariki na magharibi,momba tunduma mbeya mjini na vijijini CCM haikushinda kwny sanduku la kura bali waliamua kujishindisha
 
Mkuu ni ushauri tu,maana watu wanataka maendeleo na Dr.Tulia nasikia ni mwendo wa kuwaletea maendedeleo tu,sasa ili chawa wasimdanye mheshimiwa Sugu,nampa ushauri,nimekosea wapi?
Wewe umeshatoa conclusion kwamba Sugu asigombee ubunge 2025 wakati ni haki yake na wewe pia una haki ya kugombea ili mradi utimize vigezo na masharti.

Jimbo la bumbuli limechoka sana kimaendeleo lakini wananchi wanamchagua tu Kipara February Marope....Kwahiyo kigezo cha maendeleo sio ndio 100% utachaguliwa hata JIWE alituaminisha analeta maendeleo lakni 2020 akaiba kura zote kinguvu.
 
Ndugu yangu sugu mwaka 2025 usipoteze pesa nyingi kwenye kampeni, maana uwezekano wa kupita ni finyu sana kutokana na maendeleo anayoyaleta Dr.Tulia.Mfano bara bara,vijana na akina mama kupewa mitaji n.k.Pona pona yako ni kuundwa kwa jimbo jipya la uchaguzi la uyole.Hakuna haja ya kukasirika ni maoni tu.
Mmeanza kuufyata Mkia tumboni hahaha Roho mbaya sura mbaya.....
 
J

Jibu swali langu. Sugu amekwambia atagombea?. Miaka mitatu bado umeanza kampeni?. Unaogopa nini?
Anaweweseka mapema maana wanajua ile mbeleko iliyowabeba uchafuzi uliopita haiko tena.Sasa hivi ni kiwewe tupu kila kona.
 
Serikali ndo imeamua toa pesa sababu Ni mbunge wao kutoka chama chao Nani asie jua hata miongoni kwa kauli za mwenda aliwahi sema nipeni mtu flani ukimleta mwengne hata maji hapa hamtakaa muyaone
Mkuu kama ni serikali imetoa pesa lakini sifa anapewa Dr.Tulia,na kwasababu hawakuona hayo kipindi cha mh.Sugu,watataka kuendelea Dr.Tulia.
 
Bado miaka miratu wewe unapiga debe leo?. Siasa haziko hivyo. Katika wanasiasa ambao hawana ushawishi ni huyo Tulia.
Mkuu naongea tu kile wananchi wanasema,kingine si huyo Dr.Tulia wala Mh.Sugu ambao nina maslahi nao.
 
J

Jibu swali langu. Sugu amekwambia atagombea?. Miaka mitatu bado umeanza kampeni?. Unaogopa nini?
😆😆Mkuu za chini kabisa ya kapeti Mh.Sugu ataingia ulingoni 2025,kama unabisha juu unihukumu 2025 kama mwenyezi Mungu atatupa kuwepo hai.
 
Wewe ndio chawa wa Tulia, maana hakuna mtu aliyeleta suala la Sugu kugombea zaidi yako. Halafu unasema unasikia Tulia analeta maendeleo, kumbe huna uhakika?
Dr.Tulia sina maslahi nae wala mh.Sugu.
 
Unasikia? Barabara za lami za mitaa Mbeya nyingi zimejengwa na Sugu (japo hili ccm hamtaki lipenye masikioni mwenu). Taja barabara gani ya lami iliyojengwa au inayoendelea kujengwa na tulia Mbeya?. Zaidi yeye anachofanya yeye kwa sasa ni kuongezea vipande vya matope pembeni ya barabara kuu. Ili bajaji zake zipate angalau njia pembeni ya barabara kuu. Ni kama kujikanyagakanyaga tu
Lakini yote kwa yote akitaka kupita kirahisi uchaguzi ujao,nenda kamwambie aachane na kurekebisha hivyo vipande. Atumie nguvu barabara kuu kuanzia igawa mpaka songwe ianze kutengenezwa kwa four way. Na kutengwa kwa barabara ya maloli.
Umeona ule mchanganyiko wa maloli,coaster,magari ya binafsi,bajaji na pikipiki katikati ya jiji Mbeya?. Unatia kinyaa. Lakini ccm wanajifanya hawaoni. Ile barabara inapitisha maloli mengi kwenda Zambia na DRC. Ona maloli yanavyoendelea kuua raia na wanafunzi pale mlima wa kuingia mbalizi.
Mwambie atengeneze jina sasa kupitia hiyo barabara tu. Zingine zote hizo anapoteza muda tu. (Bahati mbaya jinsia. Nawajua wana Mbeya. Uliopita si mnajua mlichokifanya ccm
Mkuu usiwe na shaka wanaccm wenzie watampelekea maoni yako.
 
Ndugu yangu sugu mwaka 2025 usipoteze pesa nyingi kwenye kampeni, maana uwezekano wa kupita ni finyu sana kutokana na maendeleo anayoyaleta Dr.Tulia.Mfano bara bara,vijana na akina mama kupewa mitaji n.k.Pona pona yako ni kuundwa kwa jimbo jipya la uchaguzi la uyole.Hakuna haja ya kukasirika ni maoni tu.
Kwani amekuomba ushauri?

Sugu yupo Mbeya, jimbo ambalo alikuwa mwakilishi wake. Ina maana yeye haoni mpaka wewe umwambie? Amekuwa mbunge vipindi viwili, kipindi cha tatu, kama tujuavyo, dikteta aliamua kusiwe na uchaguzi, akagawa ubunge kama njugu. Hivi unaamini kwenye hayo masuala ya uchaguzi, wewe una uzoefu kumzidi Sugu?

Mwache Sugu afanye kadiri atakavyoamua.
 
Wewe umeshatoa conclusion kwamba Sugu asigombee ubunge 2025 wakati ni haki yake na wewe pia una haki ya kugombea ili mradi utimize vigezo na masharti.

Jimbo la bumbuli limechoka sana kimaendeleo lakini wananchi wanamchagua tu Kipara February Marope....Kwahiyo kigezo cha maendeleo sio ndio 100% utachaguliwa hata JIWE alituaminisha analeta maendeleo lakni 2020 akaiba kura zote kinguvu.
Mkuu umeninukuu vibaya,mimi nimempendekezea akigombea asitumie fedha nyingi sana kwa kuwa upepo sio mzuri kwake kwa kuwa mpinzani wake amejizolea sifa kemu kemu kutoka kwa makundi yenye wapiga kura wengi,na pona pona yake ni kukamilishwa upesi kwa jimbo jipya la uyole vinginevyo asije akajikuta fedha kibao zimeenda na ubunge hola.Asiwasikilize sana chawa watamfukarisha bure.
 
1.Kwasababu anayeshindana naye anafanya yanayoonekana tofauti na alipokuwapo yeye.
2.Nampa uhalisia asijetumia kiasi kikubwa cha pesa ambacho atajutia kwa kudanganywa na chawa.
Nb:Leo ni Mbeya muda ujao nitashauri jimbo lingine na ni ushauri tu ambao yeyoye angetoa kwa kuona/kusikia uhalisia uliopo.Asante.
Ushauri wenye tija hutolewa na mtu mwenye uzoefu na uelewa wa kutosha kwenye kitu anachoshauri.

Wewe umewahi kugombea ubunge mara ngapi? Umewahi kushinda mara ngapi? Uma uzoefu mkubwa kumzidi Sugu?
 
Back
Top Bottom