Ndugu yangu wa Kiume anaoga baada ya siku mbili, maji yapo ya kutosha. Hii ni kawaida?

Tushazoea wanaume hawaogi ogi. Labda kina James delicious ndo wanaume wenye kuoga kila saa wasinuke.
 
Kawaida Sanaaaa mim huwa napiga hata mwez
 
Kama ni Mbeya mini sioni shida.

Mfano mimi nikiwa Mbeya naoga mara mbili kwa wiki[emoji846]
 
Kawaida kabisa unahisi ananuka kwa sababu ya imani yako tu
 
Mwanaume kuoga kila baada ya siku mbili huo ni utumizi mbaya wa maji
 

Mbeya naijua vizuri sana...kama hujazoea ile baridi kuoga kwako kunakuwa ni nadra..nakumbuka tulikuwa tunaenda mtoni(Mto Mbalizi)...kama ni asubuhi ukiingia mtoni pumbu zinakimbilia juu...lakini sehemu zenye baridi komesha ni Upoloto..huko hadi wanafunzi wanaenda na makopo ya moto darasani...mpaka vilabuni walevi wanaenda na moto especially mwezi wa sita ...
 
Bora unuke mwili kuliko unuke roho. Mwamba yuko sawa kabisa πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Tena umenikumbusha Mbeya Enzi flani kuoga issue hasa mtu mpk unapigwa ndo uende kuzuga unaoga, halafu huogi unajipakaza pakaza tu vimaji sa Ingine mate unageuza km umeogaπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…,
Halafu Kuna Ile style unaenda kuoga then unajipakaza sabuni Tena kama mafuta ung'ae.πŸ€”
Hiyo sayansi MI sijawai kuelewa mpk leo Ile ilikua umaskini tu hamna kingine
 
Unataka Aoge na mvua hizo asipokauka je? Au unataka alale Mbichi eee
 
Kipindi nipo O' level kuna washikaji (kundi) walikuwa wanajiita 'Camel camp'. Hawa jamaa hawaogi term to term, siku alipooga anatoka home kwenda shule ataoga tena siku anatoka shule kwenda nyumbani. Na tulikuwa tunaishi nao fresh tu.

Sent from my Nokia 7 plus using JamiiForums mobile app
 
mkuu bila shaka wewe ulikuwa ndiye kiongozi wa hao Camel Camp
 
Ungeongea nae au unamwogopa
 
Nilipokuwa nasoma Ifunda Tech. nilikuwa naoga mara mbili kwa wiki...Jumatano na Jumapili. Mimi ndio nilikuwa "toz nyangema", kuna watu walikuwa wanapitisha wiki mbili hasa waliotoka sehemu za joto.

Kula lazima ila kuoga ni hiyari.

Naimiss zaidi ile baridi ya Ifunda, Ulaya haitii mguu...teh teh teh!
 
put a joke aside lets all be honest....hivi kweli inawezekana kuna wanaume wanaoga kila baada ya siku mbili?

au ni masharti ya mganga?

katika wiki si kuna siku mbili tu za kuoga jamani au wenzangu mnatumia kalendar ambayo wiki ina siku kumi nini?i tafdhali msinipe kazi ya kuangalia upya kalendar yangu naombeni majibu
 
Wakati nikiwa Mbeya, wiki ilikuwa inakata fresh tu. Kuoga weekend, tena siku ya kwenda Church.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…