Ndugu zetu wa Kagera kwanini mkoa wenu unaongoza kwa umasikini?

Taja mkoa wako kwanza tujue unaizidi nini Kagera
 
Ukweli mtupu watu wakitoka hawarudi nyuma ila wanao matajiri hizo jamii Wana manyumba hapa DSM ,Arusha ,mwanza
 
Tatizo la wahaya huwa hawarudi kwao zaidi ya kukimbilia Ulaya
 
Wachagga mnahangaika sana kuinanga Kagera wakati huko kwenu maendeleo yameganda pale pale watu hawafanyi kazi wanasubiri ela za ndugu zao wa mikoani.
Kagera ukiacha changamoto za miundombinu bukoba mjini sehemu nyingine kuko vizuri
 
Umesema ekweli ila wakija wakujiita wa kaskazini watasema wewe ni muhaya unajisifia
 
Tatizo la wahaya huwa hawarudi kwao zaidi ya kukimbilia Ulaya
True, nikienda US, Jiji la New York, in order to save money, huwa nafikia Mt. Vernon kwa bibi mmoja wa Kihaya, yuko US amezeekea hapo. Anasaidia sana Watanzania kuishi maisha ya natural habitat ya Bongo life ndani ya jiji la New York.

Nadhani ikifanywa sensa ya diaspora wa Tanzania wenye decent jobs ughaibuni, Wahaya wataongoza.
P
 
Wahaya wanapenda sn Ulaya
 
Ni watu wasio na fikra pana. Soko ama liwe stand hii ni miradi mikubwa na ndo miradi kichocheo, haijengwi na na wananchi bali serikali ikiamua.

Kama sahivi wameamua itajengwa na ndo kupeleka maendeleo kwa wananchi. Na si hayo tu,

Wanaweka RC wanajeshi kila siku ili iweje, mbona kwingine wanapeleka watu wa maana wenye CV zao na madegree yao wanaojua kupambanua mambo sasa iweje washika mitutu Kagera enzi zote as if kuna vita ama ni darful. Sasa wanataka wananchi ndo wateue RC, hilo ni jukumu lao kweli?

Vyuo na taasisi za serikali tunaziona kwa mikoa ya wengine ila Kagera ahaa! Sasa wananchi waache kujenga vibanda vyao vya kuishi wakajenge ofisi za serikali?

Kilimo ndo hicho, mkoa unategemea kilimo kwa 70% lakini eti leo ndo wanaanza kujikosha, wananchi wakulima ndo wangenunua kahawa yao wenyewe ama serikali ilitakiwa kutafuta wanunuzi kwa wakulima wake. Leo sasa aliyeleta bei mpya ni wakulima ama serikali, siku zote ilikuwa wapi na walitegemea nini
nini kwa mkoa?

Usafiri si waliua meli ikawa hamna kwa miaka zaidi ya 15, walitaka wananchi wamudu vipi maisha yao?

Nchi hii basi tu, wabaya zaidi ni hawa watu wa jf waliopita shule lakini hata kuchambua mambo hawawezi na bado daily wanajaza saver. Hii siyo sawa kabisa.
 
Serikali wakidhani wanaibagua Kagera kuwakomoa wahaya inajidanganya yenyewe. Kagera ni Tanzania na itabaki kuendelezwa na serikali kama ambavyo sahivi wameona kuna haja hiyo, kama kule si Tanzania mbona leo wameamua kwenda kujikosha?

Na wahaya tunaelewa nchi hii tunabaguana na ndo maana wanaamua kwenda zao mbele ili kuacha ya Kagera kwa serikali kwasababu wanajua walikotoka, walipo na kwanini.

Na kama serikali haifanyi kitu basi wategemee wahaya wengi zaidi kwenda mbele huko diaspora na watakaobaki wao watahangaika na vibanda vyao vya kuishi tu na maisha yao huko vijijini wanakowekeza kama Ulaya, Sikh serikali ikiona ipo haja itakuja kuuchukua mkoa wake na ikionekana haina haja wauache tu alafu tuone itakuwa aibu ya nani.

Tutajenga vijiji vyetu view kama Ulaya lakini si kuisaidia serikali baguzi kujenga mkoa wake, kama vipi waufute kwasababu hata kuanzishwa kwake wahaya hawakuomba mkoa, Mungu ndo aliwaweka pale kama wengine walivyowekwa huko kwingineko
 
Hizi data huwa zina lengo fulani nyuma ya pazia si kweli kwamba Kagera ni mkoa maskini hata kidogo, ni ngumu kuamini haya bila mtu kuingia na kuzunguka Kagera, niliwaza kuwa labda mapato yanayo kusanywa kutoka Kagera basi hayaendi ipasavyo serikalini hivyo kuonyesha mkoa ni maskini. Ki ukweli watu wa Kagera haswa wilaya za Bukoba, Missenyi, Karagwe, Muleba, Kyerwa na Ngara wanayo maendeleo tena makubwa sana ukilinganisha na kwingineko, watu wamejenga nyumba za kisasa nk, hata vijijini ndani ndani, ukitembea mikoa mingine kama Shinyanga, singida, tabora, kigoma, nk utashangaa hizo taarifa huwa wanamaanisha nini
 
Bora wewe umesema kile ulicho kiona shida ni kwamba walio wengi wanabeba data za kwenye mitandao tu lakini hawajawahi hata kufika Kagera , ukweli huu mkoa umendelea sana kuliko mikoa mingi sana hapa nchini yamkini huwa kuna sababu zinazo chagiza jambo hili
 
Katerero, mto ngono

Nashauri serekali itume team ya watu wa kagera. Kwenda kilimanjaro ikajifunze maendeleo.
Hakuna jambo lolote mhaya anaweza kwenda kujifunza Kilimanjaro, njoo na ushaidi dhabiti ni jambo lipi watu wa Kagera watajifunza Kilimanjaro ambalo Kagera halipo?
 
utalii tu! Sema UTALII Kwa herufu kubwaa. Utalii ndo umewasaidia kagera kupata umeme wa REA tunasubiri watalii waongezeke tukipata foreign currency wazaliwa wa kilimanjaro tutashauri kagera wajengewe stand na vyoo.
 
Wewe ni kweli Kagera unaifahamu wengine wanashikilia maneno tu ya mitandao hawajui hata wanachoongea
 
Kuna watu maskini huko mikoa ya watu wamejificha nyuma ya matajiri wachache mfano mikoa yenye migodi ya madini raia huko wanateseka utasema bora Kagera Mara mia. Mchawi wa Kagera ni hii serikali kwa kutoupa mkoa kipaumbele cha uwekezaji mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…