Ndugu zetu wa Kagera kwanini mkoa wenu unaongoza kwa umasikini?

Ndugu zetu wa Kagera kwanini mkoa wenu unaongoza kwa umasikini?

utalii tu! Sema UTALII Kwa herufu kubwaa. Utalii ndo umewasaidia kagera kupata umeme wa REA tunasubiri watalii waongezeke tukipata foreign currency wazaliwa wa kilimanjaro tutashauri kagera wajengewe stand na vyoo.
Dogo acha dharau zako Kagera umeme upo tangu zamani hadi vijijini
 
Hakuna jambo lolote mhaya anaweza kwenda kujifunza Kilimanjaro, njoo na ushaidi dhabiti ni jambo lipi watu wa Kagera watajifunza Kilimanjaro ambalo Kagera halipo?
Kilimanjaro labda kujifunza ulevi, kule sasa hivi ukiwa kijana timamu huwezi kutafutia maisha kilimanjaro
 
Hatuipondi tunasema hali halisi ili ibadilike. Ikibadilika ndinyo nzuri kwetu. Hili sio dongo bali ukweli na nimesikia wenyewe Prof Tibaijuka akisema hili
Hii kitu ni kweli na inasikitisha sana. Kagera ilikuwa imestawi miaka hiyo kwa sababu ya kilimo cha kahawa,ufugaji,ndizi uvuvi na biashara za mipakani nyingi zikiwa za bidhaa za magendo hasa kutoka Uganda. Ni katika kipindi hiki kulikuwa na boom kwelikweli ndo wazee wetu wa kipindi cha nyuma wakasomesha vijana wao tunaowasikia leo wakitamba vyuoni,mahakamani,maparokiani nk. Kipindi kilidumu mpaka miaka ya mwishoni wa 90's.

Sasa matatizo ya Kagera yalianza mwanzoni mwa 2000's yakichangiwa zaidi na ugonjwa wa mnyauko wa zao la kahawa. Huu ugonjwa ulitokea Uganda. Ugonjawa ulileta shida kwelikweli maana kwa wahaya kahawa ndo pesa kwao vizazi na vizazi kwa vile ni zao la kudumu. Mashamba yaliteketea mengi sana na hivyo ikawa anguko kubwa la uchumi wa mkoa. Wilaya zilizoathirika zaidi ni Bukoba na Misenyi. Sasa hilo janga halijatulia likaja pigo la mnyauko wa migomba. Mgomba ukishatoa tu ndizi unanyauka na ndizi yake. Fikiria mapigo hayo. Kwa mhaya ndizi ni uchumi(via kuuza na kutengeneneza pombe) na ni chakula kikuu na himilivu kwa mkoa mzima. Hapo kea watu wale hawajui kilimo kingine zaidi ya ndizi umasikini wa kipato hauwezikukwepeka maana hela inayopatikana itanunulia chakula mbadala hapo unga na mchele.

Miaka 5 ya Magufuli ndo iliumiza zaidi mkoa wa Kagera maana wakati wa msimu wa kahawa kunakuwa na mzunguko mzuri wa hela mipakani na Uganda wakulima wanauza kahawa zao either chama cha msingi au kwa waganda kea magendo. Na hspa kshawa ya mgendo inakuwa na bei nzuri Sana iliyochangamka.Ni katika kipindi hiki mipaka ilifungwa,hakuna kahawa kwenda nje,vijana waliokuwa wakijishughulisha na biashara hii wengi walipata misukosuko kutiwa ndani,kunyanganywa kahawa zao na mambo mengi yalitokea. Ikawa ni kama jinai kuonekana unanunua kahawa. Mapato kwa familia nyingi yakawa yamepungua. Huko kwenye uvuvi nako ndo husiseme mitumbwi ilishikiliwa,watu walifungwa,makokoro yalichomwa na uvuvi lililokuwa limebaki tegemeo la kipato maana uvuvi ulikuwa unaajiri vijana wengi nalo likafungwa uvuvi ukawa haramu mkoa mzima umepitia mateso makubwa sana. So combination ya yote haya ndo chanzo cha umasikini wa kipato na ni kweli kwa sasa mkoa wa Kagera unapitia kipindi kigumu sana. Walau zimeanza kusambazwa miche za kisasa za kahawa kwa wakulima kitu ambacho ni tegemeo kwa baadae.
 
Nimesoma kilimanjaro advance, hawa jamaa mnawazidi utalii tu, ila kimaisha wanawakaribia sana kuanzia hali ya hewa, mandhari, tena makazi wapo vizuri haswa, mm niliishia kamachumu, yaan nyumba nilizokuta kule hadi nilishangaa maana sikutarajia kabisa, kuhusu kilimo hicho hawajuhi sana wao ni zero grazing hawani muda wa kulima mashamba eti, yaani mgomba humo humo, papai, magimbi, mahindi, mihogo humo humo[emoji119]

Hawa jamaa maendeleo wanayo, sielewagi kw nn mnawananga hivi[emoji23][emoji23], mm niliendaga mwaka jana kwkwl maeneo niliyotembelea walikuwa vizuri hasa makazi wamejitahid kama mnawazidi labda stendi, hadi nilimuuliza jamaa tulienda naye, inakuwaje wanakuwa wa mwisho

Jamaa wakati umeme wa tanesco unakata, wao hawana habari, niliambiwa wanatumia wa Uganda Owen fall [emoji23][emoji23], kila bidhaa tukinunua ni made in Uganda, hapa ndo nikasema kwl inawezekana Serikali iliwatenga hawa jamaa [emoji23]
Wewe ndo umesema ukweli.
 
Tusitafute wachawi badala yake tutafute sababu za msingi na suluhu. Kanda ziko mbali hivi hakuna sababu ya msingi ya kulinganisha kwa kujitamba. Tusiwe wepesi kutumia neno "vita" hakuna vita yeyote na tuwe makini kutunga vita ambazo hazipo
Zipo sana pitia nyuzi mbalimbali hapa jf
 
Kwa sasa tunaye adui mmoja mkubwa sana...DEMOKRASIA!
Tunahitaji dikteta mwema kwa sasa (benevolent dictator).
Tulimpata magufuri kwa miez 12 tu ya mwanzo, ghafla akageuka dikteta mwovu (tyrant)!
Demokrasia inatumika vibaya. Wasio na ufahamu (unknowledgeable) na taarifa (uninformed) wanashiriki kufanya maamuzi ya msingi katika ujinga wao! Kungekuwepo na watu, timamu waliopass ufaham na taarifa, wenye kuamua kwa ajiri ya Taifa zima. Upigaji kura hauna maana kwa asiyejua anachagua kati ya nini na nini!
Ukiachilia sheria mbovu, demokrasia inazorotesha uwajibikaji kwa raia na viongoz.
mf.
1. kuna felonies hasa za matumiz mabaya ya kibubu cha Taifa inabid watu walazmishwe kuipisha dunia!(disposed)
2. Demokrasia inakazia raia kudai haki bila wajibu hasa. Kila mtu si tu afanye kazi kujenga nchi bali aonekane akifanya kazi.
Wananchi kwa hiari wakubari kujituma na kujibana ili tupunguze kukopa kopa, tujitegemee kwa kesho.
Mbona ngaz ya familia pesa ikikata raia hawa hawa tunajua kubana matumiz badala ya kufikiria kujikopa kikangomba kangomba! Au kibutura!
Yan raia anataka vyote vinavyopishana kwa mpigo: maisha mazuri na kujituma kidogo!
Ili tufike huko lazma tuboreshe namna ya watu kuingiziwa elimu, ujuz na maarifa.
Katiba tu haitoshi kama raia wenyewe tuna nadharia hizi za kuibiana na kufuja. Tutafungana tuishe.
Overhaul ya nchi si kubadilisha tu viongoz, huenda tukawa tunabdili majina wa wapigaji tu.
Tuanze na wazaz/jamii kutohamasisha watoto kuiba vya jumuiya na uzalendo. Siku hizi mtoto mwizi aliyeajiriwa mzaz ndo anajivunia zaid. Unaweza kuta hata waliopo leo madarakan wakifa tunapata kizaz cha wapenda haki, usawa na uzalendo.
Napendekeza uwekezaj wa hivi kwa sabab njia ya uhakika ya kubadili hali ya mambo haraka naona tunaikwepa!
We need the hard way!
....LIVE RESPONSIBLY!
 
Inasikitisha kujua hili la kwamba Kagera ni mkoa masikini kuliko yote Tanzania.

1. Ina wasomi wengi sana
2. Ardhi nzuri
3. Ziwa kubwa
4. Mipaka ya nchi yetu mingi

Pamoja ya yote hayo ni swali ya kujiuliza wenyewe watu wa huko bila kuweka lawama kwa serikali. Ukiangalia vizuri Kagera na Kilimanjaro zinafanana sana lakini ki maendeleo ni paka na panya. Acheni kulaumu na kusubiri serikali na jiulizeni tatizo hasa kwenye jamii yenu ni nini?

1. Je, usomi hasa wa juu kwa watu wengi wa huko umesaidia ? Au umeongeza majigambo yasio ya msingi na kupunguza fursa
2. Tabia ya kulalamika kama vile Chato ndiyo sababu ya umasikini wenu. Je hii tabia inasaidia nini hasa? Kabla ya Magufuli bado mlikuwa masikini sana
3. Je, mnaheshimu au kudharau vijiji vyenu na mkoa wenu?

tatizo la mkoa huu,kwanza unafiki pili ukabila.watu wa mkoa huu hawataki kuchangamana na makabila mengine.mikoa ambayo watu wamechangamana na makabila mengine maendeleo huja kwa kasi.mkoa wa kagera kwa mgeni kumiliki ardhi ni ngumu sana hata tu kijieneo cha kujenga utapata kwa shida sana na ukikipata pia risk ya kutapeliwa ni kubwa mno.kagera wenyeji hawaaminki si mwanamme wa mwanamke.ukizubaa tu umetapeliwa.hivyo inakuwa vigumu sana kwa mgeni (mnyamahanga) kuwekeza ktk mkoa huo.
 
Hivi vita vya ukanda,nyanda hii vs nyanda nyingine au kabila hili dhidi ya lile vinavyoendelea humu ndani sijawahi kuvielewa.

Hiki ni kipindi ambacho tulitakiwa tuwe tumeshaondokana na ukabila na ukanda.

Hili jambo linashangaza lakini! Nchi ni ile ile wote tunataka iendelee ila mtu anataka kwao kuendelee na kwingine asipopapenda paendelee kuwa duni!

Makabila , ukanda na udini ni upumbavu mtupu unaosababisha Africa isitulie hadi leo.

Wanangu hawatakuwa na kabila lolote.Lugha watakazofahamu kwa hapa nyumbani ni Kiswahili na Kiingereza pekee.
Cha ajabu wazee wetu hawajawahi kuzungumzia mambo ya hovyo km haya, lakini ni vitoto vidogo vinazungumzia utafikiri sifa.
 
Haya yote wanayaleta watu wa kilimanjaro baada ya kuona kwao panadumaa. Hapa lengo la mleta mada sio kuisema Kagera ila anataka kujua nini kinaebdele Kagera kimaendeleo ili alinganishe na kwao. Kagera ukiacha uchakavu wa miundombinu bukoba mjini mkoa wa Kagera hauna huo umaskini wanaosema wanywa mbege
 
Back
Top Bottom