Ndugulile: Kama hauna uhakika na taarifa usipost, usiretweet, ku-like wala kukomenti

Ndugulile: Kama hauna uhakika na taarifa usipost, usiretweet, ku-like wala kukomenti

Dalili zote Mkuu tunaelekea huko, wanataka kudhibiti majukwaa yote.

Walianza na majukwaa ya siasa, wakaenda vyombo vya habari /media, vyama vya kitaaluma, vyuo vikuu wameshamaliza.

Sasa wanatafuta kuungwa mkono kwa vitisho ndani ya nyumba za ibada.

Tundu Lissu alituasa wakimalizana na "sisi", wakakwenda na sehemu zingine kujaribu kuwanyamazisha na kuwatisha.
Ndugulile aangalie kilichomkuta Nape
 
Yani Mariah Sarungi anatuma post ya kuelimisha ni jinsi gani tujikinnge na covid kulike na kuretweet ni kosa kwakuwa to mimi sina utaaramu wa magonjwa..ila jiwe anatuma post ya kusema fumigation ni ya kuuwa mende na inzi to nikilike na kuretweet ni sawa...tuachieni ujinga huwo..tutalike na kuretweet tunavyovitaka...
 
Hapo kwenye ku like ,na ku comment wanatukosea.waziri tunajua ww ni mchapakazi ,lakini Sasa usitafute kuonekana unafanya kazi kwa kuanza vituko.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
“The basic tool for the manipulation of reality is the manipulation of words. If you can control the meaning of words, you can control the people who must use them.”

Philip K. Dick
 
Stupid kabisa. Msitutishe .Tutalike na tutacoment. Sasa naona mnataka kuingilia uhuru wetu hadi vya kulike jamani ?Kwanza wakati mwingine unaweza kulike bila hata kujua.

Hawa wanataka hadi kuuingia vyumbani mwetu. Hii nchi inapoelekea sijui ni wapi??!!, hata Korea kaskazini ni afadhali.
 
Hakuna kinachonikera awamu hii kama kila kukicha uhakiki, yaani tena anamaanisha tunahakiki tena laini za simu? Kuna tatizo mahala kwa serikali hii.
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amewatahadharisha wanaochapisha taarifa wasizokuwa na uhakika nazo.

Kuanzia jumatatu, Februari 21, Ndugulile amesema wataanza kuwachezesha wote wanaotoa taarifa potofu na wanaofanya utapeli.

Amesema kama hauna uhakika na taarifa usipost, usiretweet, usilike wala kukoment.

Aidha kuhusu matapeli wa mtandaoni, Ndugulile amesema wataanza uhakiki upya ili kudhibiti hilo.

View attachment 1707876

Kama wanatupangia vya kufanya kwenye mitandao basi wawe wanatuwekea BANDO.
 
Umeambiwa kama kitu huna uhakika nacho,usipost,kukoment wala kulike...
Anayepaswa kuwa na uhakika nacho ni aliyepost, mimi msomaji nitapaje uhakika kama hata chanzo cha taarifa sikijui? Serikali itulie sasa
 
Huyu nae km ndo hivi, atumbuliwe tyuuh tena msieeeew. Hovyoooooh
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amewatahadharisha wanaochapisha taarifa wasizokuwa na uhakika nazo.

Kuanzia jumatatu, Februari 21, Ndugulile amesema wataanza kuwachezesha wote wanaotoa taarifa potofu na wanaofanya utapeli.

Amesema kama hauna uhakika na taarifa usipost, usiretweet, usilike wala kukoment.

Aidha kuhusu matapeli wa mtandaoni, Ndugulile amesema wataanza uhakiki upya ili kudhibiti hilo.

View attachment 1707876

Kuna changamoto nyingi zinahitaji utatuzi lakini mindset ya viongozi wetu imejiminya kupambana na vitu trivial sana sijui kwanini hawapanuki kimawazo, makampuni ya simu yanalalamikiwa kwa wizi kila siku hilo hawaoni kama ni shida.
 
Back
Top Bottom