Uchaguzi 2020 NEC imemteua Bernard Membe kugombea Urais na Omary Mohamed Umakamu wa Rais kupitia ACT-Wazalendo

Uchaguzi 2020 NEC imemteua Bernard Membe kugombea Urais na Omary Mohamed Umakamu wa Rais kupitia ACT-Wazalendo

Tuombe Mungu aepushie mbali, sisi wawekezaji tuna mengi ya kupoteza
Jamaa anajua jeshi lita msaidia maana kawapa ajira nyingi za kisiasa.. Hatambui kwamba hao alio wapa ajira ni wachache sana ukilinganisha na wingi wao
 
Membe wewe bado ni CCM, watanzania hatuna imani na wewe hata useme nini, tuna imani na TUNDU LISSU TU.
 
Ina maana ile sheria ya kumtaka mgombea awe amehudumu kwenye chama mwaka mmoja imekiukwa?
Mkuu kwani enzi ya kubadilishia gia angani kisa mamvi hiyo sheria ilikaaje? Tuanzie hapo ndio tuje kutegua kitendawili hiki.
 
Msije mkamdhuru ili kukwepa aibu yenu ya kesho.. kwa nini mpaka sasa hajaingia kukabidhi form?? Kwa nini mnasubiri giza nyie NEC?
 
Benard Membe na Makamu wa Rais (wagombea) wa ACT-Wazalendo wamekidhi vigezo vya kuteuliwa na kugombea

Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistolces Kaijage kwa mamlaka aliyopewa, amemteua Bernard Membe kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Omary Mohamed kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia Chama cha ACT Wazalendo

Huyu atamsaidia Rais Tundu Lisu kwenye masuala ya kimataifa akiwa kama mshauri mkuu wa Rais Lisu kwenye eneo hilo.
 
Akiongea baada ya kupitishwa na tume Membe amesema endapo tume watafanya mchezo nchi itachafuka.

Anasema ketendo Cha Kila kitu kufanywa kwa matakwa ya mtu mmoja kisa tu Ni Rais wa nchi kinaweza leta machafuko na Wala hayatazuilika kirahisi.


Amesema yeye ametembea nchi nyingi kama mwangalizi wa uchaguzi ila haya yanayofanyika Tanzania Ni kuhatarisha amani ya taifa letu pendwa..

Amesema ni wajibu wa Kila mtu kutenda haki ili watanzania wapate kiongozi wa matakwa yao.

Sio kuchaguliwa kiongozi.

Nilikuwa nikijiuliza hii propoganda ya kuwatìa wananchi hofu nani wako nyuma yake? Mmoja huyu hapa kesha jitokeza, Membe.

Kimsingi hicho kinachoitwa haki ya watanzania ni geresha tu ya kuwadanganya wajinga. Hawa wanatetea maslahi yao na wameungana kupiga propoganda za kueneza hofu. Ooh sijui nchi hii itakuwa kama Zimbabwe na blabla nyingine. Hatutasahau nchi hii ilovyo kuwa inaendeshwa kwa mtindo wa wakubwa hawa kupishana angani. Waligeuza masurufu ya safari za nje kuwa miradi yao. Mikutano ya nchi inafanyiwa sijui Dubai, Daban SA, London. Rais na Waziri mkuu wanakutana angani na kutua kwa pamoja Uingereza kusaini mikatàba etc
 
Someni ujumbe wa Mheshimiwa Lissu
View attachment 1547665
Huwa tunailaumu CCM inatumia ujinga wa wananchi kuendelea kuitawala hii nchi.

Ila nawaambieni CDM wataendelea kutumia ujinga wa wafuasi wao kupata huruma. Kwanini kiongozi asiseme sababu iliyowafanya wakasubirishwa.

Kama tunamua kuwa wakweli basi tusema ukweli wa jambo lenyewe sio kujifanya victim kwamba kusubirishwa kwako unaonewa.
 
Back
Top Bottom