Uchaguzi 2020 NEC yafafanua Timu za Kampeni baada ya Tundu Lissu kuhoji ushiriki wa Kassim Majaliwa katika kuzunguka nchi nzima

Uchaguzi 2020 NEC yafafanua Timu za Kampeni baada ya Tundu Lissu kuhoji ushiriki wa Kassim Majaliwa katika kuzunguka nchi nzima

Mkuu sio kama ni hivyo, kiufupi hakuna hiko kitu cha wengine kupita huku na huko wakimnadi mgombea urais vinginevyo NEC ingetoa ratiba zao. Team inapaswa iambatane na mgombea full stop, CCM wakifanya ni sawa na mataga hayo wanayafukia. Upumbavu mkubwa huu
Ndio maana nauliza utendaji wa hiyo timu ya mgombea (wagombea). Kama sheria imewatambua basi sheria hiyo hiyo inamtambua namna ya utendaji kazi wa timu. Wauweke utaratibu wa utendaji wao tuujue.
 
Sheria haijatafasiriwa Kama unavyotoa mfano wa kipumbavu Sheria ilo Kama inavyosema mbunge,raisi wote ni wagombea na kila mmoja anaruhusiwa kuunda timu yake...ila sio mbunge awe kwenye timu ya mgombea uraisi
 
NEC: TIMU ZA KAMPENI

Timu ya kampeni ni kundi la watu lililoundwa na mgombea wakati wa mchakato wa uteuzi au uchaguzi kwa lengo la kumnadi na kumsaidia mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi (Kifungu 7(3).

Mgombea atakayekuwa na timu ya kampeni anapaswa kuwasilisha majina ya watu wanaounda timu yake ya kampeni siku mbili kabla ya kuanza kwa mchakato wa uteuzi au siku saba baada ya uteuzi, kama ifuatavyo:

1. Mgombea Urais anapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi hamsini (50). (Kanuni 17(1)(a)

2. Mgombea ubunge katika eneo la Tanzania Bara anapaswa kuwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi ishirini (20). (Kanuni 17(1) (b);
Sasa kuhusu Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wamesemaje?

Mahera Angekuwa na akili angeikataa kazi ya kusimamia Uchaguzi, itamharibia Maisha yake yote
 
Naomba kujua!
Kwani hizo Kanuni haziathiri masharti mengine ya Uchaguzi?
Mfano Mgombea aliyepitishwa bila kupingwa kuruhusiwa kufanya kampeni!
 
Je, Mgombea anaweza kuwa kwenye timu ya kampeni ya mgombea mwingine?
Haiwezekani ,Maalim Seif hakumjaza Lisu kwenye timu yake ya kampeni wala Lisu hakujaza Maalim Seif kwenye timu yake ya kampeni
 
Anatembea akitumia rasilimali za serikali, tatizo ni hilo.

Sasa nimeelewa ruksa kina Mbowe na kina Zitto kuzungukia maeneo mengine ya nchi, kunadi wagombea wao bila kubughudhiwa.

Kiukweli Mkiti yule anatembea na timu ya watu zaidi ya 50. NEC kazi wanayo, maana huyo mkiti ndiye bosi wao.😀

Everyday is Saturday................................. 😎
 
Haiwezekani ,Maalim Seif hakumjaza Lisu kwenye timu yake ya kampeni wala Lisu hakujaza Maalim Seif kwenye timu yake ya kampeni
Tuseme basi Majaliwa yuko kwenye listi ya timu ya Magufuli ratiba ya kuzunguka Tanzania nzima peke yake iko wapi.

Kama kila mjumbe wa timu wale 50 atakuwa na convoy yake huoni itakuwa fujo.
 
Kwa maelezo ya ofisi ya msajili wa vyama ni ruksa kwa waziri mkuu kufanya kampeni kwa misingi ya yeye kuwamo ndani ya hao wanaotakiwa kumfanyia kampeni mwenyekiti wake akiwa kama mwanachana na mjumbe wa NEC ILA Usisahau kwamba bado anahodhi mamlaka akiwa waziri mkuu. Suala la kwann anazunguka bila mgombea uraisi hiyo iko hivi kanuni inaruhusu idadi ya watu kumfanyia kampeni mgombea na hiyo haijasema mipaka yako ktk utendaji wao huo hivyo sio sababu ya kujiuliza. Pia kuhusu mh.Lissu kwamba alikua hajui mpka akahoji hilo!!!!!! Kila mtu ana ufahamu wake ktk kuchambua.
 
Nakukumbusha, Baraza la mawaziri halijavunjwa kulingana na utaratibu wa sheria zetu.
Najua halijavunjwa...

Majaliwa ni waziri mkuu mpaka sasa, kisheria haruhusiwi kufanya kampeni tofauti na jimboni kwake.

Hao wanaosema ni MJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA sawa...

Je uchaguzi huu unaongozwa na sheria za chama cha ccm au Tume na Kanuni za Uchaguzi.??
 
Tuseme basi Majaliwa yuko kwenye timu ya Magufuli ratiba ya kuzunguka Tanzania nzima peke yake iko wapi.

Kama kila mjumbe wa timu wale 50 atakuwa na convoy yake huoni itakuwa fujo.
Mkuu unataka kuona ratiba au uhalali wake ktk hiyo mizunguko?
 
Nini maana ya timu kisheria? Kimichezo nikisema timu ya Yanga uwanjani namanishi watu 22. Hapa11 uwanjani 11.reserve!! Unaweza kusema Timu ya Yanga inacheza Morogoro sa 10 wakati timu hyo hyo ya Yanga inacheza Iringa mda huohuo?? Kisheria Timu ya kampeni je nini mana yake na inacheza viwanja gani wakat mmoja??Naomba mnijibu swali hili wataalam??naamini vifungu hvyo tume imetafsili isivyo kabsaa!!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Ukionyesha ratiba yake kutoka tume ndio uhalali wenyewe.
Ndo uhalali wake maana yeye anafanya kampeni akiwa mjumbe wa chama na sio waziri mkuu ingawa bado ni PM kwa sababu bado sheria inatambua hivyo. Nadhani swali la mh.Lissu halikutakiwa kua hili au alikua na maana tofauti kidogo ambacho sie bado hatujaona
 
Hahahhaha.. Washabiki wa Lisu ni wajinga sana aisee!

Sheria zipo na Lisu anaejifanya kujua sheria hatukutegemea kuhoji swali la kipopoma kama hilo
tuna kazi sana na hiki kizazi cha kina kigogo
 
Tunataka ufafanuzi wa kampeni za waziri mkuuu

Sheria imesema timu ya kampeni ya mgombea. Haijasema vyeo vyao. Hivyo awe Waziri Mkuu, Waziri, mkulima haijalishi ilimradi ameorodheshwa kuwa sehemu ya timu ya kampeni. Mbona rahisi kueleweka!
 
Ndo uhalali wake maana yeye anafanya kampeni akiwa mjumbe wa chama na sio waziri mkuu ingawa bado ni PM kwa sababu bado sheria inatambua hivyo. Nadhani swali la mh.Lissu halikutakiwa kua hili au alikua na maana tofauti kidogo ambacho sie bado hatujaona
Swali linakuwa je NEC inaruhusu kila mjumbe kati ya wale 50 wazunguke peke yao bila utaratibu au ratiba maalumu.
 
Sasa NEC waseme ratiba ya kampeni ya Kassim Majaliwa waliitoa wapi na lini?
Kila mgombea wa ubunge anaratiba ya kampeni ktk jimbo lake, sasa Kassim Majaliwa anatumia ratiba hiyo kwa jimbo husika kumwombea kura mgombea ubunge na rais! Anafanya hivyo kwa kuwa moja, ni mjumbe wa halmashauri kuu, pili, in mmoja kati ya timu ya mgombea urais!
Ukishindwa kuelewa naomba nikukumbushe, unajua Lissu alikuwa mgombea ubunge mwaka 2015 na alizunguka na Lowassa almost nchi nzima?
 
Back
Top Bottom