Uchaguzi 2020 NEC yafafanua Timu za Kampeni baada ya Tundu Lissu kuhoji ushiriki wa Kassim Majaliwa katika kuzunguka nchi nzima

Sheria imesema timu ya kampeni ya mgombea. Haijasema vyeo vyao. Hivyo awe Waziri Mkuu, Waziri, mkulima haijalishi ilimradi ameorodheshwa kuwa sehemu ya timu ya kampeni. Mbona rahisi kueleweka!
Sawa, leta ratiba yake au kwa vile ni mjumbe anaruhusiwa kujipangia ratiba.
 
you Nailed it Master!
 
Reactions: ZNM
Tume imesema wabunge wanaruhusiwa kuwa na timu ya watu 20, unataka kutuambia Majaliwa ameorodheshwa kuwa mjumbe kwenye majimbo yote ya Tanzania.

Kuhusu Lissu na Lowassa unazungumzia kanuni zipi za 2015 au hizi mpya za 2020.
 
Ndio maana tunasema washabiki wa Lisu ni wajinga kama mgombea wao.

Ni kujishushia hadhi kubishana na nyie humu kwa vitu vilivyowazi kabisa.
Una akili nzito kuelewa mambo.....
akili ngumu kama nta amaa!!!?
 
Swali linakuwa je NEC inaruhusu kila mjumbe kati ya wale 50 wazunguke peke yao bila utaratibu au ratiba maalumu.
Hapana hairuhusu hao wajumbe kufanya hivyo isipokua wawe na ratiba waliyo iwakiisha NEC.
 
Jibu wewe wa Chekechea maana hao ndo wasomi wa CCM na Serikali yake wenye kujua hata lugha za kigeni kuliko viongozi na wazazi wao wanachama wa CCM. Wa darasa la 7 hajui kusoma wala kuandika hata jina lake mpaka anamaliza Chuo Kikuu aanze kuzunguka na bahasha ya kaki na PhD yake aliyopata baada ya kumaliza bure elimu ya Awamu ya Tano. Bora bure elimu!
 
leta vifungu vya sheria ya uchaguzi inayokiukwa na waziri mkuu.
Nikisoma mabandiko yako husikia kichefuchefu! Bahati yako si mwanangu. Ningeishakuita zamani na kukukunyaga bakora kiasi cha kufa mtu. Aibu kubwa kwa mamayo na mzigo kwa babayo. Crimea commiting crime to thyself!
 
Tume imesema wabunge wanaruhusiwa kuwa na timu ya watu 20, unataka kutuambia Majaliwa ameorodheshwa kuwa mjumbe kwenye majimbo yote ya Tanzania.

Kuhusu Lissu na Lowassa unazungumzia kanuni zipi za 2015 au hizi mpya za 2020.
Ukitembea na majibu yako, si rahisi kuelewa majibu ya wengine, Hata hivyo siku hazingandi, show inaelekea ukingoni!
 
Kampeni za uraisi na makamu wa rais zina ratiba maalum, inayotolewa na NEC na ratiba ya NEC ina watu wawili tu wanaofanya kampeni ambao ni rais na Mgombea mwenza. Sasa Majaliwa yupo kwenye ratiba ipi ya NEC?

Lengo la kuweka ratiba ili ni kuweza kucoordinate ulinzi na usalama maana kama wangeacha kila mtu ajiendee kumnadi mgombea wake ingekuwa fujo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…