NEMC yatoa angalizo tabia ya wenye mabasi 'kuchimba dawa' na kutupa taka Ovyo porini wakati wa safari

NEMC yatoa angalizo tabia ya wenye mabasi 'kuchimba dawa' na kutupa taka Ovyo porini wakati wa safari

Vyoo vijengewe porin afu nani atakaa afanye usafi huko wakati vya mjini tu vinawashinda usafi.....

Solution mabus ya ruti za zaidi ya masaa 8 yawe na choo tu
 
Mkurugenzi wa Baraza la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka amezungumza na waandishi wa habari na kusema:
View attachment 2734498
Moja ya jambo ambalo limekuwa likifanyika mara kwa mara kama mazoezi ni mabasi ya abiria, malori na magari yanayofanya safari ndefu kuwa na kawaida ya kusimama porini kwa lengo la kujisaidia (kuchimba dawa).

Amesema tabia hiyo imechangia kuchafua mazingira na kuwa kero kwenye jamii, kwani hali hiyo imekuwa ikifanyika hata katika vyanzo vya maji na hivyo wakati wa mvua uchafu unasambaa na kuharibu mazingira.

“Mbali na hapo inadharirisha hasa kwa wenye jinsi ya kile, kwani mara nyingi maeneo wanayofanya hivyo si rafiki kwa binadamu kunaweza kuwa na wadudu au Wanyama wakali.
View attachment 2734502
“Hivyo ni muhimu kushirikiana na Halmashauri mbalimbali kuhakikisha vyoo vinajengwa kila baada ya mwendo fulani kwenye maeneo ambapo Barabara Kuu zinapita, pia nipongeze baadhi ya mabasi ambayo yana vyoo ndani.

“Kuna watu wengi wanapitia wakati mgumu katika kujizuia wanapokuwa njiani wakati wa safari, wapo wanaoogopa kunywa maji kwa kuwa wanajua inaweza kumsumbua anapobanwa haja.”

Ameongeza kuwa elimu itolewe kwa abiria wanaotupa takataka mbalimbali barabarani wakati wa safari.

Kuanzia Wiki ijayo NEMC itatoa elimu kwa muda wa mwezi mmoja, baada ya hapo basi litakalokamatwa, litapigwa faini ya Tsh. Milioni tano.
Halmashauri zingejiongeza kuweka vyoo, bafu na migahawa, wangetengeneza kipato cha uhakika, Ila ndio hivyo, upigaji ndio unaopewa kupaumbele na sio uwekezaji.
 
Back
Top Bottom