Neno "DEAR" linatumika vibaya au ni Ushamba wangu

Kwa nilichokiona processor yako iko slow sana
 
Nani alikudanganya dear ni kati wapenzi tu? Ushamba mwengine! Barua zangu zote nilipofika form two na kutaka kuwaonyesha ndugu zangu kuwa nimeanza kujua kiingereza nilikuwa naanza na ''Dear sister, Dear Father, Dear Brother.....
Kwenye upande wa barua ipo hivyo. Formal letter lazima ianze na dear.
Ila kibongobongo kwenye maongezi ya kawaida inaleta ukakasi.

Kwahiyo wewe mshkaji wako wa kiume akikuita dear utaona sawa? Kama ni sawa tufunge huu uzi kabisa
 
Kweli hii lugha ilikuja na Meli
Sa hapo mbona hakuna tatizo kabisa
 
Dear Ina maanisha mpendwa...

Mpendwa mteja hauna Salio la kutosha kukamilisha muamala huu

Dear customer you don't have enough balance to complete this transaction...


Cc: Mahondaw
 
Wewe ndiyo una tatizo.
Umezeeka kama mimi na English yetu ya shule za Nyerere.
Nadhani darling, My love na honey zina maana tofauti na dear ingawa dear inawahusu wote hao wengine.
 
Dear friend, dear father, dear mother, dear brothers and sisters, dear colleagues, ...
 
Yani mimi mtu nisiyempenda akiniita hivo nachukia sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…