Neno HAKI limeanza kutawala midomoni mwa watawala, alianza Rais Samia, kafuata IGP na leo nimemsikia Kinana

“Kitu kikubwa tulichojadiliana ni kuwa, Tanzania ni yetu sote na tunapaswa kufanya kazi pamoja, kuijenga, lakini hili linawezekana tu iwapo tutajenga uaminifu na kudai HAKI, pamoja na kuheshimiana”. Rais Samia Suluhu.

“Tumekubaliana kuwa, njia nzuri ya kuwa na maridhiano ni wakati kuna HAKI. Tumepitia madhila mengi, hakuna haja ya kuyarudisha mara kwa mara, badala yake tunapaswa kusonga mbele na kuwa na siasa safi na kuiunga mkono serikali”.- Freeman Mbowe.

“Mimi ndio mkuu wa jeshi la polisi leo nyie ni polisi kesho sio polisi lazima muwaheshimu watu na mtende HAKI kuna makosa mengine ya trafiki mweleweshe mtanzania mwenzako sio lazima kila kosa umuweke mahabusu”. - IGP Sirro.

“Kila mtu awe na HAKI ya kuchagua na kuchaguliwa na HAKI ya kutoa mawazo. Lazima wanachama wawe huru kutoa mawazo na hakuna mwenye hati miliki ya mawazo. Tukiweza kuimarisha HAKI ndani ya CCM tutakuwa tumeimarisha hadi nje kwenye maeneo mengine " Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM (Bara), Abdulrahman Kinana.

CCM wasikudanganye wanayoyaongea hawayatendi (zilongwa mbali zitendwa mbali) Hawa ni wanafiki wazuri kabisa
 
Hao watapata Wajibu kutoka kwa wanadamu!
Mkuu umeambiwa relax naona umechoka, soma katiba inavyotenganisha haki na wajibu.

SEHEMU YA TATU: HAKI NA WAJIBU MUHIMU

Haki ya Usawa

12.Usawa wa Binadamu.
13.Usawa mbele ya sheria.

Haki ya Kuishi
14.Haki ya kuwa hai.
15.Haki ya uhuru wa mtu binafsi.
16.Haki ya faragha na ya usalama wa mtu. 17.Uhuru wa mtu kwenda atakako.

Haki ya Uhuru wa Mawazo
18.Uhuru wa maoni.
19.Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo. 20.Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine. 21.Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.
Haki ya Kufanya Kazi
22.Haki ya kufanya kazi.
23.Haki ya kumiliki mali.
24.Haki ya kupata ujira wa haki.

Wajibu wa Jamii
25.Wajibu wa kushiriki kazini.
26.Wajibu wa kutii sheria za nchi.
27.Wajibu wa Kulinda mali ya Umma.
28.Wajibu kwa Ulinzi wa taifa.
 
“Kitu kikubwa tulichojadiliana ni kuwa, Tanzania ni yetu sote na tunapaswa kufanya kazi pamoja, kuijenga, lakini hili linawezekana tu iwapo tutajenga uaminifu na kudai HAKI, pamoja na kuheshimiana”. Rais Samia Suluhu.

“Tumekubaliana kuwa, njia nzuri ya kuwa na maridhiano ni wakati kuna HAKI. Tumepitia madhila mengi, hakuna haja ya kuyarudisha mara kwa mara, badala yake tunapaswa kusonga mbele na kuwa na siasa safi na kuiunga mkono serikali”.- Freeman Mbowe.

“Mimi ndio mkuu wa jeshi la polisi leo nyie ni polisi kesho sio polisi lazima muwaheshimu watu na mtende HAKI kuna makosa mengine ya trafiki mweleweshe mtanzania mwenzako sio lazima kila kosa umuweke mahabusu”. - IGP Sirro.

“Kila mtu awe na HAKI ya kuchagua na kuchaguliwa na HAKI ya kutoa mawazo. Lazima wanachama wawe huru kutoa mawazo na hakuna mwenye hati miliki ya mawazo. Tukiweza kuimarisha HAKI ndani ya CCM tutakuwa tumeimarisha hadi nje kwenye maeneo mengine " Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM (Bara), Abdulrahman Kinana.

Nimetafuta neno "KATIBA" katika yote waliyotamka watu hao, sikuliona mahala popote.
Hayo yaliyosemwa hapo ni nadharia tu, yanayoweza kusemwa na mtu yeyote na yasiwe na maana yoyote, kwa sababu hayana msingi wa kuisimamia hiyo "HAKI" inayoimbwa na watu ambao tumekwishaona wakivunja haki za watu.

Kama Mbowe na chama chake na wao watawekwa usingizini na hadaa hizi, basi za "HAKI" ya mdomoni na kuacha kuwaelimisha wananchi na kuwaongoza ipatikane "KATIBA MPYA", basi tutaendelea kuimba tu hiyo haki isiyokuwepo.

Kwenye mkutano wa CCM ulisikia mahali popote walipotamka maneno "KATIBA MPYA"?
 
Kutotamkwa neno Katiba Mpya kwangu naona siyo mbaya, wangesema Katiba Mpya sio kipaumbele chetu ingekuwa mbaya zaidi.
 
Ni maigizo kama maigizo mengine
They don't mean what they say....

Msiwe wepesi kuamini yatokayo midomoni mwa watawala
Leo mnaamini maneno ya kinywa cha mtesi ciro 🙄

Kabisa hizo ni lugha za ghiliba kwani wanajua wana taswira hasi kwenye jamii. Hivyo wanajua wakitamka neno haki watapata kinga kwa umma. Ukweli ni kuwa hawataweza kutekeleza haki maana muda hauko upande wao.
 
CCM wasikudanganye wanayoyaongea hawayatendi (zilongwa mbali zitendwa mbali) Hawa ni wanafiki wazuri kabisa
Yaani kama hadi sasa watu hawawezi kutambua aina ya viongozi tulionao na njia wanazotumia kuhadaa watu, hili ni tatizo.
Tumekuwa na tofauti ya njia tu zinazotumika, lakini matokeo kwetu yanakuwa siyo tofauti sana.

Kiongozi mmoja alikuwa akipiga makelele, akitukana, akinyanyasa waziwazina hata kuumiza. Watu wameyaona hayo, waliopenda mtindo huo wa uongozi wakafurahi, na wengine tuliobaki tukasononeka.

Sasa tunao viongozi "Janja", wao wanatulaza usingizi kwa maneno matamu matamu; lakini hawadiriki kutuachia tuamue tunachotaka wenyewe. Kama tunapenda hadaa zao, tuwaruhusu waendelee kutulaghai, kama hatuzitaki, tuwaondoe. Hili hawalitaki.

Kwa hiyo, aina zote mbili za uongozi huu, hauwezi kutupatia matokeo tofauti sana.
 
Kumbe na wewe unaliona Hilo Tz Elimu ya Uraia Kwa watu wengi hakuna, tena na Hawa vijana wa digital ambao muda wao wanaspend kuangalia na kusikiliza umbea wa wasanii na watu maarufu mambo miaka ijayo yatakuwa ya hovyo kabisa, Hawa viongozi ni walewale wanabadilisha staili ya kutuletea feelings too za uongozi lakini matendo yao hayaendani na maneno hata Kwa 10%
 
Kutotamkwa neno Katiba Mpya kwangu naona siyo mbaya, wangesema Katiba Mpya sio kipaumbele chetu ingekuwa mbaya zaidi.
EeeenHeee! Samahani kwa kucheka kidogo mkuu wangu Quinine.
"Kutotamka" inatosha kabisa kukuonyesha kwamba hilo halimo mioyoni mwao.

Kama kuna jambo muhimu zaidi kwa sasa kwa nchi yetu ni hiyo KATIBA MPYA. Kutoligusia kabisa, lakini wakipapasa papasa pembeni yake, kwa matokeo yanayopatikana kutokana na KATIBA; yaani kwamba HAKI ni zao la KATIBA MPYA, bado unaona ni sawa tu?
 
Kabisa hizo ni lugha za ghiliba kwani wanajua wana taswira hasi kwenye jamii. Hivyo wanajua wakitamka neno haki watapata kinga kwa umma. Ukweli ni kuwa hawataweza kutekeleza haki maana muda hauko upande wao.
Mkuu 'Tindo',
Nimesoma yanayodaiwa kusemwa na IGP Sirro hapo mwanzo wa mada, juu ya HAKI, nikatikisa kichwa kabisa!

Mtu asiyejuwa yaliyotokea chini ya uongozi wa huyu mtu wa jeshi la polisi, akisoma matamshi hayo, atasifu sana jinsi jeshi letu lilivyo na uongozi imara.
Lakini sote tupo hapa. Ni nani asiyejuwa namna ya jeshi letu la polisi lilivyogeuzwa kuwa chombo cha kukandamiza wananchi! Leo ukisikia maneno matamu hayo ndiyo yakufanye kusahau kila kitu?
Huu ni mfano tu wa huyo mmoja, Sirro. Hao wengine na wao hawana tofauti yoyote naye.
 
Ni maigizo kama maigizo mengine
They don't mean what they say....

Msiwe wepesi kuamini yatokayo midomoni mwa watawala
Leo mnaamini maneno ya kinywa cha mtesi ciro [emoji849]
Ni kweli kabisa ila maneno kutoka kinywan kwa mheshimiwa Mbowe yanamaanisha akisemacho
 
“Kitu kikubwa tulichojadiliana ni kuwa, Tanzania ni yetu sote na tunapaswa kufanya kazi pamoja, kuijenga, lakini hili linawezekana tu iwapo tutajenga uaminifu na kudai HAKI, pamoja na kuheshimiana”. Rais Samia Suluhu.

“Tumekubaliana kuwa, njia nzuri ya kuwa na maridhiano ni wakati kuna HAKI. Tumepitia madhila mengi, hakuna haja ya kuyarudisha mara kwa mara, badala yake tunapaswa kusonga mbele na kuwa na siasa safi na kuiunga mkono serikali”.- Freeman Mbowe.

“Mimi ndio mkuu wa jeshi la polisi leo nyie ni polisi kesho sio polisi lazima muwaheshimu watu na mtende HAKI kuna makosa mengine ya trafiki mweleweshe mtanzania mwenzako sio lazima kila kosa umuweke mahabusu”. - IGP Sirro.

“Kila mtu awe na HAKI ya kuchagua na kuchaguliwa na HAKI ya kutoa mawazo. Lazima wanachama wawe huru kutoa mawazo na hakuna mwenye hati miliki ya mawazo. Tukiweza kuimarisha HAKI ndani ya CCM tutakuwa tumeimarisha hadi nje kwenye maeneo mengine " Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM (Bara), Abdulrahman Kinana.

UHURU, HAKI, NA MAENDELEO YA WATU
 
Ni kama FAO LA KUJITOWA NSSF

Hii Tangañyika kuna mijitu INA ROHO MBAYA ZAIDI YA SHETANI
Ukatili wa sakata la fao la kujitoa tumeshajua sababu.
Report ya CAG imesema huko kwenye mifuko pesa inayo ingia ni chache kuliko inayotakiwa kulipa wastaafu.
Matokeo yake vijana wenye nguvu inabidi wanyimwe haki yao ya fao la kujitoa.
Hawajui hawa vijana wanahitaji mitaji wakajiajiri na kuajiri wenzao.
 
Ni kama FAO LA KUJITOWA NSSF

Hii Tangañyika kuna mijitu INA ROHO MBAYA ZAIDI YA SHETANI
Nchi hii kila mtu ana MATATIZO yake. Bahati mbaya wewe matatizo yako Hakuna atakayekumalia yakasikika.
 
Mahakama haitoi Haki bali inatafsiri sheria.
Ndio inatoa haki kwa kutafsiri hizo sheria, kwani aliyeivunja sheria amemnyima mwenzie haki yake, kama haki ingekuwa inatoka kwa Mungu pekee, basi Biblia na Quran ndio vingekuwa Katiba zetu.
 
“Kitu kikubwa tulichojadiliana ni kuwa, Tanzania ni yetu sote na tunapaswa kufanya kazi pamoja, kuijenga, lakini hili linawezekana tu iwapo tutajenga uaminifu na kudai HAKI, pamoja na kuheshimiana”. Rais Samia Suluhu.

“Tumekubaliana kuwa, njia nzuri ya kuwa na maridhiano ni wakati kuna HAKI. Tumepitia madhila mengi, hakuna haja ya kuyarudisha mara kwa mara, badala yake tunapaswa kusonga mbele na kuwa na siasa safi na kuiunga mkono serikali”.- Freeman Mbowe.

“Mimi ndio mkuu wa jeshi la polisi leo nyie ni polisi kesho sio polisi lazima muwaheshimu watu na mtende HAKI kuna makosa mengine ya trafiki mweleweshe mtanzania mwenzako sio lazima kila kosa umuweke mahabusu”. - IGP Sirro.

“Kila mtu awe na HAKI ya kuchagua na kuchaguliwa na HAKI ya kutoa mawazo. Lazima wanachama wawe huru kutoa mawazo na hakuna mwenye hati miliki ya mawazo. Tukiweza kuimarisha HAKI ndani ya CCM tutakuwa tumeimarisha hadi nje kwenye maeneo mengine " Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM (Bara), Abdulrahman Kinana.

Wanajua bila kutenda haki watatangulia kama yule wa chato
 
Haki ni ya Mungu pekee.

Binadamu tunatawalana kwa kuwekeana sheria zetu wenyewe siyo za Mungu!
Kama duniani hakuna haki wale wanaoenda mahakamani huenda kutafuta nini? usiniambie tena wajibu!.

Au unataka mtu akinyimwa haki yake (kuvunjiwa sheria na mwingine) aende kanisani au msikitini kupiga magoti?
 
Back
Top Bottom