Neno langu kwa wasaliti wote wanaorejea CHADEMA: Karibuni nyumbani, ila....

Uko sahihi kwa kiasi kikubwa. Lakini i wish watu wote tusome historia ya nchi mbali mbali ya uongozi vs vyama tujifunze. Kwenye siasa ukijifanya kufuata principal sana hutoboi. Kna wakati inabidi ugeuke nyuma na kula matapishi yako ili tu kuwafanikiwa. Yes, umakini inatakiwa uwepo lakini tusiwe rigid sana na kujiapiza. Ukisoma harakati za siasaza Kenya tangu wakati wa Moi, na jinsi kila uchaguzi wanasiasa wanavyobadilisha timu ili tu kuendana na hali halisi ya wakati husika utajifunza mengi. Huyu Rig G anayemtupia mawe ya kufa mtu uto sasa hivi waligombea wote urais na makamu. Kenyatta na Ruto sasa hivi haziivi ila once upon... walikuwa timu moja.
 
Alipewa b12 kumzuia Lissu asiwe mwenyekiti na akashindwa hivyi ni kweli ana deni kwa Samia.
 
Ila kwasasa ccm imedhoofika na kuparaganyika kabisa.. Kikichopo kwasasa ni makundi ya upigani sometimes yakisigina yenyewe kwa yenyewe
Mbona hiyo kawaida sana tangu enzi hizo. Ndiyo maana sisi kampeni zetu ni kuruhusiwa kwa mgombea binafsi. Hiyo ndiyo italeta mageuzi ya kweli katika nchi hii
 
Mawazo haya ni hatari na ndiyo maana wengine tunasita kuamini vyama. Hukitumikii chama ili upate madaraka, maana viongozi ni wachache na wanachama ni wengi. Uongozi ni dhamana tu. Mawazo haya ndiyo yaliyokiua chama cha mapinduzi, kikakosa mwelekeo hususan uongozi wa kupigiwa kura ulipokuwa ni ajira yenye marupurupu makubwa badala ya huduma.
 
Wewe ambaye sio msaliti, ukiwa mwanachadema una lipi la maana ulilolifanya ukiwa ndani ya chadema kuwazidi wakina Msigwa?
Unataka wote tuwe viongozi, ni mgawanyo wa majukumu, huwezi kumuona Heche au Katibu mkuu wa chama kila siku humu JF akianzisha uzi wa kukipambania chama kama Mshana Jr.

Anachofanya hapa JF ni kikubwa significant kwa chama kuliko machawa wanaosifia mauaji.
 
Unataka wote tuwe viongozi, hata anachofanya hapa JF ni kikubwa significant kwa chama kuliko machawa wanaosifia mauaji.
Sasa huoni kama unachanga hoja.. machawa na habari za kurudi chadema vina uhusiano gani
 
Mshana Leo umeuaaaa!!
Safi sana wakeleketwa wa chama
 
Tatizo vijana wanaweka hisia kwenye mambo yasiyohitaji hisia ndio maana wanaishia kuvunjika moyo.
 
Kwa mbwembwe na kashfa zake huyu mchungaji wakati anaondoka, wengi tukajiuliza maadili ya uchungaji wake kayaacha wapi huyu...?

Lakini tukajua tu kuwa kama ni pesa, basi kapewa furushi kubwa kwelikweli mpaka limemong'onyoa akili na ufahamu wake, likamtia kiburi na majivuno yaliyoanza kumsukumia kwenye mauti ya kuharibu kila alichokijenga kwa muda mrefu sana kwa jasho na damu akiwa CHADEMA...

Amerudi sawa. Lakini kuirejesha heshima na credibility aliyojijengea akiwa CHADEMA, itachukua muda mrefu sana unless otherwise...

Hata hivyo, binafsi, namuombea kwa Mungu Yehova amsamehe na kumpa nafasi ya pili tena...

All in all Mch Peter Msigwa aliondoka kwa mbwembwe na maneno mengi yenye karaha na kashfa akasahau kabisa methali za maonyo za wahenga wetu..

"Usitukane wakunga uzazi ungalipo"
au

"Uziwazomee mamba wakati hujauvuka mto"​

Ni wachache sana waliondoka CHADEMA kimya kimya wakitunza heshima na utu wao na ule wenzao waliowaacha...

Mfano mmoja ni aliyewahi kuwa katibu mkuu Dr Vincent Mashinji

Huyu jamaa alijiondokea kimya kimya. Inawezekana ni kwa sbb alifikia kupewa cheo cha madaraka ya uDC? uDED? (I am not sure, naweza kukumbushwa)
 
Hiki ndicho kile yule wa jana alisema"wenye" akili wanataka, tunaacha kujadili msmbo muhimu na kujikita kujadili watu!

Taifa lina mazonge mengi, yanayogusa maisha yetu sote, badala ya kuyaangalia hayo, tunatolewa kwenye mstari na mtu aliyefuata" taratibu zote" kurejea kwrnye chama.

Nsshauri tuache hawa, watapita, Tanzania itasalia magofu kama sio mahandaki na sisi tutabaki na stori kama za kibibi Gagula.
Angalia Tanzania inavyorejea nyuma kwa kasi katika kila kitu, tuwaache hawa na chama chao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…