Alisema nani na lini? Leta taarifa kutoka vyombo credible sio unaokoteza viblog vya huko Tandale.
Usikimbie swali, taja shambulizi moja tu hapo Iran ambao Israel walifanya wenyewe bila msaada wa marekani.
Ila na wewe umekosa uelewa wa mambo mengi!!
VIta pekee ambayo Israel imeshirikiana na Marekani moja kwa moja, ni hii ya mwaka huu.
Vita ya June mwakajana 2025, Israel iliipiga Iran bila ya kuwasiliana wala kuihusisha Marekani. Trump alitamka kuwa hata yeye alishtuka kwa sababu Israel haikuwahi kumjulisha. Wakati vita ikiendelea, Marekani ikaisihi Israel isimamishe vita, Netanyahu akasema hatasimamisha mpaka vinu vya nuclear vya Iran, vipigwe. Marekani ikafanya shambulio la siku moja la kupiga vinu vya nuclear, ikaiacha Israel iendelee na vita. Baada ya ombi la Iran kwa Umoja wa Ulaya, kuutaka umoja huo uingilie kati kusimamisha vita, umoja wa Ulaya ukamwomba Trump azungumze na Netanyahu, ndipo vita vikasimama.
Vita vyote vya huko nyuma kuanzia vile vya 1948, 1956, 1967, 1971, israel imekuwa ikipigana pekee dhidi ya mahasimu wake, japo ni kweli kuna wakati imekuwa ikinunua baadhi ya silaha toka Marekani. Lakini nyingi ya silaha hizo ni matokeo ya mradi wa ushirikiano kati ya Marekani na Israel kwenye tekinolojia ya silaha za kivita. Na pia kuna makubaliano kati ya Israel na Marekani, kwa Marekani kuipa Israel dola bilioni 3 kila mwaka kuimarisha sekta ya ulinzi kwa Israel, na hiyo inafuatia mchango mkubwa wa Waisrael waishio Marekani kwenye uchumi wa Marekani.
Did USA participate in 1967 israel war against arab countries?
No, the United States did not militarily participate in the Six-Day War. The U.S. provided diplomatic backing to Israel, but American forces did not fight or take part in combat operations during the June 1967 conflict.