Ad majorem
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 939
- 1,460
NETO wana hoja nyingi nzuri kuliko namna unavyotala waonekane..Acheni tu usaili wa walimu ubakie hivyo wazee. Labda kama kuna marekebisho basi yafanywe ila inerview ibaki.
Wazee niwaambie asilimia 70 ya walim wa NETO. hawako compitent. Yaan. Swala la kusahau content lipo deep sana.
Na kwa uziada wapo walopita shule kijanja janja tu so hawako na uwezo totally.... *sio kua wamesahau ila hawana uwezo. ...
Heb imagine Mwalim wa English hajui hata kuna aina ngapi za maneno (word classes) ... Kuna aina ngap za prepositions au hata issue ya tenses hajui kabisa... Ukimuuliza articles na function ndo kabiiisa. Ukitaka akimbie muulize grammatical errors ni nini na zipoje.
Mwali wa kiswahili hata kuchambua senyensi hajui . Aina na makundi ya ngeli hajui. Ukitaka akimbie muulize tu ushahidi wa kiisim kua kiswahili ni kibantu na aseme hatua za usanifishaji lugha.
Mwalim wa hesab anachojua ni kuchapa tu. Ila namna ya ku impart knowledge kwa kmtoto hajui
From there watu wataamka na kuanza kujishughurisha. .. me nawahakikishia kua wabongo ni waviv sana. .. acha wenye chembechembe za uchapa kazi waajiriwe kupitia usaili...
Ukinijib anzia penye hoja ya kuhusu kutafuta mwalim kwajil ya mwanao wewe .. unaambiwa huyu mwalim alipata 16 kwenye paper ya interview na huyu mwingine alipata 80. Je ni yupi ungependa akufundishie mtoto ??
Ukinijib kitu naomba ongeza comment. Tunafanya usaili kwa madaktari, kwa wanamichezo, marubani, madereva na hata kwa wake tunao waoa. Sasa why mwalim asifanyiwe interview ??.
Heb sogea mbele nikuulize ndugu, unadhani mwalim alofeli paper anafaa kufundisha somo husika ?
Nianze kwa ku declare interest. Mimi ni muumini wa Elimu bora hivyo naunga mkono interview kabla ya ajira yoyote including Ajira za ualimu.
Hata hivyo, mfumo wa usaili hauko fair. Na hilo ndilo NETO wanalolipigania.
Pili, NETO wanapigania usawa wa mishahara kwa walimu wanaofundisha kwenye shule za umma na wale wanaofundisha shule binafsi. Baada ya kuwa wahitimu wa fani za ualimu wamekua wengi, shule nyingi za binafsi, zilishusha mishahara. Kuna baadhi ya shule zimefika hatua ya kulipa mwalimu wa digrii mshahara wa laki moja. Huo ni unyanyasaji. Serikali inatakiwa iingilie kati. Kuna walimu ambao wanafanya kazi kwenye shule ambazo, wastani wa Mwalimu kwa wanafunzi ni Mwalimu mmoja kwa wanafunzi themanini. Halafu mwalimu huyo alipwe laki moja. Hio ni haki kweli?
Serikali inayojali raia wake haitakiwi kulifumbia macho hili.
Laiti wangesimamia vizuri, shule zikalipa mishahara kama ya shule za serikali, walimu jobless wangepungua mitaani na hizi kelele za sasa tusingeziona.
Kwenye hili, serikali waache kutumia polisi. Ni jambo la uelewa tuu ambalo linahitaji kauli moja tuu ya waziri na barua ya Katibu wa wizara kwenda kwenye shule binafsi na likaisha.