NETO punguzeni jazba: Tusiingize siasa kwenye elimu, tuache interview iamue nani aajiriwe

NETO wana hoja nyingi nzuri kuliko namna unavyotala waonekane.

Nianze kwa ku declare interest. Mimi ni muumini wa Elimu bora hivyo naunga mkono interview kabla ya ajira yoyote including Ajira za ualimu.

Hata hivyo, mfumo wa usaili hauko fair. Na hilo ndilo NETO wanalolipigania.
Pili, NETO wanapigania usawa wa mishahara kwa walimu wanaofundisha kwenye shule za umma na wale wanaofundisha shule binafsi. Baada ya kuwa wahitimu wa fani za ualimu wamekua wengi, shule nyingi za binafsi, zilishusha mishahara. Kuna baadhi ya shule zimefika hatua ya kulipa mwalimu wa digrii mshahara wa laki moja. Huo ni unyanyasaji. Serikali inatakiwa iingilie kati. Kuna walimu ambao wanafanya kazi kwenye shule ambazo, wastani wa Mwalimu kwa wanafunzi ni Mwalimu mmoja kwa wanafunzi themanini. Halafu mwalimu huyo alipwe laki moja. Hio ni haki kweli?

Serikali inayojali raia wake haitakiwi kulifumbia macho hili.
Laiti wangesimamia vizuri, shule zikalipa mishahara kama ya shule za serikali, walimu jobless wangepungua mitaani na hizi kelele za sasa tusingeziona.

Kwenye hili, serikali waache kutumia polisi. Ni jambo la uelewa tuu ambalo linahitaji kauli moja tuu ya waziri na barua ya Katibu wa wizara kwenda kwenye shule binafsi na likaisha.
 
Ndugu usibishe hilo lilifanyika kabisa kama unaweza kumpata mtu aliyehitimu kozi ya ualimu wa elimu ya hawali na makuzi ya mtoto kati ya mwaka 2015-2018 muhulize chuoni alifundishwa kwa lugha gani au muombe ata vyeti vyake uvipitie Hawa walimu walisoma mtaala wa kiswahili lakini kwenye usaili wameletewa lugha ya English
 
Kuna watu wanalipwa kwa kupinga ukweli, uhalisia. Pia wapo wanaolipwa kwa kusisitiza ushezi na upumbavu. Upumbavu, ushezi na ujinga kwa nchi za Afrika hutetewa kwa gharama kubwa. Obviously vitu vya maana havitetewi kwa gharama ya upumbavu na ushezi, na ndivyo vyenye mashiko, kuvipinga ni sawa na kupambana na mwanga kwa kutumia giza.
 
Wewe na mleta mada wote ni deluded. Anayeharibu sekta ya Elimu licha ya Jitihada za serikali ni waziri wa elimu. Mbona mfumo wa zamani wa Tamisemi haukuwahi kuleta malalamiko kiasi hiki?
 
walimu wasio na sifa hawastahili kupewa fursa ya kufundisha watoto wetu,

wanyinwe nafasi hizo wasije haribu kiwango bora cha elimu yetu 🐒
Sifa gani utazipata kwa interview ya maswali ya kuandika? Kama ni kujibu mitihani walishajibu kwa wataalamu kuliko hata wizara, huko vyuoni!
Hopeless Minister, Hopeless ministry!
 
Lakini pia jambo linalotia kinyaa ni uwepo wa michezo michafu ya rushwa ktk hizi idara zinazosimamia usaili kwa mfano mtu unapomuhoji kwenye oral interview Kwanini matokeo yake yasiwekwe kwenye account yake ajue kapata ngapi ?
Unashangaa tu mtu kaitwa kazini lkn ufaulu wake wa oral interview haujulkani maana yake ni kuwa ata ukifanya interview zote Bado anayeamua nani wa kuingia kazini ni mtu na si alama zake za ufaulu
 
Nawe utakuwa hopeless kama waziri.
Vyuo vyote vinatoa elimu ya ualimu kwa usimamizi wa wizara, na kukaguliwa na wizara. Baadaye waziri anajidai hatambui ubora wa wahitimu.

Tumedekeza kila waziri kuja na upuuzi wake na kufanya ndo mahitaji ya taifa. KIla waziri anakuja na ujinga wake!
 
Dah. Tunahitaji san watu wenye weredi wa kufikiri wa namna yako. Aise
 
Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo! Ingawa naona kuna watu wanashangilia. Yaani huoni tofauti ya waalimu na hao wahasibu?

Waalimu wanasoma vyuo vya wizara ya elimu. Hata walio vyuo binafsi, mitaala yao na ubora wake inasimamiwa na wizara ya Elimu Wanaajiliwa na wizara ya Elimu. Huoni Tofauti? Madaktari gani wanaoajiliwa kwa usaili nchi hii? Hao wahasibu wanaajiliwa na wizara ya Uhasibu? Ipo? Mitaala yao inasimamiwa na wizara ya Uhasibu? Ipo?

Nakupa mifano hiyo ili angalau uwe na akili. Kwamba Wizara ya elimu inafanya ujinga na waziri wao. Yaanio imesimamia ubora wa wahitimu na kuridhika nao, na kutoa vyeti. Baadaye wakitoa ajira, waziri anasema kama mlevi eti ubora wao sijui nyoko gani vile!
 
Zamani mfumo wa uajiri walimu walikuwa wanachukuliwa moja kwa moja na kila kitu kilikuwa kiko sawa, ni kuwashauri viongozi walete mfumo huo .
Hoja yako ni dhaifu sana. Hiyo zamani waalimu walikuwa wachache sasa hivi ni wengi kuliko mahitaji. Hata kada zingine walikuwa wanachukuliwa tu bila kuwa na mambo mengi. Na kadiri miaka inavyosonga uhitaji utazidi kuwa mdogo. Kama nchi tufikirie jinsi gani ya kupunguza ukubwa wa tatizo kupitia ujasiriamali na uwezeshaji wa sekta binafsi.
 
Ukiwa mwongo usiwe msahaulifu, katika hotuba na mihadhara ya kielimu mmesema upungufu wa waalimu Tanzania kwa uwiano na wanafunzi unaopendekezwa na walioleta huu hii formal education ni tuna upungufu wa 276,000 na Mtaani wako nusu ya hiyo pengo kufikia uwiano.. unawezaje kusema wako wengi kuzidi?

Hiyo zamani unayodai kilikuwa na shule chache sana na wengi tuliosoma privates ingawa tulifaulu sio kwamba tulikuwa na hela ni uchache wa mashule sasa yameongezwa Katibu Kila Kijiji na bado yanajengwa Kisha mnasema nafasi chache waalimu wengi!!!!!! 🙄🙄🙄
 
Haki yao kulalamika
Binafsi sikubaliani mwl aliyehitimu na vyeti vya kuthibitisha hilo anavyo,hapo ni kumpa kazi tu, unamsaili mtu kama unataka kumpa kazi ambayo hajaisomea.
Kinachotakiwa ni kupimwa afya tu, kwa sababu inawezekana wakiwa huko nje wamepata magonjwa.
 
Kumpima afya kunahusianaje na ualimu wake. Halafu huko nje wapi wakati wengine wana magonjwa ya kuzaliwa nayo au kurithi
Binafsi sikubaliani mwl aliyehitimu na vyeti vya kuthibitisha hilo anavyo,hapo ni kumpa kazi tu, unamsaili mtu kama unataka kumpa kazi ambayo hajaisomea.
Kinachotakiwa ni kupimwa afya tu, kwa sababu inawezekana wakiwa huko nje wamepata magonjwa.
 
Una uhakika walikuwa wachache!?? Bro kipindi hicho tunasoma watu wengi walikuwa wanachagua kusoma ualimu kwa sababu mkopo walikuwa wanatoa 100% .

Hoja yako ni dhaifu..mimi ni mwana CCM damu na kadi ninayo na nalipia ila katika ili tusaidie vijana wapate ajira.

"Acha kuendekeza uchawa ,saidia vijana wapate ajira"
 
Wewe umeshaamua kutoelewa kwa hiyo hata nikikuelewesha hutaelewa.
 
NETO wengi ni vijana waliofeli, au kuana na ufaulu wa chini sana,
hawana sifa na kwakweli hawaajiriki.

NETO ni hatari kwa ustawi wa taaluma mashuleni 🐒
Yaani wewe ni mjuaji wa kila kitu!! Nikizaa toto lenye kiherehere kama wewe NALICHINJA
 
Waliofaulu INTERVIEW walipata low macks kwenye mtihani wa NECTA. Wasiwasi wetu upo hapo
 
Inaonekana unaishi nyuma ya kuda, au hufuatilii vitu, katika hoja ulizotoa zinaonekana hufaham mambo mengi yanaoendelea kwa sasa.
1. Madakatari ndio wanaajiliwa kwa kufanya usaili. Kuanzia mwaka jana.
2. Vyuo vingi wanavyosoma wahasibu na madaktari ndio hivyo hivyo husoma walimu. Mfano UDOM na UDSM,
3. Sio kila anahitimu anakua amaiva vizuri.

Unaeza kukosoa lkn huwezi kusema usaili uondolewe. Kwanza unagopa nini kusailiwa na ulipita vzr kwa viwango vizuri. Hata private sector wanakuafanyia usaili, kwann wasitumie vyeti vyako tu kukuajiri.

Naamin mchakato huu ni negative lakn ni wakati watu kukubali kuwa kwa sasa ajira na maisha yamekua ya ushindani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…