Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

#TANZANIA:
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesisitiza wapangaji katika nyumba za kupanga kuwa wazalendo na kulipia asilimia 10 ya kodi wanazokuwa wakilipa kwa wenyenyumba ili kulipia kodi ya pango.

Source-MwanzoTv
 
Hahahahah hio TAX mi nikilala nazalisha nini hapo nyumbani? Nawasubiria kwa hamu na nimejiandaa kulala mahabusu safari hii!
Naomba kujua ile buku ya kila mwezi inayokatwa kupitia luku ni kodi ya nini?
 
Mwenye nyumba ndio alipe sio mpangaji! Hizo sheria kandamizi wanazojitungia tungia tu zitawafikisha mahali fulani maana hazitekelezeki
Basically analipa mwenye nyumba kwa mawazo ya Mwigulu na genge lake. TRA inawaomba wapangaji “wawe wazalendo” na waikate 10% juu kwa juu na kumpa mwenye nyumba 90% ya kodi ya pango ili hiyo 10% mpangaji asaidie kuipeleka TRA

Nani ana muda huo? Wenye nyumba hawatokubali na hakuna mpangaji mwenye moyo huo
 
#TANZANIA:
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesisitiza wapangaji katika nyumba za kupanga kuwa wazalendo na kulipia asilimia 10 ya kodi wanazokuwa wakilipa kwa wenyenyumba ili kulipia kodi ya pango.

Source-MwanzoTv
Kumekucha
 
Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi kupitia Ukurasa wake wa Instagram, imeeleza kuwa;

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imesisitiza wapangaji kuwa wazalendo na kulipia asilimia 10 ya kodi wanazokuwa wakilipa kwa wenyenyumba ili kulipia kodi ya pango.

Akiwa katika mafuzo ya wafanyabiashara juu ya mabadiliko ya sheria ya kodi mwaka 2022 wilayani Bariadi, Ofisa huduma na elimu mkuu kutoka TRA, Eugenia Mkumbo amesema kifungu cha 82(2) (a) cha sheria ya kodi kimefuta msamaha wa kodi kwa wapangaji binafsi hivyo kuwapa mamlaka wapangaji wote kuzuia kodi ya pango katika nyumba binafsi na zile za biashara ili kurahisisha ulipaji na ukusanyaji wa kodi ya pango.

"Kama umepanga chumba kiwe cha biashara au makazi unajukumu la kukata asilimia 10 na kuilipa TRA na mwenye nyumba utampelekea nakala ambayo inaonyesha umelipia kodi utaambatanisha na pesa iliyobaki unampa mwenye nyumba" amesema Eugenia.

My take
Awamu ya sita inazidi kuupiga mwingi na kuleta furaha katika mioyo na nyuso za watanzania, ama kwa hakika watanzania Mungu awape nini tena ? manataka Rais wa aina gani nyie? nchi inasonga mbele kwa kasi Tozo zinajenga nchi ,matumizi yamebanwa , pesa haziibiwi, mafisadi yamebanwa, raha sana

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia mabadiliko ya Sheria ya Kodi ya Mwaka 2022, imeanza kusimamia sheria inayowapa mamlaka wapangaji wote kuzuia kodi ya pango katika nyumba binafsi na zile za biashara ili kurahisisha ulipaji na ukusanyaji wa kodi ya pango.

=======
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesisitiza wapangaji katika nyumba za kapanga kuwa wazalendo na kulipia asilimia 10 ya kodi wanazokuwa wakilipa kwa wenyenyumba ili kulipia kodi ya pango.

Hayo yamesemwa na Ofisa Huduma na Elimu Mkuu wa TRA, Eugenia Mkumbo katika mafuzo ya wafanyabiashara juu ya mabadiliko ya sheria ya kodi mwaka 2022, leo Alhamisi Agosti 25, 2022 wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu.

Amesema kifungu cha 82(2) (a) cha sheria ya kodi kimefuta msamaha wa kodi kwa wapangaji binafsi, hivyo kuwapa mamlaka wapangaji wote kuzuia kodi ya pango katika nyumba binafsi na zile za biashara ili kurahisisha ulipaji na ukusanyaji wa kodi ya pango.

"Kama umepanga chumba kiwe cha biashara au makazi unajukumu la kukata asilimia 10 na kuilipa TRA na mwenye nyumba utampelekea nakala ambayo inaonyesha umelipia kodi, utaambatanisha na pesa iliyobaki unampa mwenye nyumba," amesema Eugenia

Aidha, amesema Serikali imefuta kodi kwa wanafunzi wanaokwenda kupata mafunzo ya vitendo kwa lengo la kuwarahisishia waajiri kuwapa nafasi ya kupata uzoefu wa kazi kwa urahisi wanafunzi wanaohitimu masomo.

Akifafanua kuhusu kodi ya pango, Kissa Kyejo, Afisa Mkuu Usimamizi wa Kodi amesema mfanyabiashara ni mbia wa Serikali na anapaswa achangie kipato unachopata kwa kulipa kodi.

"Yule mwenye nyumba anapata kipato kwa sababu analipwa na wapangaji lakini TRA tunaweza tusimfikie mwenye nyumba kwa sababu hana namba ya utambulisho wa mlipa kodi.

“Pengine amejenga nyumba na sio mfanyabiashara sheria, ilichofanya ni kwamba mpangaji ambae ndie anamlipa mwenye nyumba kipato aweke zuio na kulipa kodi ya pango," amesema

Baadhi ya wapangaji katika mji wa Bariadi, wamesema kodi hiyo ni kama mgogoro kati ya wenye nyumba na wapangaji kwa sababu ni kazi ngumu kumlipia kodi mtu ambaye hajaamua kulipa kodi kwa hiari.

"Kabla ya kumpa mamlaka mpangaji kuzuia hela ya pango ili kulipa kodi, wangewaita wenye nyumba na kuwapa elimu ili wawe tayari kukatwa pesa zao lakini saizi itakuwa ni changamoto sana kwa sababu wengi hawajui hata hiyo kodi inahusu nini," amesema John Lucas mkazi wa Kidinda.

Chanzo: Mwananchi
Mwenye nyumba ndio mwenye jukumu la kulipa maana hapo kwenye kiasi cha Kodi unachomlipa mwenye nyumba inakatwa 10% na Kwa msingi huo lazima kuwe na makubaliano ya kwenye Mkataba wa upangishaji..
 
Do you copy, do you copy over.
255 men down men down over.
Roder that.
 
Basically analipa mwenye nyumba kwa mawazo ya Mwigulu na genge lake. TRA inawaomba wapangaji “wawe wazalendo” na waikate 10% juu kwa juu na kumpa mwenye nyumba 90% ya kodi ya pamgo ili hiyo 10% mpangaji asaidie kuipeleka TRA

Nani ana muda huo? Wenye nyumba hawatokubali na hakuna mpangaji mwenye moyo huo
Hapo zitaanza habari za kutishiana matofali baina ya mpangaji na mwenye nyumba. Tunaoishi kwenye nyumba za urithi kazi ipo.
 
TRA imewashindwa wenye nyumba sasa inataka wapangaji wagombane na wenye nyumba. Kweli kwa maisha yetu ya kibongo umwachie mpangaji akate 10% si unataka umfakaranishe na mwenye nyumba na aishie kufukuzwa? Sijui tunaelekea wapi!
 
Waweke na tozo ya uhai kabisa na iwe ni 10,000 kila mtu aamkapo salama alipe ili akili ziwakae sawa
 
Eti mpangaji atoke nyumbani, alipie usafiri hadi TRA, aunge foleni kulipa withholding tax. Hizo gharama zake atalipwa na Nani,?!

Kama ni uzalendo na wao waache kutumia Ma-vieit mjini wapande Harrier!
Na huyo mpangaji akifanya hivyo and then akamletea mwenyenyumba kodi ambayo imepungua 10% atambiwa hi kodi yako ikiisha nataka chumba changu

Hata hao wenye Nyumba zenye fremu za biashara hi kodi hawalipi badala yake analipa mpangaji kwa kulazimishwa na TRA na mpangaji analipa hiyo 10% ya pango ili kukubali yaishe na sio kama TRA hawalijui hili wanajua vizuri sana kama hi kodi inalipwa na mpangaji na si Mwenye Nyumba



Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Waiweke tena kwenye LUKU ili kuepusha kukimbizana kimbizana barabarani
 
Nashauri hizi sheria zingeanza na elimu ya mlipa kodi kama ilivyo fanyiwa sensa ila viongozi wanakaa na kuamka tu kodi ya mpangaji si vizuri sana
 
Unakuta mpangaji kakaa na zuio miezi sita hajapeleka kisha mwezi wa saba anahama na kodi ya nyumba
 
Back
Top Bottom