Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

Ngoma Inogile: Wapangaji sasa kulipa asilimia 10 ya kodi TRA

Mpangaji unatakiwa kuzuia 10% ya kodi unayolipa. Mfano kodi yako kwa mwaka ni 2m unapeleka tra 200,000/- mwneye nyumba unampa 1.8m na ushahidi kuwa umelipa 10% tra.
Atakachokifanya ataongeza kodi badala ya kuwa 2m itakuwa 2.25 ili hiyo itakayoongezeka ndo uipeleke TRA yeye atabaki na fedha yake.
 
Nyumba za kupanga sio biashara rasmi sana ndio maana wengi hatujui...

Lakini kwa watu wenye fremu, apartments zenye leseni ya biashara huwa wanafanya withholding tax kwa niaba ya wapangaji...

Hivyo wewe mpangaji utaona umetoa kodi yako kama kawaida, lakini mwenye nyumba anarejesha 10% ya serikali huko 'tiaraei'...
Anakuongezea kodi tu. Mwisho wa siku maumivu ya mwisho ni mpangaji.
 
Hizi hela tunazokamuliwa hivi zinaenda wapi??? Double Tozo+double kodi + mikopo+ kupanda bei ya vitu hovyo hatar sana,,,,yani ikifika 2025 hakuna kilichofanyika sijui kama kuna raia ataelewa!
 
Mwenye nyumba atakuambia kaishi huko TRA pale hela yake isipotimia
 
Mpangaji unatakiwa kuzuia 10% ya kodi unayolipa. Mfano kodi yako kwa mwaka ni 2m unapeleka tra 200,000/- mwneye nyumba unampa 1.8m na ushahidi kuwa umelipa 10% tra.
Hiyo Kodi mwisho wa mwisho siku atakaebebeshwa ni Mpangaji.
 
Hii ni nzuri, mradi tu wajitahidi kodi hii ilipwe na wenye nyumba tena wangejitahidi kuweka system ambayo haikwepeki kabisa.
 
Naona mahomeless wakiongezeka dar,,,Maisha yalivyokua magumu hivi hakuna mwenye nyumba atakayekubali hela yake kukatwa HAKUNA!!!Hapo ataona bora aachiwe nyumba yake au kodi iongezeke!!!
 
Hapo mwenye nyumba lazima apandishe kodi ili kuziba pengo matokeo yake ni maumimivu kwa sisi tusio na nyumba. Ila kwa jicho lenye kuona mbaaali, gharama za maisha zinaenda kupaa tena maana mpangaji nae atapandisha bei ya bidhaa au huduma atoaye kwa wengine ili kufidia ongezeko la pango.

Sauti ya akina nape iliyonaswa na Magufuli ndio inafaa kutumika awamu hii kuwa nchi inatawaliwa na ....
Zinaenda huku
20220825_191727.jpg
 
Anakuongezea kodi tu. Mwisho wa siku maumivu ya mwisho ni mpangaji.

Wenye fremu zinazokaguliwa mahesabu na TRA wanafanya withholding na bado haijaathiri bei za pango za fremu...
 
Kwa uelewa wangu ni kuwa kodi hiyo anayelipa ni mpangishaji

Kama unalipa pango 100,000 maana yake sh 10,000 inabidi iende TRA na sh 90000 atachukua mwenye nyumba

Waandishi wa habari uandishi wao ni wa kuokoteza sana, maana hii kodi ipo tu sema utekelezaji ndiyo changamoto
Hiyo 100 alipanga mwenye nyumba mwenyewe kwahiyo ukienda kulipa 10 TRA jiandae kulipa 100 ambayo jumla itakuwa 110
 
Najua hlo kwa upande wa biashara na kinachofanya huko iwe na wepesi ni kwasababu mfanyabiashara anahitaj idhini ya TRA na hatua hyo ya kulpa hyo 10% ni kigezo kimoja wapo

Ila sasa kwa hizi nyumba za makazi naonelea ni vizur mwenye nyumba ndio angehusika.

Kwa lugha nyingine, muda si mrefu TRA au serikali inaweza ikairasimisha biashara ya nyumba za kupanga, ikalazimu mtu awe na kibali na leseni ya biashara 😊
 
Msisahau kuwa hii kodi wameambiwa walipe wakaazi wa Bariadi pekee, so kama wewe huishi Bariadi hiyo kodi haikuhusu.
 
Back
Top Bottom