Ng'ombe mwenye thamani ya IST

Ng'ombe mwenye thamani ya IST

mkuu we ni mfugaji au ni mtazama video za wafugaji yutubu?
Naam mkuu, ni mfugaji mtarajiwa.

Kupitia mada za humu JF na video za YouTube, nimeshashawishika kwa zaidi ya asilimia tisini. Huenda na mimi nikaanza kufuga muda si mrefu. Kuna vitu vichache bado nafuatilia, nikishajiridhisha, mradi unaanza mara moja.
 
ufugaji unalipa mkuu, juzi kati nilimtembelea bi mkubwa kijijini kauza dume mdogo tu kwa 1.5m, nilishangaa sana
 
Ila nyie motivation speakers huwa mnaongea vitu kiurahisi rahisi sana
Kuna motivation speaker mmoja alisema alianza kuuza fungu moja la mchicha Sasa hivi anauza michocha kupeleka nje ya nchi makontaina Kwa makontaina ya michicha yanaondoka Kila siku bandari ya Dar es salaam kwenda ulaya
 
Motivation
Ng'ombe haitaji kula majani tu ili kukamuliwa
Kuna kuacha kunyonyesha kwa kipindi fulani na kuna kipindi cha mimba na sidhani kama huwa ananyonyesha kwa mwaka mzima
Kwa ufugaji wa kisasa, kunyonyesha si lazima mkuu.
 
hii hesabu haina uhalisia mkuu, utaingia chaka buree, halafu lita 60 kwa siku? sipingi ila kwa tanzania sidhani kama kuna ngombe wa kutoa hzo lita kwa siku.
Lakini mfugaji kasema anapata lita 60 kwa siku mkuu.
 
Kwa maelezo yake yanauzwa almost yote mengine anajiuzia mwenynyewe kwenye miradi mingine ya mbwa..Ng'ombe inakamuliwa mara tatu sio mchezo kwa huku nilipo bei ya lita ni 2000×60=120000 kwa siku kwa ng'ombe mmoja kwa mwezi unaongelea Tsh 3,600,000/= kwa mwaka unaongelea Tsh 43,200,000/= endapo ngombe atakamuliwa mwaka mzima kitu ambacho ni nadra sana maana kuna majira huwa wanakaaaida ya kupunguza utoaji.

Mzee apewe pongezi sana ameamua kwakweli.
✅🙏🙏🙏
 
kwa hyo jk yeye ana ng'ombe kama hao? kuna mwamba alishasema hapa jf kuna kwenye baadhi ya ranch za taifa tuna pure breed ya boran, ambao nao kwenye uzito wanatisha.
Kama ni kweli apongezwe👏👏👏
 
Duuh,lita 1500??

Dsm tunauziwa 2000
Pembezoni ni 1,000 au 1,500 sana sana 1,000 Lita 1 huko maeneo ya pembeni mwa mji huku katikati ya mji ni 2,000 mpaka 2,800/3,000 inategemea ulipo
 
ufugaji unalipa mkuu, juzi kati nilimtembelea bi mkubwa kijijini kauza dume mdogo tu kwa 1.5m, nilishangaa sana
Hukupaswa kushangaa, bali kusikitika, na ingebidi, kuunda tume itakayomsaidia kujua sababu iliyopelekea ng'ombe kuuzwa bei ndogo hivyo.

Hata mimi, kwa "Jana", ningeweza kushangaa kama wewe.

Lakini baada ya kupitia majarida kadhaa ya huko "duniani", nimegundua ng'ombe ni bei kubwa sana. Ng'ombe anauzwa zaidi ya sh bilioni moja😀
 
Hapo bado hujalipa mkata majani + gharama ya usafirishaji
Kuna biashara zingine kichaa
Kuna mzee nilimtembelea ni mstaafu akaamua kuwafuga kwake kama watano
Nikamuuliza vipi lishe akasema nilikuwa nawaletea majani ila mwisho nikaajiri kijana nikanunua na Guta
Dogo alifanya mda tu akaondoka mazima na Guta hakurudi tena
Halafu mtu anakuambia hesabu za alinacha eti unapata 32m
Akifa je na huyo dogo nae
 
Kuna motivation speaker mmoja alisema alianza kuuza fungu moja la mchicha Sasa hivi anauza michocha kupeleka nje ya nchi makontaina Kwa makontaina ya michicha yanaondoka Kila siku bandari ya Dar es salaam kwenda ulaya
Mpe maua yake🙏
 
Kuna biashara zingine kichaa
Kuna mzee nilimtembelea ni mstaafu akaamua kuwafuga kwake kama watano
Nikamuuliza vipi lishe akasema nilikuwa nawaletea majani ila mwisho nikaajiri kijana nikanunua na Guta
Dogo alifanya mda tu akaondoka mazima na Guta hakurudi tena
Halafu mtu anakuambia hesabu za alinacha eti unapata 32m
Akifa je na huyo dogo nae
Inawezekana mkuu. Ingia mtandaoni uone wsnavuonufaika wafugaji wa huko "dunianai"
 
Back
Top Bottom