Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,718
- 3,465
Juni 10 si ndio jana ambapo tuliambiwa na Yule Bwana kwamba hali ni tulivu?
Tuna PM wa ovyo sana. That loony is a pathological liar!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Juni 10 si ndio jana ambapo tuliambiwa na Yule Bwana kwamba hali ni tulivu?
Ivi mnataka aende kinyume na maagizo ama vipi.Yule jamaa tangu atangazie uma kwamba mzee anachapa kazi wakati mzee amelala yaani imani yangu...
Wapewe fidia wahame!
Hiyo handeni ni kubwa balaa...I love the place
Poa tu ajali kazini Ala wawache washkaji zetuAskari Polisi mmoja ameuawa kwa kupigwa mshale wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati wa zoezi la uwekaji mpaka katika eneo la pori tengefu kwenye Tarafa ya Loliondo.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella akisema kwamba kifo hicho kilitokea Juni 10 alasiri, na kusisitiza kwamba kama serikali wanatambua uzalendo wa askari huyo.
Ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro kuwa watulivu na kusikiliza maelekezo ya serikali katika zoezi la uwekaji mipaka.
Wananchi wanatakiwa na Serikali kuhama katika eneo la Ngorongoro na kwenda kuishi Handeni, Tanga ambapo Serikali itawasaidia katika kuhama. Nia ikiwa ni kuhakikisha uhifadhi endelevu katika Hifadhi ya Ngorongoro.
Baadhi ya Wananchi wa Ngorongoro hawataki kuhama katika ardhi yao ya asili kwani Wanaishi hapo kisheria na Wanatambulika.
View attachment 2257198
Basi waende wakakaushe maji kwenye mito ili iendelee kubaki ardhi kama kawaidaAridhi yote Tanzania ni mali ya serikali inauwezo wa kuipangia matumizi yoyote kwa mda wowote, labda mbadili katiba iondowe hicho kipengere
Askari ameuawa halafu unasema hali ni shwariAskari Polisi mmoja ameuawa kwa kupigwa mshale wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati wa zoezi la uwekaji mpaka katika eneo la pori tengefu kwenye Tarafa ya Loliondo.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella akisema kwamba kifo hicho kilitokea Juni 10 alasiri, na kusisitiza kwamba kama serikali wanatambua uzalendo wa askari huyo.
Ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro kuwa watulivu na kusikiliza maelekezo ya serikali katika zoezi la uwekaji mipaka.
Wananchi wanatakiwa na Serikali kuhama katika eneo la Ngorongoro na kwenda kuishi Handeni, Tanga ambapo Serikali itawasaidia katika kuhama. Nia ikiwa ni kuhakikisha uhifadhi endelevu katika Hifadhi ya Ngorongoro.
Baadhi ya Wananchi wa Ngorongoro hawataki kuhama katika ardhi yao ya asili kwani Wanaishi hapo kisheria na Wanatambulika.
View attachment 2257198
Samia alipoongopa kifo cha Magufuli akiwa Tanga hakuongea maneno ya shombo ya Majaliwa. Mnataka Rais aje mumuone Magomeni? Kamateni wanaosema Rais mgonjwa! Nyinyi ni maadui wa nchi.Lakini wote na malikia hangaya nae aliongopa enzi zile
Aridhi yote Tanzania ni mali ya serikali inauwezo wa kuipangia matumizi yoyote kwa mda wowote, labda mbadili katiba iondowe hicho kipengere
Wamejengewa nyumba huko,maji na huduma za afya,Kuna watu wapo nyuma yao
Kaulize mgodi wa bulyanhulu watu walihamishwa vipi..pakiwa na maslahi ya nchi utahama tu,hao walihamishwa kistaarab tu,Sasa hv wanaleta ununda..utakutana na dolaWewe ndio upo nyuma yao. Kuhama kule ni hiari halafu mnatumia risasi kuhamisha watu. Huo sio uungwana.
Wilaya ya Ngorongoro ina tarafa 3 Loliondo,Ngorongoro na Sale tarafa ya Ngorongoro ndiko kunapatikana kreta ya Ngorongoro na pia ndiyo ilipo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro jina hili ndiyo jina la wilaya lakini makao makuu ya wilaya yapo Loliondo mbali sana kutoka Hifadhi ya Ngorongoro Wamasai wanaohamishwa ni wale wanaoishi kwenye eneo la Hifadhi ya Ngorongoro iliyopo tarafa ya Ngorongoro Taarifa ya askari kupigwa mshale kama ni kweli basi tukio hilo litakuwa limetendwa nje ya Tarafa ya Ngorongoro na zaidi ya hapo Wamasai hawatumii sana mishale kabila wanaotumia sana mishale tena kwa weredi mkubwa ni kabila la Wasonjo wanaoishi tarafa za Loliondo na SaleNgorongoro na Loliondo!!!! mbona vinachanganya
Wananchi wapi wanatakiwa kwenda Handeni?
Ni wanachi wa tarafa ya Ngorongoro, Loliondo au wote?
Sisi tushakukufa sana tu.Mkifa ninyi msilalamike pia, tit for tat
Apewe eneo ZanzibarMwe
Mwekezaji yoyote kitu Cha kwanza ni kuwa na mahusiano mazuri na wananchi wanaomzunguka, unawekezaje katika sehemu ya mgogoro?
Hapewe hifadhi ya bugiri period,
Yule bwana huenda dishi haliko sawa.Juni 10 si ndio jana ambapo tuliambiwa na Yule Bwana kwamba hali ni tulivu?
kuwa mwenyeji haimaanishi ni kwako, ardhi yote ni mali ya serikali na inaweza kubadilishwa matumizi mda wwte, kuna watu wanawapa viburi wamasai halafu wao wako nyuma ya keyboardKwani kati ya Wamasai (wenyeji wa hilo eneo), wanyama na Waarab! Nani wenye haki ya kuishi hilo eneo?
Wapigania uhuru walikuwa wakipigania nini?kuwa mwenyeji haimaanishi ni kwako, ardhi yote ni mali ya serikali na inaweza kubadilishwa matumizi mda wwte, kuna watu wanawapa viburi wamasai halafu wao wako nyuma ya keyboard
Tulia anajulia wapi vita vya kiuchumi? Yaani tumeshindwa kupromote utalii kwa vivutio lukuki, tatizo dogo tu la Ngorongoro tunaona tunahujumiwa au vita ya kiuchumi?Jana spika WA Bunge kasema hivi ni vita vya uchumi yaani Tanzania itakuwa na laana tu
Serikali ni nani?!kuwa mwenyeji haimaanishi ni kwako, ardhi yote ni mali ya serikali na inaweza kubadilishwa matumizi mda wwte, kuna watu wanawapa viburi wamasai halafu wao wako nyuma ya keyboard
Usitukumbushe maumivu hayo! Wasichojua ni kuwa Mungu anawaona!Yule alisemaga Maghufuli anabarizi ikulu kumbe hola!!