BREAKING: MFALME WA SOKA DUNIANI PELE AAGA DUNIA
Gwiji wa soka wa Brazil Pele amefariki dunia leo kufuatia kuugua saratani kwa muda mrefu, wakala wake Joe Fraga na familia yake wamethibitisha.
Wawakilishi wa Pele walitangaza kifo chake kwenye mtandao wa kijamii wa nyota huyo wa michezo: "Msukumo na upendo viliashiria safari ya Mfalme Pele, ambaye aliaga kwa amani leo."
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mara tatu, ambaye jina lake halisi ni Edson Arantes do Nascimento, anakumbukwa kwa mafanikio yake mbalimbali, kwenye uwanja wa soka na nje ya nchi.
Chapisho la ukumbusho kwenye mtandao wa kijamii wa Pele liliangazia kisa cha kimataifa cha nyota huyo, likirejelea tukio wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Nigeria wakati pande zinazopingana zilikubali kusitishwa kwa mapigano ili kufurahia mechi ya Pele iliyochezwa nchini humo.
"Katika safari yake, Edson aliuchangamsha ulimwengu kwa kipaji chake katika mchezo, akasimamisha vita, akafanya kazi za kijamii duniani kote na kueneza kile alichoamini zaidi kuwa ni tiba ya matatizo yetu yote: upendo. Ujumbe wake leo unakuwa urithi kwa vizazi vijavyo,” ujumbe huo kwenye mtandao wa kijamii wa Pele ulisomeka.