TANZIA Nguli wa Soka Duniani, Mbrazili Pele afariki dunia

TANZIA Nguli wa Soka Duniani, Mbrazili Pele afariki dunia

Ila wadada bana, haya mambo ya mpira huwa mnalazimisha tu!

[emoji28][emoji28][emoji28]
He had a great talent,it would have been nice to see him sharing his skills with youngsters too just like other great footballers do e.g zizou
 
BREAKING: MFALME WA SOKA DUNIANI PELE AAGA DUNIA

Gwiji wa soka wa Brazil Pele amefariki dunia leo kufuatia kuugua saratani kwa muda mrefu, wakala wake Joe Fraga na familia yake wamethibitisha.

Wawakilishi wa Pele walitangaza kifo chake kwenye mtandao wa kijamii wa nyota huyo wa michezo: "Msukumo na upendo viliashiria safari ya Mfalme Pele, ambaye aliaga kwa amani leo."

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mara tatu, ambaye jina lake halisi ni Edson Arantes do Nascimento, anakumbukwa kwa mafanikio yake mbalimbali, kwenye uwanja wa soka na nje ya nchi.

Chapisho la ukumbusho kwenye mtandao wa kijamii wa Pele liliangazia kisa cha kimataifa cha nyota huyo, likirejelea tukio wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Nigeria wakati pande zinazopingana zilikubali kusitishwa kwa mapigano ili kufurahia mechi ya Pele iliyochezwa nchini humo.

"Katika safari yake, Edson aliuchangamsha ulimwengu kwa kipaji chake katika mchezo, akasimamisha vita, akafanya kazi za kijamii duniani kote na kueneza kile alichoamini zaidi kuwa ni tiba ya matatizo yetu yote: upendo. Ujumbe wake leo unakuwa urithi kwa vizazi vijavyo,” ujumbe huo kwenye mtandao wa kijamii wa Pele ulisomeka.

1672366140688.jpg
 
R. I. P Edson Arantes do Nascimento...
Bile... Pele..
Asante kwa kutuburudisha, katika mpira.
#King 🤴
#Legend of all Legends...
#Greatest player of all time...
 
R. I. P Legend.
Ukapumzike kwa amani. 🙏
Sikuwahi kukushuhudia ila kwa taarifa zilizopo ulifanya makubwa sana. Wataibuka wengine wenye vipaji kama ww au zaidi.
Sasa huyu unaemuambia haya maneno anayaona kweli?
 
Tulitegemea kuliona hili likizungumzwa

Bila kuona vitu kama hivi unafikiri tutajuaje kuwa tupo bongo??

Just incase umesahau au hukuwa na taarifa ni kwamba siku ya christmas familia yake ilienda kusheherekea hospitali pamoja naye.

Picha zilitumwa na video zilionesha tena akiwa katika tabasamu kubwa
Wabongo na hisia za kudanganywa muda wote..😂😂
 
Sitaki kuingia kwenye ligi ya maneno na nyie

Msije mkanisema na mimi nikafa bure
Kwamba mashariki wa Messi wamekuwa kama wazaramo😂😂. Wanakichamba Hadi unadead?
 
RIEP legend

Brazil wangechukua tena kombe mwaka huu ingekuwa kama heshima fulani hivi kwake in his last days

Sababu ilishasemekana hatoboi next year
Kachukua mess maaana alikuwa anamuhusudu sana LEO
 
Back
Top Bottom