Nguruwe mmoja anaweza kukupa hadi zaidi ya TSh. Milioni 1 ndani ya muda huu tu!

Nguruwe mmoja anaweza kukupa hadi zaidi ya TSh. Milioni 1 ndani ya muda huu tu!

Labda kama kwato na utumbo navyo utapata wanunuzo wake kwa bei ya kitalii
Watanzania tusha zoea biashara za kijamaa sana, Mfano ukiwaambia huku Arusha unakuta kilo ya nyama ng'ombe kuna sehemu kilo ni sh 35,000/ nazani mtaandamana.

Njoo Nanenane Arusha mwezi huu uone bei za hao nguruwe
 
Pole sana ndugu, itakua umekosea njia
Sa mtu anakutapalije kiaje an! Em acheni fikra mgando ishu ya nguruwe ni faida kuliko ata ufugaji wa kuku! may be! so jamaa kaongea kitu apo! Ila inatakiwa uwe na mzigo kuhudumia wale viumbe wanakula sana! mimi mkuu Imani rubaba siji wasap ila wazo lako ni zuri sanaa! hongera Kwa kunikumbusha hii kitu! ntaliwekea bajeti next ea
 
Watanzania tusha zoea biashara za kijamaa sana, Mfano ukiwaambia huku Arusha unakuta kilo ya nyama ng'ombe kuna sehemu kilo ni sh 35,000/ nazani mtaandamana.

Njoo Nanenane Arusha mwezi huu uone bei za hao nguruwe
Kama ni hivyo basi hata kuku mmoja wa kisasa anaweza akakuingizia hadi laki moja
 
Nilitegemea uelezee changamoto pia Ile umeweka faida tu, yaani nani akakuambia Kuna upande mmoja pekee wa shilingi
 
Mwenyewe tuu anaonekana mbona

Hizi bei mkuu kamba hiyo?
Nimeanza ufugaji miaka mitatu iliyopita kwa kuanza na jike moja. Leo nina majike matano na madume mawili. Ninazalisha vibwagala na kuviuza.

Kwa mfano, mwezi May pekee, niliuza vibwagala 39 kutoka kwa majike 4. Kila kibwagala niliuza kwa sh 70,000. Mwezi June nikauza jike mmoja kwa sh.600,000 tu ambaye ana umri mkubwa. Hii ina maana kwa huu muda nimeingiza 3,330,000. Hawa ni wa kienyeji.

Kwa sasa nimepandikiza majike matatu ambayo yatazaa ndani ya mwezi Septemba na watauzwa mwisho mwa mwezi Novemba. Nikibahatika vitoto 30 tu, huenda nikaingiza 2,100,000.

Changamoto zipo, lakini ni suala la kujipanga na kupambana nazo. Hakuna kizuri kinachokuja kiurahisi rahisi. Labda akina Abdul ndo wanapata pesa bila jasho.

Mapato ya vibwagala nimefanikiwa kununua ng'ombe wawili nitakaowafundisha kulima.

Kuna ushauri ukiamua kuufanyia kazi unaweza kubadilisha maisha yako. Ingawa ni lazima uwe na dhamira ya dhati na kuweka malengo yanayotekelezeka.

Tupambane, tusibeze kila kitu.
 
Mlitaka a present vipi? aseme nguruwe wa aina hio ukimfuga unakula hasara? mnataka negative story tu humu, Forum isha haribiwa na wapumbavu, kupingana kwa hoja hakupo sasa ni ujinga ujinga tu.
Usinipangie cha kupost nguruwe wewe
 
Nguruwe wanalipa lakini si kama ulivyoandika
Na hapo unaposema watu wajiunge kwenye group la Whatsapp hapo ndipo unataka uwatumie kwa faida yako.
 
Back
Top Bottom