Nguvu nilizowekeza kwenye ujana wangu nakula Matunda yake sasa

Mzee gani unaandika habari unaweka mambo ya mkoa X, hii ni code ya vijana wadogo. Wazee wana codes zao sio mambo ya X na Y.
Well, ila kaongea point. Uzee/ Ujana wake sio wa kuujali kivile.
 
Sawa Mzee was y and x
 
...shukuru sana kilichokusaidia kipindi hicho hakukuwa na mibususu kama za kipindi hiki, vijana wanahitaji maombi maalum maana maneno hawasikii tena sababu vita yao ya kutoboa na kufanya saving kwa miaka hii ni shida.!
 
Hiyo ni pointless maana anaandika vitu ambavyo hajapitia yeye. Asubiri mda wake utafika. Sio sasa
Unamaanisha kuwekeza ujanani kwa maandalizi ya uzee ni pointless sababu aliyezungumza sio mzee?
 
Unamaanisha kuwekeza ujanani kwa maandalizi ya uzee ni pointless sababu aliyezungumza sio mzee?
Simaabishi hivyo. Namaanisha huyu mtoa mada hajafikia huo uzee anaojinasibu nao hapa. Asubiri mda wake. Hii ndio pointless yenyewe.
 
Nashukuru sana. Mi pia nina imani nafuata nyayo zako.
 
Asante Kibabu ila hujafafanua uliwekezaje?,...
 
Ila haya maisha ni ungesr mtupu!

Yani unahangaika alafu ukija kufanikiwa na uzee huu hapa hata hela zenyewe huzifaidi
 
Huu uandishi ni kama wa jamaa mmoja hivi aliyepigwa banπŸ˜‰πŸ˜‰. Coz Yule jamaa mda wote alikuwa anajisifu tu.,..
 
Asante grandpa.
Mungu akupe umri mrefu ufaidi jasho lako.
Dream yangu nikustaafu nikifika 45yrs nikiwa na hazina ya vitega uchumi.

Kuhusu hawa wajukuu zako wengine sijui kama watakuelewa coz akili zao zote ziko kwa mambo yetu yaleee
 
Sawa mkuu umewekeza kwenye Nini hasa
 
Tunashukuru sana kwa nasaha zako mzee wetu....!

Uzee mwema huja kwa gharama kubwa wakati wa ujana...! Kuepuka uzinzi ili usichafue nafsi na roho, kuepuka starehe za kufuja pesa na kuchosha mwili

Uzee mwema huja kwa kuzingatia uwekezaji sio tu wa kiuchumi, bali pia kiroho,kiafya na kijamii....!

Ijali sana afya ya mwili wako, kwa kuhakikisha unakula chakula chenye manufaa, ufanyishe mazoezi mwili wako hakika katika uzee wako utakushukuru, epuka vilevi viharibio mwili maana afya ndo utajiri wa kwanza na usijinyime usingizi sababu ya starehe za usiku.

Ijali sana familia yako, zawadi pekee nzuri na itakayoacha kumbukumbu zisisofutika vichwani mwa wanao ni kumpenda na kumjali mama yao...! Wafundishe wanao yaliyo mema na maarifa yote uliyonayo yatakayowasaidia katika maisha yao, tenga muda wa kufurahi na kutaniana na wanao, wafanye marafiki hakika watakutunza uzeeni..

Kuna nguvu iliyo kuu kuliko zote, tafuta namna utakayoimini na kujiunganisha na nguvu hiyo, ili ikusaidia kufanikisha mambo yaliyo nje ya uwezo wa kibinadamu, kwa hakika binadamu ni roho, na mambo yote yanaanzia katika ulimwengu wa roho.

Kuwa mwenye utu kwa kujali hisia na maumivu ya wengine, usimfanyie mwenzio jambo usilopenda kufanyiwa. Pale utakapoweza kuweka tabasamu na furaha katika maisha ya wengine, hakika hayo ndio tunaita mafanikio...!

Kumbuka kile unachokula ndicho chako, pesa na vitu visikutoe utu wako kwa kuwa mbinafsi wa kutaka kujilimbikizia mali...!
 
Vitu gani unashauri mtu afanye akiwa kwenye 20's, mi npo mwanzon kbs mwa 20
 
Asante grandpa.
Mungu akupe umri mrefu ufaidi jasho lako.
Dream yangu nikustaafu nikifika 45yrs nikiwa na hazina ya vitega uchumi.

Kuhusu hawa wajukuu zako wengine sijui kama watakuelewa coz akili zao zote ziko kwa mambo yetu yaleee
Shukran mjukuu, maisha ni kuchagua tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…