Nguvu nilizowekeza kwenye ujana wangu nakula Matunda yake sasa

Angalia sana hizo nyumba na frem zikianza kuchakaa zitakula pesa nyingi kuzikarabati kiasi kwamba unaweza kufikiria kuzibomoa na kuzijenga upya. Wekeza kwenye fursa zingine pia.
 
Jamani wasomaji wa huu uzi zingatia ushauri badala ya kutafuta details za mwandishi. Hata kama ametunga story lakini mi naona content ni za kufanyia kazi. Wanaopinga hawana lengo la kutengeneza kesho yao. Mshahara mkubwa siyo kigezo bali kanuni za kutumia kipato kidogo ukawekeza na kuendesha maisha.
 
Ahsante Sana mkuu kwa kutuhamasisha.
Vijana tunatakiwa tupambanie maisha yetu kwa jasho, machozi na damu.
 
Shikamoo bro! Asante kwa kuwatahadharisha vijana! Mbona hata uzeeni watu wanatoboza tu! Fikria mzee aliyewekeza kwenye Kilimo cha ngano mwaka jana kapiga 600m huyo ni mwenzetu kweli? Kupambana haina mwisho mzee!
 
Uzi wako hauna tofauti na wa vijana wa digitally.
Ungeeleza nini ulisoma, ulivyowekeza, turn over na cgallenges ulizokutana nazo si ungekuwa umefunza vijana wengi.

Yaani umestaafu na upo the end unaongea kijuu juu kama unajibu mtihani wa drs la saba unamuogopa nani?
Ungekuwa bosi wangu ungenifukuza kazi maana ningekuchana tu kwa uwasilisgaji jana huo.
Ilikuwa unaandikaje project/report huko kazini?
Uzi wako unatakiwa uakisi uwezo wako na uzoefu wako kazini na ktk ujasiliamali.
Nadhanu hujaamua kutuasa vihana au nawe ni kijana uliejivika uzee, vinginevyo umesahau jinsi ya kuwasilisha maudhui.
Samahani kama sijakuelewa ila huja ni impress sana kama ule uzi wa "magofu ya Rapta" na "nimeamka jioni sana".
Hao wawasilishaji waliamua kutuelimisha,
nyuzi zao zimeandikwa kwa Lengo la kuelimisha kweli.
Simaanishi uandike nyuzu ndefu ila utupe content kamili kwani umeamua kuibana kwa makusudi.
 
ujana zama hizi vishawishi vimezidi hela haikai ukiikamata tu chawa hawa hapa, mara msg za mbet, pisi kali hao kama wakimbizi
 
Kweli kabisa ni vema kujipanga ukiwa na nguvu kuliko kufanya starehe zisizo na faida ukaja kusumbua watu uzeeni Vijana zungatieni ushauri huu
 
ujana zama hizi vishawishi vimezidi hela haikai ukiikamata tu chawa hawa hapa, mara msg za mbet, pisi kali hao kama wakimbizi
Kwani lazima kuwa na hizo pisi Kali chagua mmoja mnaeendana fanyeni maisha
Hao chawa ni matokeo ya kukosa kwako mipaka na nidhamu ya matumiz ya fedha
 
Wewe Mzee mwenzangu tumezaliea mwaka mmoja na tukasitaafu mwaka mmoja! Hongera sana. Hata mimi sijuti kwa kweli.
 
Mzee gani unaandika habari unaweka mambo ya mkoa X, hii ni code ya vijana wadogo. Wazee wana codes zao sio mambo ya X na Y.
 
Japo inawezekana wewe sio mzee ila umeongea jambo zuri sana. Nami naongezea
"MKUMBUKE MUUMBA WAKO SIKU ZA UJANA WAKO KABLA............"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ