GE2025 Nguvu wanayotumia CCM kukusanya watu kwenye mikutano ni kubwa mno na inawatesa

GE2025 Nguvu wanayotumia CCM kukusanya watu kwenye mikutano ni kubwa mno na inawatesa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
CCM ishakufa zaman, ni dola ndo inakiweka madarakani na sio wananchi.
 
CCM ishakufa zaman, ni dola ndo inakiweka madarakani na sio wananchi.
Ukweli ni kuwa hata hiyo "dola" siyo. Hao wanatumiwa tu na GENGE la Samia,
Dola wanafuata tu maelekezo wanayo pewa.
GT
Asikwambie mtu. Hakuna mda CCM wanateseka kama kipindi hiki unajua kumshawishi mtu ahudhurie mkutano ambao hana shida nao ni kazi ngumu sana.

Yaani kumpa.hela tu huyo mtu peke.yake haitoshi maana anaweza kula hela na akaingia chocho ha ha 😂 😄 Sasa inabidi uwakusanye watu kama mbuzi wasitoroke na uwaandalle usafiri kwenda na kurudi hatari sana.

Sasa hivi viongozi wa mtaa wanapita nyumba hadi nyumba kuan̈dikisha upya watu na namba zao za simu yaani ni tabu tupu. Wanatembea hao kama vichaaa 😆 🤣 😄 .

Na Samia akishapita sehemu hawezirudi maana kuwapata watu kama hao ni mtihani kiufupi akipita sehemu kamaliza kabisa kwa Nchimbi hatupewi coverage kubwa maana watu ni wachache sana
Haya yote uliyo eleza hapa ni mambo yanayojulikana toka muda kitambo.

Lakini umuhimu mkubwa sana wa mada yako unakuja iwapo pangekuwepo na nguvu pinzani ya huku kuwa kusanya watu kuwapeleka kwenye mikutano.

Hoja yangu ni kwamba, kwanza ni njia hizi hizi wanazozitegemea Samia na Genge kuwakusanya watu kwenda vituoni na kupiga kura. Kutakuwepo na kampeni kubwa sana na njia za kila namna hapo siku ya uchaguzi itakapo karibia kuhakiisha watu watakuwepo kwenye vituo.
Hapo sasa ndipo njia pinzani zingetumika kuwawezesha watu hawa wasiende kuuza utu wao na heshima ya nchi yao kwa kupiga kura.
Nyenzo kubwa na muhimu ingetegemea kuwaelimisha wananchi hawa madhara yatakayotokana na wao kuitikia kwa sababu zozote zile kwenda kupiga kura.

Hii ni fursa ya kipekee, ambayo wananchi wanaweza kuleta mabadiliko ndani ya nchi yao bila ya kuogopa kumwaga damu. Hakuna polisi atakayekwenda mitaani kwenye makazi ya watu hawa na kuwalazimisha kwa mitutu ya bunduki kwenda kupiga kura; tofauti kabisa na kutegemea kufanya maandamano barabarani.

elimu hii inge enezwa nchi nzima wiki moja kabla ya uchaguzi, kila mTanzania angetimiza wajibu wake huo muhimu.

Kama Samia na Genge watajitangazia ushindi bila ya waTanzania kwenda vituoni, hilo litakuwa ni jambo tofauti kabisa.

Kwa hiyo, mkuu 'Burning Spear', mada yako ni muhimu sana, iwapo itasaidia wachangiaji wa mada yako kubuni njia rahisi na nyepesi za kuwashawish waTanzania kukataa kulazimishwa kwa njia yoyote siku ya "uchafuzi" kwenda vituoni kupiga kura.
Hili ndilo tegemeo pekee sasa la kuiokoa nchi yetu na janga la kuleta mabadiliko bila ya umwagaji wa damu ya waTanzania.
 
kwan wamevunja sheria?
Wewe unaonaje; huoni wanakula njama; kuelekea kwenye kuvunja sheria?
Hujui kwa nini inawalazimu watumie nguvu nyingi kiasi hiki sasa hivi kujenga taswira ya kuvunja sheria?
 
Hivi Polepole anashindwa kumwaga siri nzitonzito zitakazomfanya waliyopo kwenye uhaguzi wapoteane?
 
GT
Asikwambie mtu. Hakuna mda CCM wanateseka kama kipindi hiki unajua kumshawishi mtu ahudhurie mkutano ambao hana shida nao ni kazi ngumu sana.

Yaani kumpa.hela tu huyo mtu peke.yake haitoshi maana anaweza kula hela na akaingia chocho ha ha 😂 😄 Sasa inabidi uwakusanye watu kama mbuzi wasitoroke na uwaandalle usafiri kwenda na kurudi hatari sana.

Sasa hivi viongozi wa mtaa wanapita nyumba hadi nyumba kuan̈dikisha upya watu na namba zao za simu yaani ni tabu tupu. Wanatembea hao kama vichaaa 😆 🤣 😄 .

Na Samia akishapita sehemu hawezirudi maana kuwapata watu kama hao ni mtihani kiufupi akipita sehemu kamaliza kabisa kwa Nchimbi hatupewi coverage kubwa maana watu ni wachache sana
Wewe umejuaje kama inawatesa?
Wewe unaumia nini ikiwa kweli wanateseka?

Chadema acheni kuhangaika we have our targets. Hawa ni viongozi kuanzia ngazi za mashina hadi mkoa. Huwezi watembeza kwa miguu kuanzia kijiji A hadi makao makuu ya wilaya mathalani.
Hawa viongozi wakija wanapewa maelekezo maalumu ya kufanya kampeni nyumba kwa nyumba kwenye balozi zao ili kuhakikisha chama kinashinda. Nyie endeleeni kulalamika but CCM when it 6 comes Kwenye uchaguzi hakunaga jambo dogo
 
Hivi Polepole anashindwa kumwaga siri nzitonzito zitakazomfanya waliyopo kwenye uhaguzi wapoteane?
mbona yeye kashamaliza kazi yake, unafikiri ni siri gani nyingine kubwa zaidi ya ile ya mifumo kuunganishwa, yaan mm na ww hapa tayari tushampigia kura samia.
 
Wewe umejuaje kama inawatesa?
Wewe unaumia nini ikiwa kweli wanateseka?

Chadema acheni kuhangaika we have our targets. Hawa ni viongozi kuanzia ngazi za mashina hadi mkoa. Huwezi watembeza kwa miguu kuanzia kijiji A hadi makao makuu ya wilaya mathalani.
Hawa viongozi wakija wanapewa maelekezo maalumu ya kufanya kampeni nyumba kwa nyumba kwenye balozi zao ili kuhakikisha chama kinashinda. Nyie endeleeni kulalamika but CCM when it 6 comes Kwenye uchaguzi hakunaga jambo dogo
Barca
Wewe ni mtu mzima, unajua CCM iko madarakani tangu uzaliwe. Unafikiri nguvu na pesa inayotumika kuja kutuambia "maiti hazitazuiliwa hospitalini" ni sawa?
Kwanza waliozuia maiti ni wao, Leo wanatumia mabilioni pale kawe, kusababisha foleni halafu wanakuja kutueleza habari za maiti, wakati huo huo kumuona daktari hapa Mloganzila ni sh 30,000. Kipimo cha CT scan ni zaidi ya laki tatu, si hizo pesa wangeipa Muhimbili waka subsidise baadhi ya huduma na dawa.
Au wewe unaona bora watu wafe kwasababu maiti hazitazuiwa ili hela zitumike kusomba watu? Remember hata wewe unaweza ukaumwa ukahitaji huduma ya Mloganzila Leo.
 
Ccm wapewe kesi ya usafirisha haramu wa binadamu hayo malori had tipa zinabeba watu kutoka vijijini
 
Nilicheka sina mbavu kijiji kimoja walitumiwa basi nikaona waliopanda ni wanafunzi na wajumbe wa nyumba kumi, wanakijiji wengine hawakuhangaika kwenda mjini mkutanoni. Kijiji cha pili niliona basi lipo vichakani likisubiri wanakijiji waingie na mwisho likaondoka na wajumbe wa mashina yao. Ni full vituko ccm inahangaika sana kujaza mikutano yao hasa ya mgombea wao wa urais. Wagombea ubunge na udiwani ndio wanapata msoto mkubwa mtaani, kampeni zao zinapuuzwa sawa na wale vikaragosi wanaogombea nao. Huu uchaguzi umekataliwa ndio maana kuna hali hii ya kutumia mbinu za ajabuajabu kujaza watu viwanjani kwenye kampeni zao
 
Kama hamna sheria wanayovunja acha wakusanye
Na siku ya uchaguzi, bila shaka CCM itawaandalia malori hao ng'ombe watu, na kuwalazimisha kusafirishwa mpaka vituo vya kupigia kura.
 
Nilicheka sina mbavu kijiji kimoja walitumiwa basi nikaona waliopanda ni wanafunzi na wajumbe wa nyumba kumi, wanakijiji wengine hawakuhangaika kwenda mjini mkutanoni. Kijiji cha pili niliona basi lipo vichakani likisubiri wanakijiji waingie na mwisho likaondoka na wajumbe wa mashina yao. Ni full vituko ccm inahangaika sana kujaza mikutano yao hasa ya mgombea wao wa urais. Wagombea ubunge na udiwani ndio wanapata msoto mkubwa mtaani, kampeni zao zinapuuzwa sawa na wale vikaragosi wanaogombea nao. Huu uchaguzi umekataliwa ndio maana kuna hali hii ya kutumia mbinu za ajabuajabu kujaza watu viwanjani kwenye kampeni zao
Hawa watu wamelaaniwa. Na hii hali itaendelea hata baada ya kujitangaza kuwa wameshinda uchaguzi itakuwa ni Serikali ya kuletewa na wahuni, ambayo haikutengenezwa na wananchi. Kushindwa kwake itakuwa ni furaha kwa wananchi. Ni Serikali itakayotengwa na mataifa mengi ya kidemomrasia. Itabakia kuwa karibu na zile Setikali za kidikteta ambazo kwa kawaida huwa hazina msaada wowote. Na kujishikamanisha na na setikali hizo zitazidisha kutengwa zaidi, hasa na mataifa ya Ulaya, America, na hata yale ya koafrika yenye ukaribu na Ulaya na America.
 
Nilicheka sina mbavu kijiji kimoja walitumiwa basi nikaona waliopanda ni wanafunzi na wajumbe wa nyumba kumi, wanakijiji wengine hawakuhangaika kwenda mjini mkutanoni. Kijiji cha pili niliona basi lipo vichakani likisubiri wanakijiji waingie na mwisho likaondoka na wajumbe wa mashina yao. Ni full vituko ccm inahangaika sana kujaza mikutano yao hasa ya mgombea wao wa urais. Wagombea ubunge na udiwani ndio wanapata msoto mkubwa mtaani, kampeni zao zinapuuzwa sawa na wale vikaragosi wanaogombea nao. Huu uchaguzi umekataliwa ndio maana kuna hali hii ya kutumia mbinu za ajabuajabu kujaza watu viwanjani kwenye kampeni zao
 
UMD nao wana vimaigizo, wanafanyia mikutano yao kwenye vijiwe vya bodaboda, bao, drafti na kahawa, mara unaona watu wawili watatu wanaibuka na bendera zao kukipa chama hicho vibe kionekane nacho kina watu wakati hata hakijulikani kwa wananchi. Kuna michezo inafanyika kuweka shamrashamra kwenye vyama shikizi navyo vionekane wananchi wanavipenda na wanahudhuria kampeni zao
 
Wewe unaonaje; huoni wanakula njama; kuelekea kwenye kuvunja sheria?
Hujui kwa nini inawalazimu watumie nguvu nyingi kiasi hiki sasa hivi kujenga taswira ya kuvunja sheria?
swali umelielewa ama umekurupa
 
Hakuna kitu kama hicho. Hebu angalia aina ya watu waliopo kwenye mikutano ya CCM, unaona ni watu wa aina gani wale?
Wale watu wana tofauti gani na wanaojaa Simba au Yanga Day? Hawana tofauti yoyote. Maana yake ni kwamba asilimia kubwa ya Watanzania wanachukulia siasa kama ushabiki wa mpira tu. Hawana wala hawahitaji sababu maalum ya kuwa chama fulani, na kwa sababu hiyo unaweza kuta asilimia kubwa ya mashabiki wa yanga ni CCM kwa sababu ndogo tu ya ufanano wa rangi.

Unachotakiwa kufanya ni kujaribu kuangalia watu au vitu nje ya mtazamo wako wewe, vaa viatu vyao na ufikirie kwa kutulia na umakini kwanini fulani anafanya anachokifanya, sababu watu hatufanani na wewe hauwezi kuwa yeye.

Hiyo inaitwa logical thinking au reasoning. Otherwise utaishia kutumia hisia binafsi na kuja na matokeo biased yanayoakisi unachotaka kukiamini.
 
swali umelielewa ama umekurupa
Ukweli ni kwamba akili yako imeathirika kwa hizi kazi za kuwafanyia maovu waTanzania mnazotumwa kuzitekeleza kuwanufaisha Samia na Genge lake.
Huwa sijibu kwa "kukurupuka".
 
Back
Top Bottom