Ninachelea kumnyooshea kidole Maalim Seif kama navyochelea kuwanyooshea Malema au Raila katika walio hai. Kwa maana nyingine hao wamefanya mengi kuliko labda yote tutakayoweza kuyafanya sisi katika maisha yetu yote.
Kwangu miye kina Mandela, Tutu, Mtikila na kina Nyerere wanaangukia kwenye daraja hilo.
Nipende kumwalika mjumbe kutoka zenji bar kwa mwongozo wake kumhusu Maalim na wasifu wake. Mjumbe huyu labda walikuwa naye katika harakati zao za mapambano.
Zawadini ikikupendekeza tafadhali, kwa maana ya nini kuandikia mate?