Uzima Tele nimekupata na hoja yako inayonitaka nilianzishe peke yangu wengine mfuate..
Hivi, kwanini mnisubiri nilianzishe peke yangu ili nanyi mnifuate? kwamba ndio tuseme bado mmelala mnasubiri mpaka nitakapolianzisha ndipo nanyi mtaamka?
Hebu tutazame mifano iliyoletwa na mleta mada au mingine ambayo tumekuwa tukiishuhudia mara kwa mara maeneo tofauti; anzia na Kenya, nenda hapo Senegal, tusogee kule North kwenye ile Arab Spring ya wakati ule...
hivi huko kote ni nani aliyelianzisha akawapeleka watu barabarani kuwatoa vyumbani kwao?
Hii mambo ya kusubiri fulani alianzishe kwangu naona ni usanii tu, tunategana, kwasababu naamini kabisa, deep inside, hata wakina nyie mnaosubiri wengine waamke nanyi pia mnajua vizuri mnatakiwa kulianzisha, tatizo sijui mnachosubiri ni kitu gani...
Ndio maana kule juu nikasema hili ni taifa teule la wanakondoo, wasio na tofauti na marehemu..