Nguvu ya Umma Senegal, funzo jingine kwetu

Nguvu ya Umma Senegal, funzo jingine kwetu

CHADEMA wasingempokea Lowasa Leo wangekuwa hivi

Mkuu siasa hazina rafiki wala adui wa kudumu bali agenda. Kwani aliporudi nyumbani hawakumpokea?

Jingine la msingi tumpumzishe na masimango mzee huyu ambaye sasa ni mgonjwa mno kitandani.

Nadhani anastahili sala zetu zaidi kuliko masimango.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Sijui tunahitaji mafunzo mangapi ya aina hii ili tuamke..

Inawezekana "tulishakufa" siku nyingi lakini sisi tunajiona bado tupo hai, kama tunashindwa kujifunza kwa majirani zetu hapo Kenya, hivi inawezekana kweli tukaenda kujifunza Senegal?

Naona hili letu ni taifa teule la wanakondoo.

Mkuu elimu haina mwisho. Ila pamoja na hayo uzi huu unahusika:

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Pasi na kumung'unya maneno tunakwama hapo.
 
Mimi Nina mchango kuliko kelele zako zisizo na msingi..

Nimekupa mfano hapo kwamba kumuandamania mwanasiasa ni upuuzi, Ufaransa watu Huwa wanaandamana Serikali ilipitisha au kutaka kupitisha Sheria za hovyo nk.

Nauona mchango wako kwenye post #21 kwenye Uzi huu:

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Ninasoma ukijibiwa:

"Waziri anasema hitaji la katiba mpya ni hitaji la watanzania.

Kwani mbinafsi wewe ni Mrundi?"

Sijayaona majibu yako mheshimiwa Mrundi tokea pande za pale Bujumbura.
 
Sijui tunahitaji mafunzo mangapi ya aina hii ili tuamke..

Inawezekana "tulishakufa" siku nyingi lakini sisi tunajiona bado tupo hai, kama tunashindwa kujifunza kwa majirani zetu hapo Kenya, hivi inawezekana kweli tukaenda kujifunza Senegal?

Naona hili letu ni taifa teule la wanakondoo.
Kwa hiyo hata denooJ hujaamka...??

Ina maana wewe denooJ ulishakufa siku nyingi..??

Na wewe denooJ hujajifunza toka kwa majirani..??

====Umeelewa maana ya maswali yangu haya..??====

Nina maana kuwa, movement yoyote huanza na mtu mmoja. Huyo mtu anaweza kuwa wewe..!!

Usifikiri kuwa Kuna mtu atafanya Kwa ajili yako. Lianzishe tu mwanangu wewe halafu wengine tutakufuata nyuma...!!
 
Movement zinazoanza na mtu mmoja ni exceptions. Movements kwa kawaida huwa na viongozi na huratibiwa vilivyo. Viongozi hapa huwa ni moto wa kuotea mbali.

Ya Kenya, Museveni, Afrika kusini nk ni mfano wake. Kuna nyuzi zimekuwapo humu:

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Aina hii ya watu wasingeita watu barabarani wakaacha kutokea. Anayekuita ukimwangalia usoni ulione hilo kwamba naye kadhamiria kweli kweli.

Huu hapa ulikuwa yet another uzi wenye kuonyesha kuchoka;

Magumu yetu Viongozi wa Upinzani mkwepe lawama vipi?

Ninadhani Hawa viongozi wetu wasipoangalia Pana hatari ya kufanyika mapinduzi ndani.

Kwa hakika ni effort kubwa inayofanyika kuacha utulivu uliopo kuendelea ikidhaniwa jaribio la mapinduzi linaweza kuwanufaisha CCM zaidi.

Imekuwa ikichelewa kutaja watu Kwa majina kuulinda Umoja huu ambao tumeupigania sote muda mrefu:

Uchaguzi 2024/25 wa nini kama hakuna Katiba Mpya?

Kwani viongozi kazi yao nini mkuu? Kama hawawezi Kwa sababu yoyote si wanawapisha wenye uthubutu?

Kufukuzana ki Mbatia Mbatia katu si ustaarabu.
 
Alisema baba wa taifa, "binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja."

Kwa hakika Afrika ni moja na waafrika ni baba mmoja mama mmoja.

Haikuwa tofauti kwa kinara wa upinzani Senegal Ousumane Sonko hadi nguvu ya umma ilipoamua kutoa hukumu yake ya haki:

View attachment 2566852

Ousumane Sonko sasa yuko huru baada ya vishindo vya wakoma kuwafurusha washami.

Hii ni kama kwetu tu:

"Katiba mpya ipo kwa wakati tunaoutaka Sisi na kwa namna tunayoitaka. Hii ni hata kama tukiamua iwe hivyo sasa."

Bila ya hivyo ngonjera zitakuwapo nyingi, mara kuhusu pesa, wakati magoli tunanunua na tunawasaidia hadi ulaya kwa pesa zetu wenyewe.

Akiziita JPM -- "pesa zetu za ndani!"
Nyomi nimeiona, hiyo haikuwa na mashaka kabisa.
Ila uli'assume' tu kwa uamzi wako mwenyewe kudhani kila mtu anajua kilichotokea huko.

Badala ya kueleza haya meeengi uliyoweka hapa, ungetumia muda huo, kutupatia nasi 'background' ya stori yako, nasi tungeungana nawe kuwasifu hawa wenzetu waliojitambua sana.

Huyo "Jamaa" wa Senegal, inaonekana na yeyey anataka kupitia kwenye njia zile zile za madikteta wengi hapa Afrika. Sall ni lazima adhibitiwe, na natumaini huu ndio mwanzo wa kufunga geledi nyani.
 
Kama ilivyoelezwa au alivyonukuliwa Kenyatta, kama wakenya wamelala basi sisi ni marehemu.

Nini kisichoeleweka hapa? Nyomi imemuweka huru aliyekuwa mikononi mwa dola. Iwe kuwa kuna ambaye hakujua anafanya nini hiyo itakuwa inahusika vipi tena.

"Obviously of importance was the end, and the means justified it!"

Tutakaa tunasimuliana hapa hadi lini ndugu zangu? Tulipo tunataka Katiba mpya sasa. Hadithi za Samia ni kutupa Katiba mpya baada ya 2025.

Ni mjinga peke yake atakuwa halioni hilo. Hata hivyo Mama anaweza kushawishiwa kuyaona mambo more logically:

Uchaguzi 2024/25 wa nini kama hakuna Katiba Mpya?

Nisiache kusema wazi wazi kuwa walamba asali, wahuni na wale vijana wa hovyo hawana mchango wowote kwenye jitihada kama hIzi.

Asiyeujua umuhimu wa Katiba mpya ambayo Dkt. Ndumbaro anasema wazi kuwa watanzania wanaitaka, ni wa nini huyo?

Asiyejua kuwa Katiba tunayoitaka hatutapewa bali ni ya kupiganiwa tena kwa maumivu sana, huyo naye wa nini?

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
 
Kama ilivyoelezwa au alivyonukuliwa Kenyatta, kama wakenya wamelala basi sisi ni marehemu.
I do not subscribe to such nonsensical talk! Has no logic whatsoever!
Aliyenukuliwa kuyasema maneno hayo, rekodi yake haina la maana sana la kumsikiliza yeye.
Nini kisichoeleweka hapa? Nyomi imemuweka huru aliyekuwa mikononi mwa dola. Iwe kuwa kuna ambaye hakujua anafanya nini hiyo itakuwa inahusika vipi tena.
Usikimbie ukweli. Una tendency ya kuuza maneno mengi saaana, kama inavyoonyesha hata kwenye andiko lako hapaa, lakini unakuta mengi ya hayo maneno ni mzunguko tu, hayazungumzii swala lilolengwa.

Nenda tena kwenye bandiko lako la mwanzo, ondoa huko kujihisi kuwa unasemwa na kujitetea. Utaona hukueleza tukio maana ya tukio hilo. Badala yake uazunguka kila mahali isipokuwa tukio husika.
 
Back
Top Bottom