Nilianza na swali la kwamba nani ataanza kuhamasisha? Kule watu walihamasishwa kwanza kuamini uongozi/viongozi wao kwamba kinachodaiwa ni kwa maslahi yao.
Walipohamasika wakajengwa kujiamini na hivyo kuthubutu kuingia barabarani kuandamana; wakaingia.
Kuna umuhimu wa kujenga hamasa na kujiamini kabla ya kutenda.
Watu pia wahamasishwe kupokea matokeo ya matendo yao hayo, watapokuwa tayari. Nadhani una kumbukumbu japo kidogo ya matokeo yenyewe. Kwenye hili ukipata nafasi wasikilize wale wajumbe walioteuliwa, sijui niseme, kufuatilia au kutafuta ukweli wa mambo? Hao watu wapo bado.
Z
Ninakusoma vyema ndugu mjumbe. Yapo mengi ya kujifunza katika bandiko lako fupi. Itakuwa muhimu kwa wataka haki hapa nchini kulidadavua vyema.
denooJ,
Sexless,
Econometrician ,
Erythrocyte makaveli10 na wapambanaji wengine mahiri, pana wito wenu mahsusi huku, badala ya kusubiria dodo kwenye minazi.
Kwa hakika hili ndilo linalokosekana. Niungane nawe kwenye kuyaona hivi:
1. Ni lazima ifahamike kuwa nguvu ya Umma ndiyo njia pekee ya kuaminika ya kupata suluhu kamili.
2. Njia hii pamoja na kuwa ndiyo bora zaidi ina gharama zake ambazo ni lazima tuwe tayari kuzilipa. Hizo ni pamoja na kudhulumiwa, kukamatwa, kufungwa, kuteswa, kujeruhiwa na hata kufa.
3. Kuwahamasisha watu ili kuwajengea kujiamini kwa ajili ya utekelezaji na ujasiri wa kuyakubali matokeo yoyote yatakayotokea, kunataka viongozi mahiri kweli kweli. Bila shaka wa aina ya kina Nyerere, Maalim Seif, Mandela, Malema, Tutu, Odinga, Sonko na wa namna hiyo.
4. Viongozi wetu ni muhimu wajkajihoji wenyewe kwa kuanzia, kuona kama kwenye kigezo #3 wanatosha.
Ieleweke kuwa viongozi wanaohitajika wanaonekana hivyo kwa matendo, maneno na hata kwa kuwaangalia usoni.
5. Badala ya kukaa kuwalaumu wananchi kuwa hawachukui hatua, tuwe tayari kupanga safu zetu za uongozi pasi na kuangaliana usoni.
Ni muhimu ikafahamika wavumao baharini papa, lakini na wengine wapo. Kwa maana kamili ya kufahamu kuwa hayupo ambaye ni indispensable.
Pamoja na kukushukuru niweke wazi kuwa nyuzi mbili hizi kutokea katika mchango wako naziona kuwa zingali zinaishi:
Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu
Magumu yetu Viongozi wa Upinzani mkwepe lawama vipi?
Mdogo mdogo, tunasonga. Mdogo mdogo tutafika.
Cc:
joka kuu,
Yoda,
Mag3,
Proved