Nguvu zitokanazo na kutokufanya mapenzi kwa muda mrefu(celibacy)

Nguvu zitokanazo na kutokufanya mapenzi kwa muda mrefu(celibacy)

Natumai mmeshinda salama salimini. Jioni hii ningependa kuwashirikisha mambo kadhaa kuhusu dhana ya celibacy

Celibacy ni neno lenye maana ya kutawala tamaa za ngono kwa muda mrefu aidha kwa kufuata utamaduni fulani au utaratibu wa mtu binafsi
Zifuatazo ni baadhi ya faida zitokanazo na Celibacy

1.Hutunza nguvu za asili(spiritual energy)

2.Spiritual energy ndo nguvu kubwa zaidi kushinda nguvu za kimwili

3.Huimarisha afya ya akili na utulivu

4.Hufungua milango ya mafanikio kwa maana Mungu huwasiliana na kilichotakaswa(Mtu msafi)

5.Huleta mvuto kwa watu,biashara,kazini,mapenzi n.k

6.Humfanya mtu asizeeke mapema(living young)

7.Huimarisha mfumo wa uzazi kwa mwanaume hasa akitunza shahawa kwa muda mrefu
N.B:Uzi huu hauwafungi wanandoa
Hayo matokeo yote yanapatikana baada ya muda gani? Kama ni kwa siku kadhaa kama 2 mbona sijawahi kuyaona?
 
Ukifatilia vizuri hizo ni pumbazo tu hakuna faida ya kufanya mapenzi wala ya kutofanya mapenzi

Ni ujinga ujinga ambao upo tu ili mradi kupumbazana tu akili

Tafuta kazi, anzisha biashara, ajiriwa, jiajiri.. pata pesa jenga himaya yako kuwa na pesa zako benk nyingi, jinengee heshima.. ukiamua ua hautak usioe

Zalisha wanawake hautak acha.. maisha tu ukifika mda kufa, uzikwe

Vitu vingi duniani ni porojo tu
Shangaa na wewe ndugu Hakimu
Maisha yenyewe ni ubatili mtupu
Wakati tukijitahidi kujizima data ili tuishi na kuinjoi maisha huku tunajua kabisa kuna siku tunakufa, wengine huku wako bize uijnga ujinga utadhani wanaishi milele
 
Huwezi kuwa double standard lazima uchague kimojawapo
Unaweza ukawa duniani alaf usiwe chochote ukazaliwa ukaishi maisha marefu hata ya miaka 100 mda ukafika ukafa ukazikwa

Katika maisha yako unaweza ukawa, haujawahi gombana na mtu, wala haujawahi kuzaa mtoto, na wewe ulikuwa mtu mzuri tu, hauna kesi yeyote serikalini wala uraiani na majirani zako, maisha yako hayajawahi kuwa ya majuto wala kulalamika chochote, wala haukuaga malaya, na haukuwa una upungufu wowote kizazi unacho na wala haujazaa

Na ulikuwa mwanaume/mwanamke kamili tu…

KUTAKA KUJITIA STRESS TU..
 
Back
Top Bottom