Nguzo za umeme za zege sasa ni hatari kwa maisha kuweni makini msikae karibu

Nguzo za umeme za zege sasa ni hatari kwa maisha kuweni makini msikae karibu

Mkataba wa utegenezaji na usambazaji wa hizi nguzo za zege ni kama ulivyo Mkataba wa @DP_World tu! Hizo nguzo za zege ni dili la Kipara & Maharage.!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kudondoka kwa nguzo za umeme za zege imekuwa kawaida kabisa. Mimi mwenyewe nimeshuhudia nguzo mbili Moja ikijeruhi mtu akiwa ndani ya gari.

Wahusika wawataarifu wananchi wasisogelee hizi nguzo. Ni hatari hazina vyuma ndani yake. ikipata unyevunyevu tu inaanguka.

Mimi nilishangaa engineers waliyozitengeneza hizi nguzo hazina expansion joints. Sasa sijui technology iliyotumika hapo ni ipi. Mimi ninavyojua hizi hazidumu kabisa.

Kuna nguzo za umeme za zege zilijengwa kwenye Reli ya kati. Zile nguzo kwakuwa hazina expansion joints zilibubujika zikabakia vyuma.

Hawa sijui wanatumia science gani. Ukipita kwenye madaraja yote, barabara ya mwendokasi na sehemu nyinginezo. Huwezi kuweka zege kwenye jua bila expansion joints. Hayanihusu.

Video hii hapa nguzo imeanguka


Tafuta mtaalamu au mwenye tenda au wizara ielezee gharama ya nguzo hiyo na ndipo tutapata majibu ya chanzo.

Ninachofahamu nguzo hiyo inagharimu kiasi cha laki NNE pingeni hesabu muje na majibu.
 
Sikiliza kwa makini yaani jua kali likipiga zege linatanuka likipigwa Baridi ninasinyaa Sasa ukiwa na zege lefu au Pana. Juu panakuwa pabaridi chini panakuwa pamoto. Lazima lipasuke tu. Angalia zile njia za kuvukia Magufuli hostel zilipasuka
Hizo nguzo zina uwazi katikati ni kama pipe/bomba la mafuta
 
Nguzo hizi za zege zilizoanza kutengenezwa kuanzia march 20/2021 hadi sasa 2023 zimechakachuliwa sana.hata kwa kuziangalia tu kwa macho zina nyufa kabisa
 
Nyie si mnataka kila kitu wafanye wazalendo? Vumilieni sasa. Nguzo zinatengenezwa na wazalendo ambao upigaji ndiyo asili yao lazima zianguke. Unaweza kukuta bajeti ya nondo ilikuwepo lakini watu wamepiga.
 
Nadhani kuna makosa tu ya kibinadamu
Wewe ni mpumbavu kabisa. Makosa ya kibinadamu au ni uzembe uliopitiliza? Huu ni uuaji na wahusika ndiyo walitakiwa kushitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi. Hii tenda ya kutengeneza ngozo wamepeana wenyewe baada ya kuanzisha viwanda uchwara ili wapige fedha. Kutengeneza kwenyewe hawajui. Ujinga kama huu ndiyo kesho wanakuja na kusema tuchukuwe waarabu kwa sababu tumefeli kumbe ni ushenzi kama huu umefumbiwa macho. Nchi hii imefikia kwenye level ya juu ya ushenzi na viongozi hawajali tena maisha.
 
Inatafutwa sababu ya kuanza kununua nguzo kutoka Nje ya nchi nadhani!!! Mleta mada Nisamehe kwa mawazo yangu haya maana sina uhakika lakini fikra zanituma kuwaza hivyo!
Kuna muwekezaji wa ndani, mjumbe wa NEC wa Ccm aliyeongoza kwa kupigiwa kura nyingi Dodoma, anatokea Mufindi, yeye ni Swahiba wa January Makamba, ameahidi kutowa nguzo za miti bure kwenye project ya Rea mkoa Fulani.

Sasa hapa kuna Uturn inaandaliwa kurudi kwenye woods material.
 
Kuna muwekezaji wa ndani, mjumbe wa NEC wa Ccm aliyeongoza kwa kupigiwa kura nyingi Dodoma, anatokea Mufindi, yeye ni Swahiba wa January Makamba, ameahidi kutowa nguzo za mati bure kwenye project ya Rea mkoa Fulani.

Sasa hapa kuna Uturn inaandaliwa kurudi kwenye woods material.
duuh urasimuu kila konaaaa...!! nchi za afrika kuendelea ni ngumuu sanaa aiseee
 
Wabongo washaanza kuchakachua huko....

Ova
mrangi ndugu yangu hii nchi imeshafikia level mbaya sana ya uzembe. Hizi nguzo zimetengenezwa kwenye viwanda vilivyoanzishwa chap chap na hao hao watu wa Tanesco ili kupiga fedha. Wahusika wa huu uzembe wanatakiwa kushtakiwa na kuhukumiwa hata kifo kwa uzembe huu. Hawa sasa ndiyo wahujumu uchumi na siyo watu wema wanaobambikiwa.
 
style ya nguzo inafikirisha ..... hata mie nilijua ndani inasukwa kwa nondo kuongeza uimara

watakuja wachambuzi wa gharama za nguzo za zege vs miti
zege ni shingi XXX
miti ni shilingi XX
Zege zina faida X
  • Tuliambiwa zinaweza kudumu mpaka miaka 100.
  • Ikiwa kama tu nguzo zinatoa jasho, kujadili mikataba mizito kama ya DP inawezekana?
  • Huo udhaifu inaweza kutumika kuliuza shirika.
 
  • Tuliambiwa zinaweza kudumu mpaka miaka 100.
  • Ikiwa kama tu nguzo zinatoa jasho, kujadili mikataba mizito kama ya DP inawezekana?
  • Huo udhaifu inaweza kutumika kuliuza shirika.
Pita reli ya Tazara, hiyo reli imejengwa kuanzia mwaka 1968 na hizo nguzo mpaka leo zipo imara.

Kwahiyo ni kweli kama ukifuata quality life span yake ni miaka 100.

Mradi wa barabara za DMDP unaona una quality kwa sababu world bank wanasimamia na wanakaguwa wenyewe wana wataalam na maengineer wote, na kampuni zinazopewa kandarasi ni kampuni zenye uwezo hakuna magumashi.
 
si kweli! Nakupa homework tafuta tofauti ya hivyo viwili then utajua weigt ya pole 9m haizidi 400 kg!

Weight and load mean the same thing. Sijui mantiki yako hasa ni nini, magogo yanaweza kutofautiana ila hizo nguzo zinatengenezwa kwa uzito unaowiana.
Load refers to the amount of weight being carried or transported, while weight is the force exerted by an object due to gravity.


 
Load refers to the amount of weight being carried or transported, while weight is the force exerted by an object due to gravity.


If you read carefully, you end up with the same thing.
 
Nadhani kuna makosa tu ya kibinadamu
Makosa ya kibinadamu yapi tena?

Nimewahi kuangalia video ya namna hizi nguzo zinavyotengenezwa, kuna nondo ndani yake, ina maana hapa walisahau?

1689858820227.png
 
Back
Top Bottom