Nimekaa maeneo uliyoyasema, jamii hizi si masikini kama unavyosema. Ni wakulima wazuri, wafugaji na wafanya biashara. Kuna wasukuma wanafedha na wengine wanamigodi mikubwa tu ya dhahabu na almasi. Ila huwezi kuta msukuma anajisifia, au kujionesha kwamba ni tajiri. Hawa upenda maisha ya kawaida, japo wana hela.
Unakuta mtu ana ng'ombe wengi, ardhi kubwa ya kulima, wanakula vizuri, ndo maana miili ya kisukuma ni mikubwa, hivi wangekuwa masikini hiyo afya wangetoa wapi? Wengine ni tajiri wa biashara za samaki. Huo umasikini unao usema ni upi?
Mie nachoona kwa wasukuma uwa hawaachi mila zao za kuwa na nyumba za nyasi. Hata ukikuta kajenga nyumba ya bati nyasi lazima iwepo na hasa vijijini. katika nyumba hizo za nyasi ndiko wanakofanyia matambiko yao.
Mwanza, Kahama, Geita, Bariadi, Shinyanga, wasukuma wana fedha, lakini uwezi kuta hata siku moja mtu kaitwa Billionea, au kufahamika ana hela. Wasukuma ni wanyenyekevu, mpaka umchokoze ndo utajua ukorofi wao.