Alisema anatoa 70 per day so he is capable na kingine ukute hamisa anajua south zinapelekwa kias gani ndo maana
Mpwa bhana... eti pengine anajua South zinaenda kiasi gani!!!
Mpwa, hivi viwango sio kwamba vinatolewa tu! Mosi, ni kweli kigezo cha kwanza kinatokana na uwezo wa yule anayetakiwa kutoa hayo matunzo! Na kwa kutumia kigezo hicho, kiwango atakachotakiwakutoa Diamond ni tofauti na kiwango atakachotakiwa kutoa mtu wa kawaida!!!
Hapa inaweza kuonekana kwamba, kwavile ni mtoto wa Diamond, basi 500K ndicho kiwango sahihi.
Pili, lifestyle ya wazazi! Hapa ndipo watu wanaposhindwa kuelewa!!! Kinachoangaliwa hapa sio kwa watu waliokutana barabarani bali watu waliokuwa wanaishi pamoja. Kwa mfano, leo K-Lyn akitarakiana na Mzee Mengi, kitakachoangaliwa ni lifestyle ya K Lyne na Mzee Mengi ambayo assumption itakuwa kwamba, mtoto nae atatakiwa ku-enjoy the same lifestyle ya kwenda vacation Paris, J'burg n.k kwa sababu, endapo
wasingetengana, mtoto angekuwa anaendelea kukwea pipa kwenda Seychelles kula upepo wa bahari!
Lakini haiwezekani wewe mama hujawahi kuishi (hata kama sio kwa ndoa but in commitment way) na mwanaume husika halafu u-demand lifestyle ambayo sio ya kwako kwa sababu tu umezaa na huyo mwanaume!
Which means, leo hii Zari na Hamisa wakienda kwenye same mahakama na kesi kusikilizwa na wale wale kwa Hamisa na Zari, bado Zari atapewa pesa nyingi kwa mtoto mmoja kuliko Hamisa kwa sababu, lifestyle ya Zari na Hamisa ni tofauti! Hizi lifestyle ndizo zitakazo-determine kigezo #2 cha kutoa matunzo baada ya kuangalia uwezo wa baba!!
Aidha, Zari ameishi na Mond in commitment way kwahiyo watoto wanatakiwa ku-enjoy the same lifestyle ambayo wange-enjoy kwenye nyumba ya wazazi wao endapo ingekuwa
hawajatengana. Msisitizo, hawajatengana!!!