Ni aibu kuwa na taifa ambalo Rais wake anaingilia Mhimili wa Mahakama na anajinasibu kufutia wakosaji makosa kinyume na katiba

Sabaya ataachiliwa karibia na uchaguzi ili kupata kuungwa mkono na Sukuma Gang.

Mambo aliyoyafanya Sabaya yana tofauti gani na aliyoyafanya Bashite?

Katiba mpya itaheshimisha nchi
 
Sidhani kama tatizo la nchi hii ni katiba.
Nijuavyo Rais Hana mamlaka ya kumfutia yeyote kesi kama anayo kwamujibu wa katiba hii tupate kifungu kinachomruhusu.

Labda kupitia DPP, Rais angesema DPP amesema Hana Nia ya kuendelea na kesi labda ingekua sawa lakini si kumfutia mtuhumiwa kesi ni mahakama ndio inafuta kesi. Kumsamehe aliehukumiwa na mahakama hilo linawezekana na Rais.

Rais anayomamlaka ya kumsamehe mfungwa akiwa ameshahukumiwa na mahakama. Mahakama inakua ilishamaliza kazi yake.

Tatizo letu sio katiba Bali hatuwezi kuisimamia katiba hata iliyopo sijui hiyo mpya watakuja malaika kuisimamia.


Hata jaji mkuu aulizwe nikweli rais anaweza kufuta kesi? Atakataa kwamba Hana mamlaka hayo.

Washauri hawakumshauri vizuri mama yetu katika Hili na wala tusishupaze shingo hii haikua sawa kutamkwa hadharani hata kama limetendeka kwa maelekezo ya raisi angeachiwa DPP amalize kazi hiyo na watu waambiwe DPP Hana Nia ya kuendelea na kesi basi.

Leo hii watuhumiwa wengi watakua wanamuomba raisi awasaidie kufuta kesi zao na wataona kufungwa kwao sio mahakama ni rais ameamua wafungwe.
 
Katiba hii inayofutia wapinzani kesi ni nzuri sana hakuna haja ya kuibadili.
 
unaropoka tu unaulizwa vifungu unabaki mwaga uharo

unasema vifungu husema hivi unaombwa kuviweka hapa unaanza kuhara tu

weka kifungu hapa tukuone ujuvi wako tofauti na hapo umeme wa kichwani kwako ni mdg sana
Kavitafute utaviona....acha uzembe wa kutafuniwa....zuzu wewe
 
Ama kweli wapinzani wa nchi hii ni vigeu geu. Kumbe kuvunja katiba sio tatizo kama inawapendelea wao. Upinzani hawana kanuni(principles) zinazowaongoza.
 
Kawaulize waliojiweka karibu na Samia maana mimi sio msemaji wao.
Mimi nataka kujua mtazamo wako wewe sio mtazamo wao kwa wanachofanya, wewe unapoona viongozi wa chadema wanajiweka karibu mno na Rais Samia unalichukuliaje hili suala?
 
Ibara ya 107B ya katiba ya JMT imetamka wazi kuwa mahakama zitakuwa huru kuendesha mashauri.

Inashangaza Rais Samia kumfutia mharifu makosa

Hii ni kinyume na katiba.
👇



Hakuna muhimili ulioingiliwa.
Mwendesha Mashataka (DPP)ambae bosi wake ni amirijeshi mkuu, ana mamlaka kisheria chini ya kifungu cha 91 (1) cha sheria ya makosa ya jinai (CPA), kuondoa mashitaka dhidi ya mtuhumiwa yeyote lakini vipo vigezo vya kawaida vya utoaji wa 'Nolle' lakini kigezo kikubwa kinachotumika sana ni kama DPP anaona hakuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani mtuhumiwa. Kisheria makosa ya jinai yanapaswa kuwa na ushahidi wa kutosha na usio na shaka hata chembe ili kumtia hatiani mtuhumiwa.
 
Una ijua AK47 wewe kweli
 
Ibara ya 107B ya katiba ya JMT imetamka wazi kuwa mahakama zitakuwa huru kuendesha mashauri.

Inashangaza Rais Samia kumfutia mharifu makosa

Hii ni kinyume na katiba.
👇



Hujui usemalo. Mahakama haiingiliwi bali ndivyo mfumo ulivyo. Anayepeleka Shitaka la Jinai Mahakama I ni DPP, na anaweza kuliondoa Mahakama I wakati wowote. Sheria inasema anapotaka kuliondoa halazimiki kutoa maelezo yoyote.
Hoja inatakiwa iwe kwamba, DPP anapofungua Shitaka la Uongo, achukuliwe hatua gani.
Na anayefunguliwa Kesi ya Uongo, alipwe fidia kiasi gani?
Hapo ndipo inatakiwa Katiba Mpya.
 
Wewe umesoma kweli? Dpp anatakiwa awe huru. Katiba ipo wazi. Hapa raisa anatamka hadharani kufuta kesi baada ya kuombwa na mtu. Kesi inapofunguliwa mahakamani inatakiwa iishe on merit.
 
Kwamba mhimili mwingine unaingilia mwingine?
Ulikuwa wapi wakati, tunaambiwa upo muhimili uliojichimbia zaidi hii ilikuwa wakati CAG anakamatishwa adabu.

Lakini katika nyakati fulani "supika" aliwahi kupewa maelekezo kuwa huko ndani washughulikie wakija huku nje na mimi nitawashughulikia.....sasa ni kipi mnashangaa bhangoshaaa.
 
Kama mwanachama ni shetani....

Mwenyemeza atakuwa nani??

Kama Rais kaamua kusamehe na kufuta kesi kwanini asifute ya Sabaya??

Mwanachama wake ??

Kesi tofauti kabisa watu tofauti
 
Sabaya ataachiliwa karibia na uchaguzi ili kupata kuungwa mkono na Sukuma Gang.

Mambo aliyoyafanya Sabaya yana tofauti gani na aliyoyafanya Bashite?

Katiba mpya itaheshimisha nchi
Sabaya anaonewa.

Kama walitaka kuondoa tabia za aina hiyo.

Wangemshitaki na makonda pia.

Mbuzi wa kafara.
 
Sabaya anaonewa.

Kama walitaka kuondoa tabia za aina hiyo.

Wangemshitaki na makonda pia.

Mbuzi wa kafara.
Sabaya hajaonewa bali ni karata ya kisiasa.

Wahalifu huangaliwa sura zao kwanza kabla hawwjashughulikiwa. Ukiwa na chongo ndo umejiharibia kabisaa
 
Mimi nataka kujua mtazamo wako wewe sio mtazamo wao kwa wanachofanya, wewe unapoona viongozi wa chadema wanajiweka karibu mno na Rais Samia unalichukuliaje hili suala?
Ww ulitakaje labda?
 
Soma upya katiba ya Tanzania ndiyo utajua nguvu aliyonayo Rais wa Tanzania.
 
Kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu kumfutia kesi Godbless Lema imewaibua wanasheria wanaosema inashusha hadhi ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), wakitaka mfumo wa haki jinai ufumuliwe ili kuilinda.

Maoni ya wanasheria hao yanazingatia Ibara ya 59B hususan kifungu cha nne kinachosema: “Katika kutekeleza mamlaka yake, Mkurugenzi wa Mashtaka atakuwa huru, hataingiliwa na mtu yeyote au na mamlaka yoyote na atazingatia, nia ya kutenda haki, kuzuia matumizi mabaya ya taratibu za utoaji haki, na maslahi ya umma.”

Akiwasalimia wakazi wa Usa River mkoani Arusha juzi, Rais Samia alisema Lema alipotaka kurudi nchini alimuuliza kuhusu kesi zake na akamwambia atazifuta.

“Kwa hiyo mdogo wangu amerudi, aliniambia mama nataka kurudi nikamwambia rudi, akasema mama nina kesi nikamwambia nazifuta, rudi. Amerudi tuimarishe siasa, si ndio?” alihoji Rais.

Lema aliyerudi nchini Machi mosi tangu alipokimbia Novemba 2020 kuelekea Canada, amekuwa akimshukuru Rais Samia kwa kubadilisha hali ya siasa nchini.

Akizungumza juzi wilayani Karatu mkoani Arusha, Lema alisema “nataka nitumie fursa hii kumshukuru, lakini afikirie jambo moja, mimi ni kiongozi wa kisiasa, viongozi wangu ama mimi mwenyewe nimepata fursa ya kupigania haki yangu lakini wapo masikini wengi magerezani ambao wamebambikiwa kesi, hawawezi kuwa na access ya kukufikia wewe, wala wazazi wao, hawa wanahitaji Katiba mpya na sheria bora.”

Katiba inavunjwa
Akiizungumzia kauli ya Rais Samia, Wakili Jebra Kambole alisema Ibara ya 59B(4) ya Katiba inaunda ofisi ya DPP na kutaka iwe huru, isiingiliwe na mtu wala mamlaka yoyote.

“DPP anafanya kazi kwa niaba ya Watanzania sio Serikali wala Rais na walalamikaji ni wananchi si Serikali. Ndiyo maana DPP anatakiwa kuwa huru, anashtaki, anaendesha mashitaka, anafuta kwa niaba ya wananchi, siyo kwa niaba yake, Rais wala Serikali,” alisema Kambole.

Kwa nafasi yake, alisema Rais anaweza kumteua DPP au kumwondoa wakati wowote hata kutumia madaraka yake kutoa maagizo kwa ofisi ya DPP.

Chanzo cha udhaifu huo alisema ni Katiba japo inatoa ulinzi kwa DPP na ofisi yake kuachwa huru. “Kwa sababu hii Katiba imempa Rais mamlaka ya kumteua na kumwondoa DPP, lakini Katiba hiyohiyo inamlinda DPP asiingiliwe na mtu yeyote. Kwa hiyo tuna tatizo la Katiba na la kiutendaji. Rais asingetoka hadharani na kusema amemfutia Lema kesi, hiyo haikuwa sawa,” alisema.

Akifafanua zaidi kuhusu madaraka ya DPP, Kambole alisema masilahi ya kesi ni ya wananchi na yamekaimishwa kwa DPP.

“Ukisema mwanao amebakwa na unataka DPP afute kesi, haiwezi kufutwa kwa sababu ukibaka unaiathiri jamii sio mtu mmoja. Au mtu akifanya mauaji, mtu akasema hata kama ameua sisi hatuna shida naye, haiwezekani kwa sababu madhara yanakwenda kwa jamii,” alisema Kambole.

Kuhusu uhuru wa DPP, alisema utalindwa vizuri endapo nafasi hiyo itaombwa kwa ushindani.

“Kwa mfano Kenya, DPP anakaa miaka minane. Kwa kipindi chote hicho hawezi kuondolewa labda afanye makosa ya jinai na baada ya miaka minane, hatakiwi kupata kazi Serikalini,” alisema Kambole.

Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk Rugelemeza Nshala naye alisema Katiba iko wazi.

“Inawezekana ni kuteleza tu au kujipatia sifa kidogo na kuchangamsha watu. Kisheria anayefuta kesi ni DPP, Rais anaweza kuzungumza kisiasa au inaweza kuchukuliwa kuwa ameteleza ndiyo maana kwa sasa tunazungumzia mfumo wa haki jinai ufumuliwe.

Wote umeoza kwa hiyo huwezi ukatibu uozo kwa kupachikapachika tu, unachotakiwa pengine ni kufukua wote unakwenda unazika,” alisema.

Juhudi za kumpata DPP, Slyvester Mwakitalu hazikufanikiwa baada ya simu yake kuita bila kupokelewa huku wasaidizi wake wakisema yupo kwenye kikao cha kikazi.

Akizungumza katika jukwaa la Club House jana asubuhi, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alisema kauli ya Rais haikumaanisha kwamba taratibu hazikufuatwa.

“Si kesi za Lema pekee, huwa mnaona mahakama mara nyingi ama inatupilia mbali kesi au anakwenda DPP anaifuta kesi.

Rais akisema nimemfutia Lema kesi haina maana kwamba alitoka mahali akaenda akafuta hiyo kesi, hapana, ile ni lugha ya mazungumzo.

Pengine tulizitazama kesi zake tukauliza, ninyi mnao ushahidi wa jambo hili? Hapana, ondoeni hiyo kesi, sasa ile ondoeni hiyo kesi haina maana kwamba wanaamka asubuhi wanaiondoa. Lazima ule utaratibu iufuatwe,” alisema Dk Tulia.

Kesi za Lema
Lema alikuwa anakabiliwa na kesi namba 63/2020 iliyokuwa na mashtaka 15 likiwamo la kusababisha taharuki kwa jamii baada ya kusambaza taarifa zinazodaiwa kuwa za upotoshaji kuhusu mauaji ya watu 14 wilayani Manyoni mkoani Singida.

Alidaiwa kutenda makosa hayo Februari 29 mwaka 2020 wilayani Manyoni kwenye mazishi ya kiongozi wa Chadema.

Aprili 27 mwaka 2018 Mahakama ya Wilaya ya Arusha ilimwachia huru Lema aliyekuwa akituhumiwa kwa uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli baada ya Jamhuri kushindwa kupeleka ushahidi.

Hata hivyo, baada ya kuachiwa, alikamatwa tena na kusomewa mashitaka ya kutoa lugha zenye kujenga hisia mbaya ambayo aliyakana.

Credit: Mwanachi newspaper
 
Upuuzi tu kipindi watu wanabambikiwa kesi wangeandika pia!! Haya magazeti ya kufungia tu maandazi hamna chochote!!

Kama kuna anasomaga hivi vikaratasi bado inabidi ajitafakari sana IQ yake maana waandishi wake kichwani hamna kitu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…