Ni aibu kwa vyuo vikuu hapa nchini kushindwa kugundua chanjo ya Corona na sasa vinashindana kutoa tahadhari

Hapana sio kwamba wanaonewa. Huo ndio ukweli wenyewe kwamba ma-professor na ma-doctor(PhD) wetu wamekosa committment kabisa.

Hawajakuwa serious at all. Kama hawajakuwa committed kwenye masuala ya tafiti zinazoweza kuleta positive impact mwenye jamii taasisi gani itawapati fedha kwaajili ya kuendesha hizo tafiti??....ma-professor na ma-doctor wetu hawana focus wameamua kujali matumbo yao na familia zao which has nothing to do with maendeleo ya taifa.

As said earlier, Mwl. Nyerere ali-invest sana kwenye the then the village for science and technology lakini ma-professor wetu wakaamua kupenda zaidi siasa na kuitelekeza ile taasisi ambayo ingeweza kuwa ni engine kwa maendeleo ya Taifa letu.

Sasa hivi ma-professor na ma-doctors wetu wameacha ku-dwell na fafiti na ufundishaji wamekaa wakisubilia teuzi za kisiasa serikali.......shame on them!!!!!😓😓😓😓
 
Researcher hawezi kurupuka na kufanya research bila kupata Sponsor au Funding Agent.
Kwann Oxford, Harvard, etal wapate vya Tanzania hata kimoja visipate? Ni kwasabb hamuaminiki, havijitumi, havina wabobezi na vipo vipo tu.
 
Kama hawajakuwa committed kwenye masuala ya tafiti zinazoweza kuleta positive impact mwenye jamii taasisi gani itawapati fedha kwaajili ya kuendesha hizo tafiti??...
Swali zuri sana hili mkuu
 
Kwann Oxford, Harvard, etal wapate vya Tanzania hata kimoja visipate? Ni kwasabb hamuaminiki, havijitumi, havina wabobezi na vipo vipo tu.
Nope,
Its funding!
Hivyo vyuo vya Oxford, Havard na vingine vinapewa funds za kufa mtu!
 
Mkuu inaonekana wewe ni kichwa maji kabisa. Unaongea mipasho isiyo na mantiki
 


Acha kutukana vyuo vikuu vya Tanzania, jiulize swali simple tu Kwa Afrika nzima umesikia chuo kikuu kipi kimetoa chanjo ya Covid? Achilia mbali vyuo vyetu vya Tz ambavyo hata top 20 ya vyuo bora Afrika havipo, nchi za South Africa na Egypt zenye vyuo vikuu bora Afrika wametoa lini hiyo chanjo ya Covid mpaka uwatukane wahadhiri wa Tanzania?

Unafikiri miundombinu ya maabara ya kufanyia Tafiti za Magonjwa hatari ya mlipuko yanayosababishwa na virusi gharama yake ni kiasi gani? Nchi yako inaweza kuimudu au unataka itembeza bakuli kuomba hisani kwa mabeberu? Nchi yako imetenga kiasi gani kwaajili ya kuwezesha tafiti vyuo vikuu? Au unafikiri kupata chanjo hao ma-Dr na Ma-Prof wanazipata kwa njia ya midahalo?

Umekurupuka mkuu mimi nadhani hata ungewashukuru kwa kuibuka na dawa zinazotibu baadhi ya symptoms za Covid kutoka NIMR,UDSM na TIRDO
 
Vyuo vikuu vipi unabizungumzia? Kule tunakaririshana tu notice, quiz za kuviziana na assignment za kukomoana.
 


Mkuu, kuna njia kuu mbili za kupata elimu, njia ya kwanza ni kupitia "acquisition" na ya pili ni kupitia "learning".

Mfano wa "acquisition" ni kama vile mtoto anavyojua kuongea lugha yoyote, yeye hujua hiyo lugha kwa ubongo wake kunukuu maneno yote anayoyasikia kutoka kwa wazazi na jamii inayomzunguka, ubongo wake hauna uwezo wa kuhoji neno lolote analolisikia isipokuwa ubongo wake hubeba tu kila neno na matumizi yake.

Mfano wa njia ya "learning" ni mtu yeyote anapojifunza lugha mpya, akili yake inatafakari kila neno na matumizi yake na sababu gani neno fulani litumike mahali fulani, kifupi ni kwamba kujifunza kwa aina hii kunazingatia hoja.

Maprofesa wetu na waalimu wetu wengi wamejifunza/wamepata elimu zao kupitia njia ya "acquisition", kifupi njia hii inalemaza akili kushindwa kuchanganua na kuhoji mambo mtu aliyojifunza, ni katika kuhoji na kuchanganua ndipo uwezo wa akili kufikiri zaidi ya kile ulichojifunza huanza, Maprofesa na Waalimu wetu hawezi kufikiri beyond what they have acquired.

Ili kuepuka huo msiba wa acquisition ni muhimu wapatikane waalimu watakao fundisha wanafunzi kupitia njia ya learning na sio acquisition na hatimaye wapatikane Waalimu na Maprof, watakaoweza kufanya mambo makubwa si kwa Tz au Africa pekee bali kwa dunia yote.

Acquisition perse is worse than Covid-19 & 20.
 
Kuna mtoto wangu alikuwa anashindwa kusema neno ''kilaza'' anasema ''kilatha''.
Kuna reserch nyingi zilizo kwenye uwezo wetu ni utashi tu. Kutengeneza chanjo hatuwezi na wala hatuna wataalam na uwezo. Hizi chanjo zinazotumika sasa hivi kuna serikali zimemwaga fedha nyingi kufadhili. Lakini bado kuna research nyingi tungeweza kufanya kuhusu huu ugonjwa. Una habari kwa mfano tangu hawa virus wa covid wapambe moto Kenya wanafanya research nyingi tu kuhusu hawa virus? Kwa nini kusiwe na research kwa mfano kuangalia kwa Tanzania ni watu wa aina gani wanaathirika zaidi au pengine kufa wengi? Kwa nini tusiangalie ni mikoa gani imeathirika zaidi na ni kwa nini? Je virus wana-mutate? Haya yote wala hayahitaji uchumi mkubwa ni suala la kuwa na viongozi wenye maono tu na utashi wa kutenga fedha za utafiti. Ila siyo ''kilatha'' kama bwana yule!
 
Kwani umesikia serikali imetenga kiasi gani kwa ajili ya utafiti juu ya Covid 19?, hakuna tafiti bila resource next time piga kelele juu ya uwezeshaji kwanza kabla hujashambulia vyuo vikuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…