Ni akili ama matope ? Unasomesha mtoto shule za ada kubwa anaishia kuwa Winga , sababu wewe mzazi huna kampuni wala biashara yoyote ya kumrithisha

Ni akili ama matope ? Unasomesha mtoto shule za ada kubwa anaishia kuwa Winga , sababu wewe mzazi huna kampuni wala biashara yoyote ya kumrithisha

Hakuna ajira ya ngazi za juu unapata kwa sababu umesoma EM ajira za ngazi za juu wenzako wamesoma nje ya nchi tena watoto wa wakubwa.

Wewe wa EM utaishia tamisemi huko, ukasaidie wananchi.Ukibahatika sana utapate kwenye vitaasisi vya serikali utakuwa middle income ila hamna kitu bado ni mtumwa tu maana hata kidumu na fagio wapo kibao level hizo.

CEO wa NMB ana umri unaofanana na umri wa TID.

CEO wa NMB amesoma shule za serikali. Kayumba kuanzia msingi mpaka chuo

TID kasoma shule za kulipia

Ila leo hii kayumba product ndie CEO wa bank kubwa huku shaban robert product TID anaunga unga anaishi kwao
 
Kuna dogo mtaani alikuwa anasomeshwa international school akiwa la kwanza baba ake ni mchaga ila mama ndio anakaza eti mtoto wampeleke international school basi siku za likizo akija na vingereza vyao vya kuunga unga mother anafurahi kweli mtaa wote wanavimba

Hawajafika mbali mtonyo ukakata wakamhamisha boarding za kawaida mtoto kaishia form two kaacha leo hii ukimkuta ni maharage ya mbeya kama wengine, sifa huwa hazisaidiii
Tatizo watu wanaigiza sana maisha yaani mtu unakuta ni middle income tu ila anavyovimba😄😄😄😄akiyumba kidogo tu chali.

Hao huwa wanajifunza wakati ukiwa umeshapita yanabakia majuto tu.
 
Matajiri wengi walianzia kazi ya Winga
Hizi ni ndoto za mchana msomi😄😄😄

Wakinga wanapiga uwinga huku kwao Iringa wameacha mashamba ya miti ya mbao na maparachichi. Anafanya uwinga kupata experience ya biashara ila anajua after sometime mtaji upo shamba ni swala la muda tu.Shtuka wenzako wanahesabu kali.
 
Nimekutana na Winga karikoo anatema ung'eng'e umenyooka. Baada ya kuzoeana nae. Akanipatia CV yake nimsaidie kusaka kazi.

Kucheki CV ya winga huyo wa karikoo naona primary kasoma St marys, O level kasoma Shaban robert, A level kasoma Feza. Chuo pekee ndio kasoma chuo cha kayumba Udsm.

Nikamuuliza kwa nini asiombe mtaji kwa wazazi wake maana wanaonekana wana uwezo.

Akanijibu wazazi Wake hawana hela wala chochote cha kuwapatia leo hii. maana Hela zao waliwekeza kwenye kusomesha watoto tu.

Hata nyumba yao ya kuishi haijakamilika mpaka leo hii sababu ya kusomesha
Usitafute kichaka Cha kujificha wewe peleka tu mtoto wako kayumba akadumishe uzalendo wa lugha ya kiswahili
 
Wanawake wengi wana hii mentality na kuwalazimisha waume zao kusomesha watoto shule za gharama

Hoja yao ni kuwa pesa zitatumika kwa michepuko mwisho wa siku mzee anashindwa kupanga list yake vizuri huku umaskini ukitamalaki kwenye familia
Hata hivyo kwani ni uongo kuwa pesa zinatumika kwa michepuko, wanaume mnaweza kuwaambia wake zenu hamna pesa kumbe huko nje mnahonga, halafu mkifilisika mnataka wake zenu ndio wawavumilie wakati huo hiyo michepuko mliyokuwa mkiihonga ishawakimbia
 
Mchepuko hauwezi kumaliza milion 4 kwa mwaka hata niwe nayo kumi

Sasa ada ya mtoto kwa mwaka ni shingapi kutaka kujimwambafai tu mtaani na nyie muonekane
 
wahindi na Wachaga wanasomesha watoto shule za gharama ila wanabalance wanamiliki na biashara za familia pia.

Ni upuuzi kuwekeza hela yote ya familia kwenye kusomesha tu
Sasa boss, Maelfu ya watu walioajiriwa kwenye ng'o na mashirika ya kimataifa, mabank na taasisi za fedha wamesoma shule za kata? Au hizo taasisi zinamilikiwa na wazazi wao?
 
Labda Nipo wrong,,,Ila sio wote wanaosoma feza wanamaisha mazur wengine wanakua na vipaj maalum wanapata scholarships,
 
Nimekutana na Winga karikoo anatema ung'eng'e umenyooka. Baada ya kuzoeana nae. Akanipatia CV yake nimsaidie kusaka kazi.

Kucheki CV ya winga huyo wa karikoo naona primary kasoma St marys, O level kasoma Shaban robert, A level kasoma Feza. Chuo pekee ndio kasoma chuo cha kayumba Udsm.

Nikamuuliza kwa nini asiombe mtaji kwa wazazi wake maana wanaonekana wana uwezo.

Akanijibu wazazi Wake hawana hela wala chochote cha kuwapatia leo hii. maana Hela zao waliwekeza kwenye kusomesha watoto tu.

Hata nyumba yao ya kuishi haijakamilika mpaka leo hii sababu ya kusomesha
Early grey
 
Ukweli mchungu ambao darasa la saba na form 4 wazamani watakuja kupinga😄😄😄😄

Kwa utafiti usio rasmi wengi wa waliosomesha vijana EM na wanaoendelea kusomesha watoto EM ni;

1. watu waliopata pesa kwa shida sana bila kuwa na elimu kubwa yaani darasa la saba na form 4 wa kayumba.Hawa wanakuwa na hali ya kutokujiamini(inferiority complex mfano ni Msukuma yule mbunge) wawapo mbele za hawa wasomi uchwara. Kwahiyo hasira zote za kuzarauliwa na wasomi uchwara wanapeleka watoto huko EM.

2.Middle class wa kibongo ambao hawana akili timamu ya kujua nini cha kuwekeza mwishowe unakuta hawana hata nyumba wala gari mpaka wanafikia kustaafu.

3.Malimbukeni wanaopenda mashindano na majirani wa mtaani kwao au ndugu zao.Hawa hawajui nini kinaitajika kwa dunia ya sasa wala hawana dira ya miaka 10 au 15 ijayo.Baada ya kusomesha watoto zao EM watarudi kulaumu serikali baadae kuwa wapewe ajira.

Kwa kifupi haya ndo makundi ya jamii ya watanzania watetezi wa EM na washabiki kindakindaki wa huu upotevu wa rasilimali.
100 percent fact
 
Kwa hiyo hoja Yako wazazi wasisomeshe?
Kwanini hujiulizi wazazi hao walimudu vipi kumlipia ada huyo dogo kwenye shule za gharama kubwa namna hiyo? Kwanini usidhani kuwa wazazi huenda walifilisika?

Maisha haya fundi ila ni mipango, utashangaa huyo dogo akapata ajira Tena ya ngazi za juu!

Tusilazimishe kujipa unafuu wa fikra kwa kuweka mbadala rahisi wa vitu. Kila mtu kwenye maisha ana ramani thabiti ambayo hudhihirishwa na Muda na Nafasi.
Mkuu wimbi la hizi nyuzi ni stress za ada 😆
 
Back
Top Bottom