Ni akina nani waliohukumiwa kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Mbowe kama alivyosema Rais Samia?

Ni akina nani waliohukumiwa kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Mbowe kama alivyosema Rais Samia?

Kila atakapofungua mdomo wake huyo wa vichokochoko ndiyo anazidi kujiingiza kwenye tope zito kujichomoa 😜 itakuwa shida sana. Kaamua kuukumbatia uongo na unafiki kwa nguvu zake zote hajui kama Watanzania tunaojitambua TUNAMZOOM tu na kumuona anavyozidi kujifanya kituko.
Nadhani Huyu Mama wabaya wake wamemlengesha ili aonekane kituko mbele ya jamii. Nae vile wakusinzia anadhani anapendwa kumbe makukuru tiyari washampigia hesabu.
 
Inawezekana hiyo press Rais hakujiandaa nayo, amekurupushwa akaenda, naona kila swali aliloulizwa amekosea kujibu, hana uhakika na kila alichozungumzia.

Atakuwa alijiandaa na kuandaliwa kweri kweri. Uwezo wake na uwezo wao ndipo ulipoishia.

Yule wa kifo cha Azory kwani naye ilikuwa je?

BBC siyo TBC.

Njia ya mwongo haijawahi kuwa ndefu.
 
..Maza anajaribu kumdanganya Salum Kikeke, ambaye anaishi ulaya, kuhusu maandamano yanayofanyika ulaya.🤣🤣

Ulaya ambako chaguzi hutokea kutokana na utawala uliopo unaposhindwa kutatua changamoto zilizopo.

Anataka kumwaminisha nani kuwa Ulaya yote chaguzi ni preset kila baada ya miaka fulani?
 
Please, respect our Head of State...Huna adabu wewe!

Kumtusi Rais ni kutukana watanzania wote; inamaana sisi tuliopiga kura kumweka kama Makamu wa Rais ambaye ni Rais in waiting hatukua akili....

Kwanini mnapenda provocation?

Namba ya simu umesahau jombi
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mkuu,

Mbona unajichanganya?

Si unapigania serikali TATU sio? Ni kitu gani na kitu ukijumlisha kinaleta TATU?

Wanaodai serikali MBILI iendelee wanatoa sababu ya kihesabu kwamba 1 jumlisha moja ni MBILI

Je Ngapi jumlisha ngapi upate TATU?

Tanganyika HURU=1

Zanzibar HURU=1

Tan-Zan......(Kimalizio ni kifupi cha jina la mtu binafsi na dini yake)

IA.......Iqbal+Ahmadiya

Tan-Zan-IA (Mmiliki halali wa jina la Tanzania ni MOHAMMED IQBAL DAR muumini wa dini ya AHMADIYA MUSLIM JAMAAT)

Nchi hii imepatikana kimaajabu, watu wake ni waajabu na matukio ya yanayoendelea kutokea ni ya adabu, mauzauza na giza tupu

Mwanzilishi wa jina hili ni mstaarabu wa kiwango cha juu sana vinginevyo angedaia haki yake mpaka kwenye mahakama za kimataifa ikiwemo kusudio la kumilikishwa nchi na kuabudiwa kama mwenye mali

Wananchi msigombane bure nchi hii siyo yenu ina mwenyewe kwahiyo unapojitwika jeuri kwamba lazima ni dai hili ama lile litekelezwe ni ajabu maana hata viongozi inawabidi kutii masharti na kiapo wanachokutana nacho ambacho wewe na mimi ambao hatujawahi kuingia kwenye tanuru la jumba la kiutawala wa nchi kushuhudia hivyo madai yoyote ukianzisha yatakuwa hewa na ukishupaza shingo utavunjika.
Heri wewe unayemjua mwanzilishi wa jina la Tanzania ambalo lilikuja baadaye sana baada ya Aprili 26, 1964. Kabla ya jina hilo muungano uliendelea kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa miezi kadhaa

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Mtuhumiwa wa ugaidi alikimbilia Nairobi ila uchaguzi ulipofika akarudi kufanya kampeni mpaka mwisho na baada ya hapo ndio jeshi la polisi likamshika. Kweli jeshi la polisi lina adabu kwa watuhumiwa wa ugaidi.
 
Please, respect our Head of State...Huna adabu wewe!

Kumtusi Rais ni kutukana watanzania wote; inamaana sisi tuliopiga kura kumweka kama Makamu wa Rais ambaye ni Rais in waiting hatukua akili....

Kwanini mnapenda provocation?
Wewe ulimpigia kura Mama lini? Lakini pia, kama ulipiga kura, halafu ukachagua vibaya, kwa sababu hukuwa na uelewa sahihi, kuna ubaya gani ukijiita huna akili? Mimi naona ni sawa tu, kama kura yako inazingua.
 
Respect is ALWAYS a TWO WAY TRAFFIC. Provocation!? Who is provocating who? Wewe babaako angekuwa yuko ndani kwa ushahidi FEKI ungeandika upuuzi kama huu!? Au mkuki ni kwa nguruwe!? 😳😳😳
Huyo naye amebaki na tu-akili twa kuendea msalani asijigonge ukutani tu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Namba hazijawahi kudanganya, kwa mujibu hati ya mashitaka ,Mbowe ameshitakiwa pamoja na wenzake watatu, kwa mashitaka kadhaa huku Mbowe akikabiliwa na mashtaka mawili, hawa wote wako rumande na kesi yao inaendelea .

Nukuu
Rais Samia: Mimi sidhani kama yamechochewa kisiasa kwasababu navyojua Mbowe alifunguliwa Kesi mwezi wa Tisa mwaka jana (2020), kwa hiyo yeye pamoja na wengine na kama ulivyosema mashtaka ni ugaidi na kuhujumu uchumi. Nadhani wenziwe kesi zao zimesikilizwa na wengine wameshapewa sentence zao wanatumikia. Yeye (Mbowe) upelelezi ulikuwa haujeisha, uchunguzi ulikuwa unaendelea so amekwenda amefanya tumeingia kwenye uchaguzi, amemaliza uchaguzi nadhani sasa Polisi wamekamilisha uchunguzi wao, wamemuhitaji waendelee na kazi yao.

Sasa hao wengine ambao Mtukufu Rais Samia anadai walikwishahukumiwa ni akina nani na wako wangapi na wako gereza gani?
Kama Mbowe alishtakiwa tangu mwaka Jana, ikawaje polisi waende kumkamata saa nane za usiku na kumuweka mahabusu? Tunajua wazi Kama tayari alikua na kesi, kwa mujibu was rais, basi angeitwa tuu na mahakama akahudhurie kesi yake. Rais ametudanganya?
 
1 Wafalme 12:
1 Rehoboamu akaenda Shekemu; maana Israeli wote walikuwa wamekwenda Shekemu, ili kumfanya mfalme.

2 Ikawa Yeroboamu mwana wa Nebati alipopata habari (maana alikuwa akaliko Misri, huko alikokimbilia awe mbali na mfalme Sulemani; Yeroboamu akakaa huko Misri,

3 wakapeleka watu kwenda kumwita); basi Yeroboamu na jamii yote ya Israeli wakaenda, wakamwambia Rehoboamu, wakasema,

4 Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa utupunguzie utumwa mzito tuliotumikishwa na baba yako, na lile kongwa zito alilotutwika, nasi tutakutumikia.

5 Akawaambia, Enendeni zenu hata siku ya tatu, kisha mnirudie tena. Watu wakaenda zao.

6 Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee waliokuwa wakisimama mbele ya Sulemani, baba yake, alipokuwa hai, akasema, Mwanipa shauri gani ili niwajibu watu hawa?

7 Wakamwambia wakasema, Ukikubali kuwa mtumishi wa watu hawa leo, na kuwatumikia, na kuwajibu, na kuwapa maneno mazuri, basi watakuwa watumishi wako daima.

8 Lakini akaliacha shauri lile la wazee, walilompa, akataka shauri kwa wale vijana waliokua pamoja naye, na kusimama mbele yake.

9 Akawaambia, Mwanipa shauri gani ili tuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakinena Utufanyie jepesi kongwa lile alilotutwika baba yako?

10 Na wale vijana waliokua pamoja naye wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliokuambia, wakisema, Baba yako alilifanya zito kongwa letu, bali wewe utufanyie jepesi, uwaambie hivi, Kidole changu cha mwisho ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.

11 Basi kama vile baba yangu alivyowatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, bali mimi nitawapigeni kwa nge.

12 Basi, Yeroboamu na watu wote wakamfikia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu.

13 Mfalme akawajibu watu wale kwa ukali, akaliacha shauri lile wazee walilompa;

14 akawajibu kama vile walivyomshauri vijana, akasema, Baba yangu alilifanya zito kongwa lenu, bali mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, bali mimi nitawapigeni kwa nge.

15 Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa BWANA, ili alitimize neno lake, BWANA alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa kinywa cha Ahiya Mshiloni.

16 Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hakuwasikia, hao watu walimjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya! Nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi. Hivyo Israeli wakaenda zao hemani kwao.
 
Namba hazijawahi kudanganya, kwa mujibu hati ya mashitaka ,Mbowe ameshitakiwa pamoja na wenzake watatu, kwa mashitaka kadhaa huku Mbowe akikabiliwa na mashtaka mawili, hawa wote wako rumande na kesi yao inaendelea .

Nukuu
Rais Samia: Mimi sidhani kama yamechochewa kisiasa kwasababu navyojua Mbowe alifunguliwa Kesi mwezi wa Tisa mwaka jana (2020), kwa hiyo yeye pamoja na wengine na kama ulivyosema mashtaka ni ugaidi na kuhujumu uchumi. Nadhani wenziwe kesi zao zimesikilizwa na wengine wameshapewa sentence zao wanatumikia. Yeye (Mbowe) upelelezi ulikuwa haujeisha, uchunguzi ulikuwa unaendelea so amekwenda amefanya tumeingia kwenye uchaguzi, amemaliza uchaguzi nadhani sasa Polisi wamekamilisha uchunguzi wao, wamemuhitaji waendelee na kazi yao.

Sasa hao wengine ambao Mtukufu Rais Samia anadai walikwishahukumiwa ni akina nani na wako wangapi na wako gereza gani?
Umeniudhi kumwita mtukufu... ana utukufu gani?
 
Back
Top Bottom