GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
- Thread starter
- #41
Hata Introvert akiamua kuuiga uetrovert, "mtaalam" wa Saikolojia atamgundua tu.Introvet raha sana. Unapiga zako gambe unatulia. Pia unapata muda wa kuwazua mambo, siku hizi nimejifunza kitu nikiwa na jambo gumu nalipa muda nakaa ata siku tatu silifikirii.
Kumbe akili inaliwazua bila mimi kujua mwisho wa siku nashangaa nakuja na solution ya ajabu sana kila mtu anabaki mdomo wazi.
Napenda usiri japo siku hizi nimeiba tabia za extrovet najichanganya na kusalimia kila mtu maeneo ya kazi but baada ya hapo napotea kujichimbia kwa computer. Kuna muda nahisi siko introvet 100%. Sababu pia naweza kudanganya sana ila kwa kutumia akili, natabia ya wasiwasi sipendi kuacha alama kwenye harakati zangu.
Napenda kutumia majina bandia sitaki mtu ajue jina langu halisi na hii ni tokea nikiwa sekondari mpaka sasa wanaojua jina langu halisi ni wachache. Miaka ya hivi karibuni ndio nimeanza tena kutumia jina langu halisi baada ya kuhama mazingira. Inshort kila mtaa niliokaa nilitumia jina tofauti.....NB: SIJAWAHI KUTAPELI WALA KUIBA CHA MTU ILIKUWA NASIKIA FURAHA TU KUWA MTU BANDIA
Nakipaji cha kuandika na kuchakata maneno, naweza kusoma matamshi ya sauti ya mtu na kujua hatua itakayofuata. Naweza kuonana na mtu kwa dakika chache nikaandika historia yake kwa usahihi 70% na kuweza kubashiri kesho yake kwa 60%.
Wewe ni "typical Introvert!"
Na kwa jinsi walivyo na "akili nyingi", wakiamua kudanganya au kuwa wahalifu wanaweza wakafanikiwa kuufanikisha uovu bila kufahamika kwa sababu ya ya tabia zao za kutokufanya jambo kwa kukurupuka.
Ila hongera kwa kuwa unautumia uintrovert wako kwa manufaa👏👏👏