Ni basi gani uliwahi panda ukajuta na ukasema hutokaa ulipande tena?

Ni basi gani uliwahi panda ukajuta na ukasema hutokaa ulipande tena?

Mm huku nilipo magari yote ni ngarangara tu na hakuna options maana njia bado ni ya vumbi. Unaingia kwenye bus tu unakaribishwa na vichambo vya konda, unakuta konda na dereva wote washachafukwa ni full matusi tu na vichambo.
Gari kuharibikia njiani huku sio ajabu, gari kuzama ndio balaa. Kufika town uko mwekundu sio ajabu, unashuka stend abiria wanakushangaa[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Kuna mabus Fulani yalikuwa nayaenda kusini enzi hizo yanaitwa AKIDA aisee ilikuwa balaa Kwanza kabisa Siri zote zimefungwa na kamba alafu ngumu kama unazo ikinyesha mvua ndani mnaloa kama umejicha mvua chini ya mwembe yaani shida Tu..
Bus haina tyres spare wala jeki na kila baada ya km kadhaa wanaziba pancha nilishuhudia Kwa mara ya Kwanza engine inawashwa Kwa kutumia body spray (ilikuwa inapulizwa kule kwenye nozzles ili kurahisisha mlipuko kwenye engine)

Mabus ya zamani ilikuwa ni vita hata ule msemo WA "msafiri kafiri" walikuwa sahihi kabisaa!!!
 
Haujawahi kupanda mabasi ya mwanza ee[emoji23][emoji23]movie za mkojani hazijawahi kukosekana.
Kwa mabasi niliyoyapanda kwangu yote ni mazuri kwa safari.
Tanzanite kabla hazijaamia mbeya,Ally’s no 1,Zuberi na mwisho ni Travel Partners yote haya kwangu ni mazuri sana tatizo ni movie za mkojani tu kha
Nilishawahi kupanda Ally's ya Tanga To Mwanza nilitoka nilipandia Arusha kwenda Kahama
 
Mm huku nilipo magari yote ni ngarangara tu na hakuna options maana njia bado ni ya vumbi. Unaingia kwenye bus tu unakaribishwa na vichambo vya konda, unakuta konda na dereva wote washachafukwa ni full matusi tu na vichambo.
Gari kuharibikia njiani huku sio ajabu, gari kuzama ndio balaa. Kufika town uko mwekundu sio ajabu, unashuka stend abiria wanakushangaa[emoji28][emoji28][emoji28]
Wapo huko mkuu
 
Daah umenikumbusha mbali sana, kuna basi lilikua na nembo kubwa "Pride of Mwanza" Super Najimunisa. Wakati huo magari mengi yakiwa yanatoboa Mwanza kutoka Dar mida ya saa tatu, saa nne, sisi tulifika siku ya pili yake saa nane, tukiwa hoi kama wana wa Israel.
 
ABC Dar iringa...Nilijuta nikajuta.
Kwanza gari haitembe na nilikua nawah kikao iringa
Pili wanaingia pale cate hotel (za kwao) chakula cha kawaidaaaa ila gharama juu
Tatu ile tent kubwa ya kulia chakula pale juu inapitisha kali kinoma imagine unakula juan kama uko msibani uswahilini tandika..
Gari ina choo ndan ila usafi shida harufu.

NILIVYOSHUKA NIKASEMA LEO MWANZO NA MWISHO
 
Back
Top Bottom