ngaboru
JF-Expert Member
- Mar 3, 2016
- 2,069
- 5,411
1.3m inatosha Kwa kuazia kweli
Inategemea uko wap ukijitoa akili hela unapata cha msingi ni uuze kila kitu kuanzia vinywaji vya kuongeza nguvu,bia,soda maitaji ya nyumbani...kua na viti viwili vya plastic hapo nje ya duka...
Alafu mbele ya duka lako weka genge kuanzia nynya mpaka nazi uwe nazo...
Hapo hapo asbh(kuanzia saa 4 ivi maana mapema yake unaenda kuchukua mzigo) kaanga mihogo inafaida kwa pembeni hapo alafu jioni warostie chips na ndizi na mishkaki ukimaliza kaanga maandazi ya asbh.😂😂😂😂😂
hapa mtaani kwetu kuna mmama ndio mapambano yake na bado mauchafu yote yanayobaki anachemshia nguruwe zake.
Kama unataka pesa ni kujilipua na kutokujionea huruma kuwai kuamka kuchelewa kulala baada ya muda flani unaanza kuajiri.
Mi namkubali sanaa ndio ma iron lady hawa na naamini mambo makubwa na mazuri yako mbele n suala la muda tuu.