Sasa mkuu wewe unaleta utani na maisha watu tupo mtaani tumepigika, siunaona mtu kaanzisha uzi kama hivi! Maana yake anahitaji msaada, pia wengine wanafaidika kupitia michango ya mawazo inayotolewa,
Unaposema unabiashara ya mtaji mdogo na inakupa faida kubwa, na huisemi, mtu anaona kama unambania au kumnyanyasa kisaikolojia, unatuongezea maumivu mkuu ujue watu tumewahi kwenda kuomba kazi kwenye makampuni ya wageni tukazuiliwa kuingia ndani na wabongo wenzetu,ma secretary wanachana na kutupa barua za maombi ya kazi kwenye dustbin. Kiufupi tunapitia mengi sana mpaka tumejawa na stress inafikia point tunajikuta tukikutana na mtu anayekunyima mchongo kama hivi unakumbuka maumivu yote uliyopitia ya kunyanyaswa na wabongo wenzetu.
Nisamehe sana mkuu niliandika kwa makosa na hasira tu zinazotokana na stress I'm sorry [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Nikuombe kitu kimoja siku nyingine ukitaka kutusaidia ficha location yako alafu eleza wazo lako ili kulinda maslahi yako kama anavyofanya
CONTROLA, wengi tutanufaika na Mungu atakubariki [emoji120][emoji120]